Dirisha la udahili NACTE limefunguliwa leo 15/6/2020

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Posts
44,629
Reaction score
83,056
Vijana changamka, omba vyuo.
Kila la heri!
===
Moderators samahani mliweka Tangazo la mwaka jana. Nimefanya editing na kuweka la mwaka huu posted on 15th June 2020

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI TAARIFA KWA UMMA KUHUSU WAOMBAJI WA NAFASI ZA MASOMO KWA NGAZI YA ASTASHAHADA NA STASHAHADA KWA MWAKA WA MASOMO 2020/2021 Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ni chombo kilichoanzishwa kwa Sheria ya Bunge Sura ya 129, ili kusimamia na kuratibu utoaji wa elimu ya ufundi na mafunzo katika Vyuo ambavyo si Vyuo Vikuu ama Vyuo Vikuu Vishiriki nchini. Jukumu mojawapo la Baraza ni kuhakikisha kuwa mafunzo yanayotolewa katika Vyuo vya Ufundi nchini yanakidhi vigezo na ubora unaohitajika katika soko la ajira ndani na nje ya nchi. Pia Baraza linao wajibu wa kuratibu udahili wa Wanafunzi kwenye Vyuo na kozi/programu zinazotambulika na mamlaka husika.

Baraza (NACTE), linapenda kuufahamisha umma kuwa udahili wa wanafunzi katika ngazi ya Astashahada na Stashahada kwa kozi/programu zote zinazotolewa na Vyuo vya Elimu ya Ufundi umefunguliwa rasmi kuanzia tarehe 15 Juni, 2020 hadi tarehe 15 Septemba, 2020.

Hivyo, Vyuo vinaruhusiwa kupokea maombi ya udahili kuanzia leo tarehe 15 Juni, 2020 hadi tarehe 15 Septemba, 2020. Vyuo hivyo vitachagua waombaji wenye sifa kati ya tarehe 16 hadi 21 Sepetemba, 2020 na kisha tarehe 22 hadi 29 Septemba, 2020 majina ya waombaji waliochaguliwa yatawasilishwa NACTE kwa ajili ya uhakiki. Majina ya waliochaguliwa na kuhakikiwa na NACTE yatatangazwa na Vyuo husika tarehe 8 Oktoba, 2020 kwa ajili ya kuanza masomo tarehe 16 Novemba, 2020.

Aidha, waombaji wa programu za Afya kwenye Vyuo vya Serikali watatuma maombi yao moja kwa moja kupitia tovuti ya Baraza (NACTE) kuanzia leo tarehe 15 Juni, 2020 hadi tarehe 15 Agosti, 2020. Majina ya watakaochaguliwa yatatangazwa tarehe 26 Agosti, 2020.

Vyuo vyote vya Elimu ya Ufundi vitakavyopokea maombi ya wanafunzi kwa ngazi ya Astashahada na Stashahada kuanzia leo tarehe 15 Juni, 2020 vinaelekezwa kuzingatia taratibu za udahili kama zilivyotolewa na Baraza kwa mwaka wa masomo 2020/2021.

Wahitimu wote wa Elimu ya Sekondari na Vyuo wenye sifa za kujiunga na kozi za Astashahada na Stashahada, wanashauriwa kufanya maombi yao kwa umakini ili kupata nafasi ya kujiunga na kozi/programu wanazozipenda na wanatimiza vigezo/sifa za kujiunga nazo kwa mwaka wa masomo 2020/2021.

Hivyo, Baraza linawashauri waombaji na wazazi kuhakikisha kuwa wanaomba kwenye Vyuo ambavyo vimeorodheshwa kwenye Kitabu cha Mwongozo wa Udahili kwa mwaka wa masomo 2020/2021 (Admission Guidebook for 2020/2021 Academic Year). Mwongozo wa Udahili unapatikana pia katika tovuti ya Baraza (www.nacte.go.tz).

IMETOLEWA NA: OFISI YA KATIBU MTENDAJI BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE) TAREHE: 15/06/202
 
Asante sanaaa...

Wakuu Mwenye uelewa jinsi ya Kufanya application kupitia NACTE online, tunaomba aweke mwongozo hapa kusaidia/kurahisishia wengine.
 
Vijana changamka, omba vyuo.
Kila la heri!
===
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDITAARIFA KWA UMMA KUHUSU MAOMBI YA UDAHILIWA MACHI2020 (MARCH INTAKE) KWA WAOMBAJI WA ASTASHAHADA NA STASHAHADA

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ni chombo kilichoanzishwa kwa Sheria ya Bunge Sura ya 129, ili kusimamia na kuratibu utoaji wa elimu na mafunzo ya ufundi katika Vyuo ambavyo si Vyuo Vikuu ama Vyuo Vikuu Vishiriki nchini. Jukumu mojawapo la Baraza ni kuhakikisha kuwa mafunzo yanayotolewa katika Vyuovya Ufundi nchini yanakidhi vigezo na ubora unaohitajika katika soko la ajira ndani na nje ya nchi.Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) linapenda kuufahamisha umma kuwa Udahiliwa wanafunzi katika ngazi ya Astashahada na Stashahada kwa kozi/programu zote isipokuwa Ualimu umefunguliwa rasmi kuanzia tarehe 15 Januari, 2020 hadi Tarehe 20 Februari, 2020kwa vyuo vyote vinavyotoamafunzo katika ngazi hizokwaUdahili wa mwezi machi.

Aidha Udahili huu hautahusisha waombaji wa programu za Afya kwenye vyuo vya Serikali. Hivyowaombaji wa programu hizo waombe kwenye vyuovyaafya visivyo kuwa vya SerikaliKwa waombaji wa programu za afya kwenye vyuo visivyo vya Serikali na waombaji wa progrmu nyingine zotewatatakiwa kuomba moja kwa moja kwenye vyuo husika. Aidhavyuo vitapokea maombi na kufanya chaguzi kwa wanafunzi wenye sifa na kisha kuwasilisha NACTE majina ya waliochaguliwa kwa ajili ya uhakiki kabla ya kuyatangaza. Vilevile vyuo vinaelekezwa kuzingatia taratibu za udahili kama zilivyotolewa na Baraza katika mwaka wa masomo 2019/2020.

Baraza pia linataarifu umma na vyuo kwamba udahili katika programu ya Huduma ya Afya Ngazi ya Jamii (Community Health)umesitishwa hadi hapo itakapotangazwa tena.Wahitimuwote wa Elimu ya Sekondari na vyuo wenye sifa za kujiunga na kozi za Astashahada na Stashahada, wanashauriwa kufanya maombi kwa umakini ili kuweza kupata nafasi ya kujiunga programu wanazozipenda na ambazo wanatimiza vigezo/sifa za kujiunga nazokwa mwaka 2019/2020.

Baraza linawashauri waombaji na wazazi kuhakikisha kuwa wanaomba kwenye vyuo vinavyokidhi ubora ambavyo vimeorodheshwa kwenye Kitabu cha Mwongozo wa Udahili kwa mwaka wa masomo 2019/2020(Admission Guidebook for 2019/2020 Academic Year). Mwongozo wa Udahili unapatikana katika tovuti ya NACTE (www.nacte.go.tz).

IMETOLEWA NA:OFISI YA KATIBU MTENDAJIBARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)TAREHE: 15/01/2020
Mkuu hebu cheki tena: Tangazo hili ni la March (2019/2020) intake na lilitoka January 15, 2020). Tangazo sahihi ni la September intake(2020/2021) ambalo limetoka leo (15/06/2020) NACTE website..
March intake 2019/2020 ilikamilika na ndiyo iliyo vurugwa na COVID 19 na waliochaguliwa ndio walioreport Juni 1, 2020.
 
Vipi kuhusu vyuo vingine application zinafunguliwa lini ???
 
Mkuu hebu cheki tena: Tangazo hili ni la March (2019/2020) intake na lilitoka January 15, 2020). Tangazo sahihi ni la September intake(2020/2021) ambalo limetoka leo (15/06/2020) NACTE website..
March intake 2019/2020 ilikamilika na ndiyo iliyo vurugwa na COVID 19 na waliochaguliwa ndio walioreport Juni 1, 2020.
Kwahiyo unamaanisha sio kwl au
 
Waliweka mods, not me na sijalisoma!
 
Mkuu hebu cheki tena: Tangazo hili ni la March (2019/2020) intake na lilitoka January 15, 2020). Tangazo sahihi ni la September intake(2020/2021) ambalo limetoka leo (15/06/2020) NACTE website..
March intake 2019/2020 ilikamilika na ndiyo iliyo vurugwa na COVID 19 na waliochaguliwa ndio walioreport Juni 1, 2020.
nimerekebisha, naomba mrejesho
 
MAOMBI YA VYUO NGAZI YA CHETI NA DIPLOMA 2020/2021.

Dirisha la maombi ya vyuo ngazi ya cheti na diploma yamefunguliwa rasmi kuanzia tarehe 15 June 2020 hadi tarehe 15 September.

Kwa wewe mwenye uhitaji wa kukamilishiwa application popote ulipo Tanzania, huduma inapatikana na ya uhakika.

Tuna wataalamu na wazoefu watakaokusaidia kukamilisha application yako ndani ya muda mfupi popote ulipo.

Kwa mawasiliano zaidi tuwasiliane whatsapp/sms/simu +255 752026992

Tunapatikana Mbagala, Maeneo ya Sabasaba.
20200616_144952_0000.jpg
 
Let me do it!
mkuu naomba unieleweshe haya. 1:Eti pale kwenye guidebook ile sehemu iliyo andikwa 'admission capacity' wanamaanisha nini? 2😛ia admission requirements za ordinary diploma in clinical medicine na certficate yake,diploma in nursing and midwifery na certificate ya nursing zote ni 4 passes including biology,chemistry,and physics/engneering science, eti "PASSES" ni ipi kati ya A,B,C na D?
 
Admission capacity ni idadi ya wanafunzi wanaopokelewa kwenye kozi hiyo tu hapo chuoni

Passes ni kama ulvivyoandika ie ABCD... you have passed. E= Fail (umefeli somo hilo).
NOTE: Vyuo vingine vinataka pass za juu mfano ABC tu! D hawaitaki!

Angalia chati hizo
1592324522613.png
 
New Intake October .20/21

Kwa wale wanaotak kuomba vyuo katika dirisha hili lilofunguliwa kuanzia tarehe 15/6/2020 mnaweza kufollow iyo link apo mtapata msaada wa kuwaeleza jinsi ya kuomba vyuo na maswali yoyote yanayohusu vyuo utajibiwa.
WELCOME
 
Kama ana C mbili na Zilizobaki D , anaweza pata ?
Na wale walio resist ?

Tupeane mawazo
 
Back
Top Bottom