Dini rasmi inaitwa the Omnitheistic Singularity jina la Mungu na kitabu kikuu ni Omnipotent Singularity. Imeandaliwa na IIT

Aliyesoma page 39 anawezaje kukurupuka? Endelea kubisha ila jua matango pori mengi sana kwenye hiyo dini yako
 
Unajua, dini nyingi zinafanana na taasisi za kukusanya fedha

Uliposema mliona mapungufu ya dini nyingine kuhusu suala la sadaka, nilidhani labda mnataka kuja na maboresho, kwa mfano, kuunda mfumo wa kusaidiana na kuinua waumini kiuchumi na kufanya muumini anufaike

Kumbe mmeweka hata mhasibu wa kufuatilia mapato na matumizi? 😂

Sasa hizo sadaka mtakuwa mnapeleka wapi?
Maana kanisani na msikitini wana vifungu vyao vya matumizi
Na wana maandiko yao yahusu sadaka na sijui fungu la kumi sijui zaka nyie huu mfumo mmeuotoa wapi huoni mna copy na ku paste

Hilo suala la sadaka kwenye dini yenu limetoka wapi? Huoni kwamba bado mnarudi kule kule mlikokosoa kwenye dini nyingine?

Na je, kwenye dini yenu mna utaratibu wa kufanya maombi?
 
Aliyesoma page 39 anawezaje kukurupuka? Endelea kubisha ila jua matango pori mengi sana kwenye hiyo dini yako
Mkuu, kama tayari unaamini kuwa haya ni 'matango pori', inashangaza kidogo kuona umepoteza muda wako wa thamani na umakini mkubwa kusoma hadi kufikia ukurasa wa 39! Huwa hatupotezi muda kusoma vitu visivyo na maana. Ukweli ni kwamba mada imekuvutia na imekuchochea kufikiri, na ndiyo maana bado upo hapa. Karibu uendelee kusoma mkuu, ila kama imekushinda, ruhusu wengine wenye kiu ya maarifa waendelee na mjadala.
 
Inasikitisha sana kuona uwezo wako wa kufikiri umeishia hapo. Yaani uwepo wa 'Mhasibu' kwako unamaanisha kukusanya fedha tu? da
Hivi akili yako haijawahi kuwaza kuwa taasisi yoyote makini inayotaka kuwasaidia watu kiuchumi, kujenga miradi, na kujiendesha kwa uwazi lazima iwe na mfumo wa kifedha na mhasibu wa kudhibiti matumizi? Ama ulitaka tuweke waganga wa kienyeji wanaoagua mifuko ya watu kwa ramli?
Kuhusu mfumo wa sadaka na maombi, usikariri kuwa kila anayeomba au kuchangia anacopy kanisani au msikitini. Binadamu tangu enzi za giza, kabla hata hujaanza kuota hizo dini unazozijua leo, walikuwa wanatoa dhabihu na kufanya matambiko (maombi) kwa nguvu kubwa inayoendesha ulimwengu. Sisi tumerudisha maana halisi ya kiroho na kiutawala, hatujacopy biashara za watu. Pole sana kama uwepo wa mhasibu umekunyima usingizi, ila pole zaidi kwa sababu ndio kwanza safari inaanza.
 
Mwalimu mzuri ni yule anayechimba kwa manufaa yake na wanafunzi anaowafundisha, nisingepata nguvu ya kukueleza ukweli kama nisingesoma hicho kitabu cha page 39. Kusoma page zote haimaanishi kilinivutia sana, kama unakumbuka nilikusubiri ukitoe na ukanitag baada ya kukirusha.
 
Huwezi kujenga hoja bila ku attack mtu ? nina wasi wasi na uwezo wako

Jenga hoja
Tetea hoja yako

Nimekuuliza swali kama umeona sina uwezo mkubwa kufikiri basi ilibidi unieleweshe
Bahati mbaya una hasira kali
 
Mkuu, naona unaweweseka unataka kunipeleka mbeleni wakati hata hatua ya kwanza hujavuka! Nilichoweka hapa ni kitabu cha kwanza (1) tu kati ya vitabu 7,312 vilivyopo kwenye hii dini yetu. Hayo maswali yote unayouliza kuhusu mifumo ya maombi, namna ya kusoma Kitabu Kikuu, mavazi rasmi, maneno ya kusema, na mbinu za kufungua uelewa yamefafanuliwa kwa kina huko mbele.


Hivi hujaona tamko rasmi hapo juu? Hebu tulia, punguza viwewe, na usome kwanza ulichopewa hapa ili ukikosoe kwa hoja badala ya kukurupuka kuulizia yaliyoko mbele wakati ya sasa hujayaelewa. Soma kwanza kilichopo mbele yako sasa hivi mkuu
 
Nimeuliza yaliyo mbele basi akili yangu ipo mbele ya muda

Lakini nakukumbusha tu nimeuliza kulingana na ulicho ni quote
Kwahiyo sijakurupuka

Nakukumbusha tena ili kufanikiwa kwa huu mpango wako inabidi ujifunze namna ya ku interact kwa sababu unaitaji watu na watu wenyewe ndio sisi
 
sawa hongera
 
Unatumia nguvu kubwa kuandika vitu ambavyo havina tija kwa jamii
Mtu mwenye akili timamu hawezi kusoma hizo takataka.
 
Huwezi kujenga hoja bila ku attack mtu ? nina wasi wasi na uwezo wako

Jenga hoja
Tetea hoja yako

Nimekuuliza swali kama umeona sina uwezo mkubwa kufikiri basi ilibidi unieleweshe
Bahati mbaya una hasira kali
Mkuu, jinsi unavyokuja ndivyo unavyopokelewa hiyo ndiyo kanuni ya msingi ya hapa. Kama ungekuja kwa nia safi ya kujifunza na kutafuta maarifa bila kashfa za 'matango pori' au dhihaka za kukusanya fedha, ungepokelewa kwa lugha ya upole na maelekezo ya kina. Huwezi kurusha mawe kisha ukashangaa ukirushiwa magongo, halafu ukasingizia mwenzako ana hasira. Ajiulize ni kwa nini wewe tu ndiye unayejibiwa hivi na sio wengine wanaochangia kwa staha? Hapa hakuna hasira, kuna kurudisha kile ulichokileta. Kama sasa umeamua kuwa mstaarabu na unataka kujenga hoja, badilika, tulia, na usome ulichopewa badala ya kulalamika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…