Dini zina maelezo gani kuhusu binadamu wa jamii tofauti kuwa na rangi tofauti?

Qurani inasema rangi za binadamu wengine kuwa weusi(Waafrika), wazungu, Waarabu, Wachina, Wahindi, Wahindi wekundu n.k ilitokeaje ?
Mchakato gani mungu aliufanya au ulitokea kulingana na dini yako hadi binadamu wakawa tofauti hivi??
 
Mbona au ulizi kuhusu mimea, wanyama na ndege?

Tunatofautiana nini navyo?

Mbona kuna aina mbalimbali za michicha? Au kuna ng'ombe wa nyama na yule wa maziwa?
Au njiwa pori na njiwa wa kufugwa?
 
Hii ni kisayansi au kidini? Rejea swali la mtoa mada
 
Kila kitu kiko wazi kwenye hili, huoni Simba wa porini siku hizi Anaishi na Watu?
Si inalazimishwa tu, unadhani hata wale wanaofuga nyoka huwa hayawakuti ya kuwakuta? Hung'atwa sana tu na kufa kabisa.

Huoni hata samaki wa kufugwa jinsi gani hawana ladha kabisa za minofu kuliko samaki asilia toka mitoni na baharini?

Ubinadamu ni kazi/the humanity is work.
 
Hayo maelezo yanaelezewa na wanasayansi. Je, dini ina maelezo yapi katika eneo hilo?
Nililenga kumjibu aliyeuliza kwa nini afro american hawajabadilika. Dini inatofautisha jamii kwa kutumia maneno kama ''watu wa mataifa'' eg
“Katika hao nchi za mataifa ya pwani ziligawanyika katika nchi zao, kila mtu kwa lugha yake, kwa jamaa zao, katika mataifa yao.”
— Mwanzo 10:5
 
Hii ni Sayansi nyepesi sana,
Domestication of animals.
Hakuna kitu kama hicho, vitu vyote vilikuwa programmed na nguvu yenyewe "Mungu" je kwanini pawepo na mpaka wa wewe kuishi katika sayari zingine, je migawanyiko ya oksijeni, carbon dioxide nazo hazikuwa programmed?

Ubinadamu ni kazi/the humanity is work.
 
Wakati natafakari swali lako kwa kina hakika Mungu amenipa jibu lifuatalo. Tofauti za rangi na nywele zimetokana na kuzaliana kwa wanadamu wa kwanza baada ya uumbaji.

Biblia inaonyesha kwamba wanadamu walitokana na familia ya kwanza na wakaendelea kuongezeka kwa kuzaliana:
Mwanzo 1:28, Mungu aliwaambia, “Zaeni, mkaongezeke…”
Mwanzo 5:4, Adamu alikuwa na “wana na binti.”
Matendo 17:26, Mungu “alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika mmoja.”
Kwa hiyo, wazo kwamba tofauti za kimaumbile zilienea na kuonekana katika vizazi vilivyofuata kupitia urithi na kuzaliana linaweza kueleweka vizuri. Kisayansi pia, mtoto hupokea mchanganyiko wa vinasaba kutoka kwa wazazi wake; vinasaba hivyo vinaathiri kiasi cha melanini, aina ya nywele, rangi ya macho na sifa nyingine.

Swali la kujiuliza labda Adamu na Hawa walikuwa na uwezo gani wa kijenetiki uliowezesha vizazi vyao kutoa watu wenye ngozi na nywele tofauti sana? Hapo ndipo genetics inaweza kusaidia sana kuelezea hoja hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…