TANZIA Director Khalfani afariki Dunia

TANZIA Director Khalfani afariki Dunia

MUONGOZAJI na mtayarishaji wa video za muziki nchini, Khalfani Khalmandro

DAR ES SALAAM: MUONGOZAJI na mtayarishaji wa video za muziki ‘vichupa’ nchini, Khalfani Khalmandro amefariki dunia alfajiri ya leo katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) jijini Dar es Salaam.

Khalmandro amekutwa na umauti baada ya siku kadhaa kulazwa hospitalini kwa tatizo la damu kuvilia kwenye ubongo lililomsababishia kupata Kiharusi ama kupooza upande mmoja wa mwili wake.

Enzi za uhai wake, Khalfan alijipatia umaarufu kwa kuongoza video za wanamuziki kadhaa, wakiwamo Aslay, Navy Kenzo, Christian Bella, Baby Madaha, Chin Bees, Shilole, Linah na wengine wengi.

Miongoni mwa vichupa vilivyowahi kupita katika mikono ya muongozaji huyo ni pamoja na video ya Aah Wapi ya Country Boy, Bishoo ya Quick Rocka ft Young Dee, I just Wanna love you ya Navy Kenzo, YESA Marioo Ft Chino Wanaman na nyingine nyingi.
 
vijana pimeni pressure ya moyo kila wakati vijana sasa hivi ndio wanaongoza kwa kufa kwa high blood pressure mnajiona mko sawa kumbe mnatembea na bomu pimeni pimeni na mtumie dawa
 
vijana pimeni pressure ya moyo kila wakati vijana sasa hivi ndio wanaongoza kwa kufa kwa high blood pressure mnajiona mko sawa kumbe mnatembea na bomu pimeni pimeni na mtumie dawa
Kwa hiyo dam ilivilia tu ubongoni
Bila kuanguka au kujipigiga kichwa

Ova
 
Kuna kitu sijaelewa kwenye ishu hii ya director Khalfan..iyo stroke aliipata kwa kuumwa au kunatukio lilitokea likasababisha stroke...kuna clips nazion insta ni kama alikuwa anashot then kuna tukio likatokea (ilo tukio kama linafichwa iv) then akapata tatizo akakimbizwa hospital

Kuna kitu sijaelewa apa
 
RIP Khalfan nilipenda sana kazi zako za viwango vya kimataifa.

Stroke ama kiharusi hutokea ghafla tu nafikiri ni kama fault tu hujitokeza mwilini na huwa mbaya zaidi kama itapiga kichwani maana hupasua mishipa midogo na kusababisha damu kuvilia kichwani.

I lost my aunt on early 2021 sababu ya same case ya stroke iliochapa kichwani. Haikumaliza week tulienda kuzika. Inaumiza sana!
Poleni Sana
kitababu na hasa hapa Tz matibabu ya Kibingwa hufanyika pale MoI wanapasua kichwa shida kubwa eneo la tiba hapa Tz liko hoi sana sana.Watu Wengi wanaokufa hapa tz hawakustahili kufa kama serikali ingekua serious.
 
Back
Top Bottom