kwa rugha nyepesi, sayansi ni mfumo wa kufikiri.
Jibu lako, kama mimi ni mwalimu, nasahihisha mtihani, nakupa kosa.
Kwa jibu hili, umejionesha hujui hata sayansi ni nini.
Jibu lako halijaweza kui define sayansi kwa namna ambayo itaeleweka kuwa tofauti na mfumo mwingine wowote wa kufikiri ambao haupo kisayansi.
Ni hivi, ukisema "sayansi ni mfumo wa kufikiri" hujaitenganisha sayansi na mfumo mwingine wa kufikiri unaosema kwamba kila kitu kinatokea kwa kudura za Mungu tu, yote hiyo ni mifumo ya kufikiri, lakini yote si sayansi.
Yani, nikikuuliza "Mbantu ni nani?". Ukanijibu "Mbantu ni mtu". Sawa, ni mtu. Lakini hata Muarabu ni mtu, Mzungu ni mtu, m Nilotic ni mtu, Mchina ni mtu, Muhindi ni mtu. Hivyo, jibu lako kuwa "Mbantu ni mtu" halijaweka the defining characteristic inayomfanya Mbantu kuwa Mbantu, kwa sababu unaweza kuwa mtu bila kuwa Mbantu.
Ni kama vile umeulizwa "muziki ni nini?" Ukajibu, "muziki ni sauti". Sawa, lakini jibu lako haliutofautishi muziki na kelele nyingine yoyote isiyo muziki ambayo ni sauti pia.
Kuna tatizo la kuelewa sayansi ni nini - au kujielezea vizuri, labda unaelewa ila unashindwa kujielezea.
Na kama kuna tatizo la kuelewa sayansi ni nini, au kuelezea sayansi ni nini, huko kwingine kwenye maswali yasiyo na hoja kama vile "Mbona sayansi imeshindwa kuelezea kifo" tutashindwa kuelewana.
Mtu asiyeelewa sayansi ni nini, ni vigumu sana kuelewa si tu kwamba sayansi imeshaelezea kifo, bali pia, hata sayansi ikishindwa kuelezea kifo leo, hilo si tatizo, kwa sababu sayansi haijawahi kudai kwamba ina majibu ya kila kitu leo.
Waamini wa Mungu wanafanya kosa moja la kutaka kuifanya sayansi kuwa mbadala wa Mungu. Kwamba, kuna Mungu huyu ana majibu ya kila kitu, na ukitaka kumuondoa Mungu huyu useme hayupo, ukatuletea dunia ambayo tunapata majibu kwenye sayansi, basi ni lazima sayansi nayo iwe na majibu ya kila kitu, leo.
Sayansi haijawahi kusema kwamba ina majibu ya kila kitu leo. Inaenda kwa observation, experiments, peer review, na inakubali kwamba haina majibu ya kila kitu leo, watu wanachunguza wapate majibu.
Kwa nini watu wanalazimisha sayansi iwe na majibu ya kila kitu leo wakati huu ni mchakato wa watu, mchakato endelevu, na ambao haujawahi kudai kuwa una majibu ya kila kitu leo?
Hivi, haiwezekani Mungu akawa hayupo na sayansi ikawa pia haina majibu kamili leo?
Mimi naweza kusema kwamba, siyo tu inawezekana kuwa Mungu hayupo nabsayansi haina majibu kamili, naenda mbali zaidi na kusema, kwa sababu Mungu hayupo ndiyo maana sayansi haina majibu kamili kwenye kila kitu leo.
Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote, kwa sifa zake hizo, angekuwepo, angetufanya tuwe na sayansi yenye majibu yote leo, kwenye kila kitu.
Sasa basi, ukiikosoa sayansi, kwamba haina majibu ya kila kitu, unaweza kujiona unapandisha umuhimu wa Mungu, wakati kiukweli, kwa ntu anayefikiri kwa kina, ukiikosoa sayansi kwamba haina majibu ya kila kitu, unazidi kuthibitisha Mungu hayupo.
Huyo Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote nabupendo wote angekuwapo, angetupa sayansi yenye majibu ya kila kitu. Mungu huyo si mchoyo hivyo aachie mamilioni ya watu wafe kwa bacteria kwa maelfu ya miaka mpaka tuje kugundua kutengeneza antibiotics mwaka 1928 tu hapa.
Yani unakubalije Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote anaweza kuwapo halafu akawa na roho mbaya hivyo kwa kitu ambacho yeye hakimgharimu lolote na sisi kitatufaidisha sana?