Vijana changamka, omba vyuo.
Kila la heri!
===
Moderators samahani mliweka Tangazo la mwaka jana. Nimefanya editing na kuweka la mwaka huu posted on 15th June 2020
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI TAARIFA KWA UMMA KUHUSU WAOMBAJI WA NAFASI ZA MASOMO KWA NGAZI YA ASTASHAHADA NA STASHAHADA KWA MWAKA WA MASOMO 2020/2021 Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ni chombo kilichoanzishwa kwa Sheria ya Bunge Sura ya 129, ili kusimamia na kuratibu utoaji wa elimu ya ufundi na mafunzo katika Vyuo ambavyo si Vyuo Vikuu ama Vyuo Vikuu Vishiriki nchini. Jukumu mojawapo la Baraza ni kuhakikisha kuwa mafunzo yanayotolewa katika Vyuo vya Ufundi nchini yanakidhi vigezo na ubora unaohitajika katika soko la ajira ndani na nje ya nchi. Pia Baraza linao wajibu wa kuratibu udahili wa Wanafunzi kwenye Vyuo na kozi/programu zinazotambulika na mamlaka husika.
Baraza (NACTE), linapenda kuufahamisha umma kuwa udahili wa wanafunzi katika ngazi ya Astashahada na Stashahada kwa kozi/programu zote zinazotolewa na Vyuo vya Elimu ya Ufundi umefunguliwa rasmi kuanzia tarehe 15 Juni, 2020 hadi tarehe 15 Septemba, 2020.
Hivyo, Vyuo vinaruhusiwa kupokea maombi ya udahili kuanzia leo tarehe 15 Juni, 2020 hadi tarehe 15 Septemba, 2020. Vyuo hivyo vitachagua waombaji wenye sifa kati ya tarehe 16 hadi 21 Sepetemba, 2020 na kisha tarehe 22 hadi 29 Septemba, 2020 majina ya waombaji waliochaguliwa yatawasilishwa NACTE kwa ajili ya uhakiki. Majina ya waliochaguliwa na kuhakikiwa na NACTE yatatangazwa na Vyuo husika tarehe 8 Oktoba, 2020 kwa ajili ya kuanza masomo tarehe 16 Novemba, 2020.
Aidha, waombaji wa programu za Afya kwenye Vyuo vya Serikali watatuma maombi yao moja kwa moja kupitia tovuti ya Baraza (NACTE) kuanzia leo tarehe 15 Juni, 2020 hadi tarehe 15 Agosti, 2020. Majina ya watakaochaguliwa yatatangazwa tarehe 26 Agosti, 2020.
Vyuo vyote vya Elimu ya Ufundi vitakavyopokea maombi ya wanafunzi kwa ngazi ya Astashahada na Stashahada kuanzia leo tarehe 15 Juni, 2020 vinaelekezwa kuzingatia taratibu za udahili kama zilivyotolewa na Baraza kwa mwaka wa masomo 2020/2021.
Wahitimu wote wa Elimu ya Sekondari na Vyuo wenye sifa za kujiunga na kozi za Astashahada na Stashahada, wanashauriwa kufanya maombi yao kwa umakini ili kupata nafasi ya kujiunga na kozi/programu wanazozipenda na wanatimiza vigezo/sifa za kujiunga nazo kwa mwaka wa masomo 2020/2021.
Hivyo, Baraza linawashauri waombaji na wazazi kuhakikisha kuwa wanaomba kwenye Vyuo ambavyo vimeorodheshwa kwenye Kitabu cha Mwongozo wa Udahili kwa mwaka wa masomo 2020/2021 (Admission Guidebook for 2020/2021 Academic Year). Mwongozo wa Udahili unapatikana pia katika tovuti ya Baraza (www.nacte.go.tz).
IMETOLEWA NA: OFISI YA KATIBU MTENDAJI BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE) TAREHE: 15/06/202