Nikifa MkeWangu Asiolewe
JF-Expert Member
- Feb 26, 2024
- 6,944
- 14,351
Wakuu Mimi Bado Kuna vitu Huwa najiuliza na mara zote sijawahi kupata majibu!
Hapa Duniani tuna dini aina tofauti tofauti na madhehebu Hali kadharika. Na dini zote/Imani zote na madhehebu yote Yana hubiri uzima wa milele baada ya kifo hii hata Mimi naamini kuwa Kuna maisha baada ya kifo/ufufuo.
Kinacho nipa ukakasi ni namna tunavyozikana. Wote hapa mmewahi hudhuria ibada ya mazishi kati ya dini2 ama zaidi bila shaka uliona utofauti mkubwa.
MFANO:-Roman catholic tuna kawaida ibada ya misa na Ibada ya kawaida ya mazishi na tukifika kaburini.
Basi kiongozi wa dini awe ketekista au padre atanyunyiza maji ya baraka kwenye kaburi lile ama ubani utachomwa na maombi kadhaa wa kadhaa.
Baada ya hapo tutafukia kabuli iwe Kwa zege ama kawaida then Tena maji ya baraka yatanyunyizwa pale juu na mishumaa kadhaa itawashwa(sio mara zote) mwisho pale juu tutaweka alama ya msalaba na badae msalaba wa mbao/chuma.
Ukija wa Kwa wahindu kama sikosei wao sitaelezea sana ila wao maiti huchomwa moto na kuwa majivu kabisa kama sikosei hawaziki(wenye dini yenu mtatusaidia Kwa kina)
Niliwahi kuambiwa baada ya kuchomwa moto Ile maiti basi majivu mengine hutupwa baharini na mengine kuhifadhiwa Kwa ajiri ya ndg walioko mbali mfano India,Canada Qatar nk hupelekewa Kwa njia ya ndege (Sina uhakika)
Ukija Kwa ndg zetu katika imani waislamu wao nao Wana namna Yao. Hata Uchimbaji wa kaburi ni tofauti na wetu wakristo kaburi litachimbwa lakini mwisho katachimbwa Tena kashimo kadogo na maiti hulazwa kiubavu kama sikosei maana Huwa wanajifunika Wakati wa mazishi Yao.
Utasikia wanaagiza lete kisu,lete mawe,lete mbao na nyasi.then watafukia na kusali Dua kadhaa wa kadhaa.
Mifano hapo juu ni michache sana
Sijasema walokole wasabato nk
Lengo nikutaka kujua yapi mazishi sahihi basi ambayo ukifanyiwa basi uhakika wa kuiona pepo ama mbingu ni 70% ukiachana na matendo Yako kabla hujafa.
Ukizingatia waislamu wao hawatumii kabisa jeneza kamwe na hajawahi tokea hata Kwa bahati mbaya uwe tajiri uwe masikini makabuli daima Huwa yanalingana lingana tu Kwa mwonekano ni tofauti na sisi wakristo ambapo Kwa kibosile utajuwa wazi kuwa huyu jamaa alikuwa nazo.
Nje na mazishi na Dua Wakati mazishi Kuna Hawa watu hufa na maiti zao kutokuonekana kabisa.
MFANO akina Ben sanane nk walipotezwa Hadi Leo hii sidhani kama ndg wamewahi kufanya ibada maalumu ya kumuombea kama kafariki maana hawana walijualo kama yupo hai ama kafa.
Video ni mtu maarufu hapo Kenya wa Mombasa Cement alivyozikwa Kwa kuchomwa moto.
Unaweza ingia YouTube kuangalia ibada yote Hadi maiti kuchomwa Kwa kuandika Mombasa Cement funeral.
View attachment 3179686