Tuliambiwa tutume maombi ya ajira za ualimu,mimi hapa nina ndugu yangu wote tulisoma ualimu,yeye alishaka tamaa muda tu,mimi nikatuma maombi nakumbuka nilitumia kama 50k katika mchakato wote wa utumaji wa maombi,kuapa na kuthibitisha vyeti kwa mwanasheria,yule ndugu hakutuma maombi yeye alikuja dar kutafuta fursa kutokea mbeya baada ya kukosa ajira...cha ajabu mimi niliyetuma maombi nikakosa ajira ,yeye jamaa alipata na kazi alipangiwa sumbawanga hadi leo hii yupo kazini,sasa hapa sijui kuna mechanism gani inayotumika hadi bado sielewi...kwa hiyo hata sasa lazima tukubali kuna kitu kimekosewa katika hii mifumo ya ajira,vijana wapo wengi mtaani na hawana ajira,hata sisi tulioamua kujiajiri bado mazingira ni mabovu kiasi ambacho hata serikali ikitoa tangazo la ajira,vijana wako radhi waache shughuli zao walizoamua kujiajiri na kutumia kiasi kidogo cha fedha walizotafuta kutuma maombi,halafu mwisho wa siku wanakosa mchongo..tutarajie maumivu mengine tena kwa vijana kupitia hizi ajira
Mfano halisi pia katika ajira za muda za NEC maombi yametumwa 3k lakini waliochaguliwa ni 500 tu katika jimbo fulani la uchaguzi hapa dar,na ile nyomi niliyoshuhudia taifa siku ile dah! Hatari sana,vijana tuna hali mbaya sana sio siri...