Habari za Zanzibar
JF-Expert Member
- Dec 18, 2024
- 651
- 433
π¦ππ π₯ππ¦ππ¦: πππ£ππ’π ππ¦ππ π¬π π§ππ‘πππ‘ππ π¬ππ‘πβππ₯π πππ ππ§ππππ πππ§πππ πππ π£ππ‘π π¬π πππ¬π π¬π π ππ π π‘π π π§π’π§π’
Ndani ya Jiji la New York, Marekani, imefanyika Sherehe Maalum ya Kampeni ya SHE RISES - Advocacy for a New Era: Women Leading Maternal and Child Health for All, iliyoandaliwa na Mhe. Balozi Togolani Mavura, Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, kwa heshima ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Sherehe hiyo inaakisi nafasi ya Tanzania katika diplomasia ya kimataifa, hususan katika kuimarisha afya ya mama na mtoto, pamoja na uongozi wa wanawake barani Afrika.
Nukuu: Umuhimu wa afya ya mama na mtoto kutoka kwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye ni Bingwa wa Umoja wa Afrika wa Afya ya Mama na Mtoto, anasema:
βJaribio lijalo la Afrika katika kulinda mamlaka yake halitaamuliwa tu katika vyumba vya mikutano, mabunge na mikutano ya kilele. Litaamuliwa katika wodi za wazazi, kliniki za vijijini, vituo vya afya vya jamii na huduma za utoaji wa chanjo kwa jamii.β
Kampeni ya SHE RISES inaweka mkazo katika nafasi ya wanawake kuongoza juhudi za kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za afya ya mama na mtoto kwa wote, huku ikiendelea kuitangaza Tanzania katika jukwaa la kimataifa kupitia diplomasia na uongozi wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.