Diva: Kama huna milioni 500 huwezi kunioa

Diva: Kama huna milioni 500 huwezi kunioa

Mil 500 ya kuchora au ya kuchonga [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Hii ndio tabu ya wadada ambao wamejikuta tu wapo, hawana hata wazazi, enzi zetu mahari anapanga mzazi... Cku hzi mdada ametokezea mjini hana wazazi, so anajipangia mahari mwenyewe... Na anapokea mwenyewe...

Sawa!!
 
View attachment 716779 Mtangazaji wa Clouds Fm Loveness Malinzi maarufu kama Diva the bawse amefunguka kuwa hawezi akaolewa na mwanaume yoyote bila kutokew mahari ya shilingi milioni 500.

Hii sio mara ya kwanza kwa Diva kuweka kigezo cha kuolewa na mwanaume mwenye pesa mbele kwani mara nyingi amekuwa akisema kuwa hawezi akaolewa kwa mahari ndogo.

Siku ya jana kupitia ukurasa wake wa Instagram Diva amekumbushia Tena vigezo vikubwa kwa mwanaume ambaye atakubali amuoe ambavyo ni awe tajiri kiasi ya kwamba aweze kutoa mahari ya milioni 500 lakini pia awe anajua kuongea kingereza:

"Kunioa ni milioni 500….set that jokes aside am deadly serious….make sure uwe unaongea English yenyewe hasa… uwe smart uwe handsome…..uwe loaded…No broke niggas in 2018 tupendane kwa faida, you can say wheteves just heard worse, seen worse SMHFG Nothing mean to me…..harsh ain’t new to me I heard it all…..Mwenye povu hana hela ruksa na povu lako nina Omo na jiki plus toothbrush na Colgate jus there for you dummy”.

Diva ametangaza ruksa mwenye hizo sifa ajitokeze hii imekuja baada ya kuachana na mpenzi wake msanii wa Bongo fleva Heri Muziki baada ya kutoswa hewani.


Mpekuzi
Hivi anajua milioni mia tano unamilik mabasi mangapi ya kusafirsha watu mikoani? Tena hata akiwa ni nusu yake hawez pata!! Ameamua kutajirsha wazaz wake kwa mahari?
 
2018 Kasema mahari M500

2022 atasema mahari M300

2025 atasema mahari M 100

2028 atasema mahari M10

2030 Ata andika uzi humu "natafuta mume " bila kuweka vigezo
Mmmh ww mbona unamwekea miaka ming sana? 2022 itakua bure tena akiwa kwa mzee wa upako akitaka kuombewa apate mume
 
Back
Top Bottom