BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 706
- 1,716
Kwa miongo kadhaa, Tanzania imejengwa na kutambulika kama moja ya shule bora za diplomasia barani Afrika. Kuanzia harakati za ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika, ushiriki thabiti katika Umoja wa Mataifa, hadi kusimama kama taifa lisilofungamana na upande, Tanzania iliweka alama yake kimataifa.
Majina kama Benjamin Mkapa, Augustine Mahiga, Asha-Rose Migiro, Bernard Membe, Jakaya Kiikwete na wengine wengi yalileta hadhi na uzito wa kimataifa kutokana na uwezo wao wa kuunganisha hoja, kuongoza majadiliano nyeti, na kuendeleza diplomasia ya Tanzania kwa ustaarabu na weledi.
Hata hivyo, katika miaka ya karibuni, taswira hii inaonekana kuingia kwenye sintofahamu. Matukio mbalimbali, hasa kabla na baada ya chaguzi, yameifanya Tanzania kuonekana kwenye uwanja wa kimataifa kupitia matukio yenye maudhui hasi ya kukosolewa, kuonywa au kutahadharishwa na jumuiya za kimataifa.
Hii imetoa taswira tofauti na ile ya Tanzania iliyowahi kutambulika kama sauti ya busara na msimamizi wa amani katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Awali moja ya dalili zilizoibua mjadala mpana ni mzunguko wa haraka wa mawaziri wa Mambo ya Nje katika kipindi cha miaka mitano iliyopita. Wizara hii ni mhimili mkuu wa diplomasia, hivyo mabadiliko ya mara kwa mara yanaathiri mwendelezo wa sera, ujenzi wa mikakati ya muda mrefu, na uimara wa mahusiano ya kimataifa.
Dunia ya diplomasia inategemea uthabiti wa uongozi, kumbukumbu ya kihistoria na misimamo inayoendelea. Mabadiliko ya mara kwa mara utabiliwa kuwa yanaweza kuashiria kutokuwa na mwelekeo thabiti.
Pia, imeonekana mara kwa mara kwamba baadhi ya misimamo ya kidiplomasia imechukuliwa kwa mtazamo wa kisiasa wa ndani kuliko maslahi mapana ya kimataifa.
Badala ya hoja zenye nguvu, za kimkakati na zilizoandaliwa kwa lugha ya ushawishi, matamko fulani yameegemea kwenye utetezi, hisia au maelezo yasiyozingatia athari za muda mrefu. Katika eneo la kidiplomasia, lugha na mantiki huwa na uzito mkubwa; hoja dhaifu huathiri taswira ya taifa kwa kasi kuliko hoja nzito zinavyojenga.
Swali muhimu linaibuka: Je, Tanzania imeishiwa wanadiplomasia wabobezi.
Kumekuwepo na tafakari na wasiwasi kwamba kizazi cha wanadiplomasia mahiri waliolelewa katika misingi ya Mwalimu Julius Nyerere kimepungua kutokana na vifo, kustaafu au kutopewa majukumu ya kimkakati.
Wapo wanoamini kwamba ingawa wataalam bado wapo, wakati mwingine nafasi ya ushauri wao imezidi kufunikwa na maamuzi ya kisiasa. Matokeo yake ni kupungua kwa mchango wa wataalam katika kupanga mikakati na kutoa tahadhari kabla ya madhara kutokea.
Uenda athari za hali hiyo zikawa zimeanza kuonekana: kupungua kwa mvuto wa uwekezaji, tetemeko la uhusiano na washirika wa kimataifa, na Tanzania kujikuta nje ya nafasi muhimu katika taasisi za kimataifa.
Ni muhimu kueleweka kuwa taswira ni mtaji; na taifa likiipoteza, hupoteza pia fursa zinazotokana na taswira hiyo. Awali Mtu aliokuwa akijitambulisha mbele ya uso wa Mataifa wengi walitokewa na picha ya ukarimu, hali ipoje sasa na itakuwaje mbeleni?
Imeshuhudiwa jumuiya muhimu ambazo zinasifika kuwa na uhusiano wa kihistoria na Tanzania zikionya na kupinga mambo mbalimbali yanayoendelea ikiwemo ukiukwaji wa haki za binadamu, ndani ya kipindi cha Mwezi mmoja Umoja wa Ulaya wamesikika, Umoja wa Mataifa pamoja na jumuiya nyingine, Marekani nao wamemulika.
Katika hali ya sasa, diplomasia ya Tanzania inaonekana kuhitaji tathmini ya kina ya kitaalamu ili kurejea kwenye mwelekeo rafiki uliozoeleka. Ni wakati wa taifa kuketi chini upya na kufikiria namna bora ya kuwatumia wanadiplomasia nguli waliopo, pamoja na uzoefu kutoka mataifa rafiki, ili kuimarisha misingi ya ushawishi wake kimataifa.
Hatua hii uenda inaweza kurejesha mwanga, kujenga hoja zenye nguvu, na kulinda taswira ya taifa ambayo katika miaka ya karibuni imeanza kupata doa. Kwa kufanya hivyo, Tanzania ikaweza tena kurejea katika nafasi yake ya kihistoria kama mshiriki makini na mwenye heshima katika diplomasia ya kikanda na kimataifa licha uenda ya kuwa jambo hilo sio rahisi.