Diva na Niffer waandika ujumbe wa kuomba radhi baada ya kukamatwa kwa kuchangisha michango maafa ya Kariakoo

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Mtangazaji wa Wasafi Fm, Diva Malinzi na Mfanyabiashara Jenifer Jovin maarufu Niffer wameandika barua za kuomba radhi (Kusamehewa) baada ya kupatikana na tuhuma za kuchangisha michango kwa ajili ya Wahanga wa janga la Kariakoo bila kufuata utaratibu.
Pia, Soma:

Polisi: Tunawashikilia Niffer na Diva kwa mahojiano na hatua nyingine za Kisheria
Polisi wamsafirisha Niffer hadi Dar kutokea Dodoma baada ya kujisalimisha kufuatia agizo la Waziri Mkuu la kukamatwa
Jeshi la Polisi tayari limempata Niffer kwa kuchangisha michango ya wahanga wa Kariakoo

Baada ya kutenda makosa hayo Diva Malinzi (36) na Jenifer Jovin (25) walikamatwa na jeshi la Polisi kwa ajili ya mahojiano na wameendelea kubaki mahabusu wakisubiria kupatiwa dhamana.
Hivyo kutokana na kutambua makosa yao wote wawili kwa pamoja, wameandika jumbe za kuomba radhi na kuomba kusamehewa kwasababu walifanya hayo kwa kutokufahamu utaratibu, huku wakiahidi kutorudia tena na Kuwa Mabalozi wazuri kwenye Jamii.
 
Basi sawa, hii ipitishwe na iwe sheria rasmi kwamba mtu mwingine yeyote akitenda kosa pasipo kujua ama kwa bahati mbaya, anaweza akaandika barua ya kuomba radhi ili asanehewe.
Sio kwamba nina wachukia wala sipendi wasamehewe.... Lahhhh ninatamani kuona haki na usawa ikitendeka kwa WaTanzania wote, na sio kwa ukubwa wa majina ama umaarufu
 
upeleke mwaada bungeni ukipita itakuwa sheria
 
Huyo niffer aendelee kushikiliwa hata barua ameandika kwa dharau pia na haijanyooka waziri mkuu shikilia hapohapo adabu imwingie alijua anaweza kutupeleka peleka kama anavyompelekesha mama yake..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…