Tuelezee haya ya obsessed
Naibu Waziri wa mambo ya nje Dr Kolimba amewashauri watanzania kutokurupuka na kukimbilia fursa Kenya kufuatia utaratibu mpya uliotangazwa na serikali ya Kenya. Amefafanua kuwa fursa za uwekezaji, umiliki ardhi na ajira alizotoa Rais Kenyatta ni nzuri lakini si vema kwa wananchi wetu kuanza kuzichangamkia bila kupata utaratibu kutoka nchi zote mbili, na ametolea mfano sheria za sasa za Kenya haziruhusu mgeni kumiliki ardhi. Dr Kolimba alikuwa akihojiwa na watangazaji wa Clouds 360 Masoud Kipanya na Sizya waliotaka kujua serikali inasemaje kuhusu fursa zilizotolewa na Rais Kenyatta kwa wananchi wa jumuiya ya Afrika Mashariki. Source kipindi cha clouds 360, Clouds Tv!