MSEZA MKULU
JF-Expert Member
- Jul 22, 2011
- 3,882
- 5,896
Moja kwa moja.
Nilikuwa nafuatilia philosophia ya Trillionea Elon Musk ya " Parkinson Law ". Yeye anaamini Project ya miaka 10 inaweza kufanyika kwa miezi 6.
Aliwahi kuwarudisha maengineer wake walipomletea mradi utakaokamilika kwa miaka mingi akawaambia rudini mniletee plan mpya inayotekelezeka kwa miezi michache.
Anadai hata kama hautafanikiwa lakini kwa miezi 6 utakuwa umefanya jambo kubwa kuliko kama ungelitawanya kwa miaka 10. Level ya usiriasi inakuwa juu kuliko ukijua linatakiwa kufanyika mapema.
Nashauri wakina Professor Mkumbo warudi tena wamuandalie Mama plan ya miaka 5 ya kutekeleza hicho ambacho wao wanaona kinatekelezeka kwa miaka 24.
Sababu:
1: Dunia ya sasa inakaribu kila kitu cha kufanya jambo refu litimie kwa Muda mfupi. Ndio maana wachina waliwahi kujenga jengo lenye ghorofa 57 kwa masaa 28. Walitumia kanuni ya " Modular prefabricated construction " na wakaongeza masaa ya kazi kutoka 8 hadi 24. Huku wakiongeza idadi ya wafanyakazi.
2: Nchi yetu ni masikini sana, yaani iko nyuma ya wakati kuliko resource na uwezo tulio nao. Kurefusha mambo ni kujiongezea umasikini.
3: Lee Kuan Yew Mchina na Baba wa taifa wa Singapole aliwahi kusema ukiwa na lengo la kitaifa lifanye hadi mtoto mdogo wa nchi hiyo ajue kuna kitu kinaendelea nchini. Iwe katika lugha nyepesi sana hata mtoto wa chekechea anaweza kuelezea. Ukisema tulikuwa tumepanga kufikia miaka 50 ijayo tanzania iwe a b c ila kwa sasa tumebadili kwa kusacrifice hiyo hali tunataka tupate kwa miaka 5. Hiyo Italeta mshtuko mkubwa wa kiakili nchi nzima. Kila akili ya mtu itawaza yeye anashiriki vipi kwenye hiyo challenge. Kinachotokea hata hii Dira wengi bado hawajui kama ipo na inawahusu vipi na yeye anamchango gani.
Naomba kwasilisha.
Kilichonisukuma kuandika haya. Jana nilikuta watoto wanaangalia TBC ila umakini wao sio kinachoongelewa bali ni tanzania 2050. Wanaulizana wewe utakuwa na miaka mingapi? Kumbe hadi mimi wananikadilia kama nitakuwepo au sitakuwepo hahaha.😁