Diva na Niffer waandika ujumbe wa kuomba radhi baada ya kukamatwa kwa kuchangisha michango maafa ya Kariakoo

Diva na Niffer waandika ujumbe wa kuomba radhi baada ya kukamatwa kwa kuchangisha michango maafa ya Kariakoo

Jamal malinzi?
kuna askari alimsweka lupango mtoto wa chawene babake akasema apelekwe mahakamani ni mtu mzima alivyomfikisha sikuhiyohiyo hukumu ikasomwa akaachiwa, baada ya muda chawene akawa waziri wa mambo ya ndani askari alitamani kuomba uhamisho wa kwenda mbambabay

mwingine alimfyatulia risasi malima wakati kesi inaendelea akateuliwa kuwa RC kesi ikafa. ukiwa mjini njoo taratibu.
 
Mtangazaji wa Wasafi Fm, Diva Malinzi na Mfanyabiashara Jenifer Jovin maarufu Niffer wameandika barua za kuomba radhi (Kusamehewa) baada ya kupatikana na tuhuma za kuchangisha michango kwa ajili ya Wahanga wa janga la Kariakoo bila kufuata utaratibu.
Pia, Soma:

Polisi: Tunawashikilia Niffer na Diva kwa mahojiano na hatua nyingine za Kisheria
Polisi wamsafirisha Niffer hadi Dar kutokea Dodoma baada ya kujisalimisha kufuatia agizo la Waziri Mkuu la kukamatwa
Jeshi la Polisi tayari limempata Niffer kwa kuchangisha michango ya wahanga wa Kariakoo

Baada ya kutenda makosa hayo Diva Malinzi (36) na Jenifer Jovin (25) walikamatwa na jeshi la Polisi kwa ajili ya mahojiano na wameendelea kubaki mahabusu wakisubiria kupatiwa dhamana.
Hivyo kutokana na kutambua makosa yao wote wawili kwa pamoja, wameandika jumbe za kuomba radhi na kuomba kusamehewa kwasababu walifanya hayo kwa kutokufahamu utaratibu, huku wakiahidi kutorudia tena na Kuwa Mabalozi wazuri kwenye Jamii.
Mambo kama haya polisi wetu wa Burundi ndiyo wanayaweza sasa! Kuandiksha watu maelezo hata kwenye mambo ya kipuuzi.
 
Kwanza kabisa Mimi Kama mtanzania mmojawapo ninayeombwa msamaha .
Nahitaji kujua kwanini wametumia herufi kubwa ,ni Kama wananilazimisha nikubali kuwasamehe .
Hivyo nataka waandike kwa herufi ndogo aidha nataka pia Diva aniambie ukweli ameishia darasa la ngapi maana amekuwa ananidanganya Sana ila kupitia mwandiko wake ,napata mashaka na elimu yake .

Sanjari na hayo ,natamani wakitimiza masharti yangu tajwa ,waachiwe huru ila Jeniffer anitafute Kuna mambo nimshauri .

Wako ,raia mwema muombwa msamha.
 
Mtangazaji wa Wasafi Fm, Diva Malinzi na Mfanyabiashara Jenifer Jovin maarufu Niffer wameandika barua za kuomba radhi (Kusamehewa) baada ya kupatikana na tuhuma za kuchangisha michango kwa ajili ya Wahanga wa janga la Kariakoo bila kufuata utaratibu.
Pia, Soma:

Polisi: Tunawashikilia Niffer na Diva kwa mahojiano na hatua nyingine za Kisheria
Polisi wamsafirisha Niffer hadi Dar kutokea Dodoma baada ya kujisalimisha kufuatia agizo la Waziri Mkuu la kukamatwa
Jeshi la Polisi tayari limempata Niffer kwa kuchangisha michango ya wahanga wa Kariakoo

Baada ya kutenda makosa hayo Diva Malinzi (36) na Jenifer Jovin (25) walikamatwa na jeshi la Polisi kwa ajili ya mahojiano na wameendelea kubaki mahabusu wakisubiria kupatiwa dhamana.
Hivyo kutokana na kutambua makosa yao wote wawili kwa pamoja, wameandika jumbe za kuomba radhi na kuomba kusamehewa kwasababu walifanya hayo kwa kutokufahamu utaratibu, huku wakiahidi kutorudia tena na Kuwa Mabalozi wazuri kwenye Jamii.
Fred Vunjabei ana Taarifa kuwa Demu wake Diva yuko Nyavuni sasa?
 
Hizi mbilinge zenu za kujuana na kutukuza majina ya “washkaji zenu wa enzi ndio yametuzalia Boys 2Men, tuko kwenye blues mpaka leo!
we sema kuna wazee wakisikia njaa wanaenda kunywa chai ikulu,

namkumbuka maj general marwa aliwahi kwenda ikulu wakati wa mwinyi kufika akamwambia amekuja kuomba kazi ya kufyeka nyasi ikulu amechoka kukaa bila kazi, mwinyi akamteua kuwa balozi nigeria.

nyerere aliwahi kwenda zambia rais akastukia yuko ofisini kwake akamwambia nimekuja kumchukua rafiki yangu kaunda, kwa kitete akaagiza apelekwe gerezani kumwona kaunda akamkuta amedhoofu sana kwani aligoma kula. akamwamuru ale na apewe maji ya kunywa alivyoshiba akamwambia twende, wakaondoka nae hadi ikulu kufika akamwambia rais naondoka nae, ndio kaunda aka opt kwenda kwa mwanae canada. mjini kuna wazee wana nguvu. usiombe. ukiona tumbili mjini anamwenyewe.
 
Wapelekwe mahakamani hilo ni kosa la uhujumu uchumi..
Kama kuandika barua manguruwe na kina JATU nao wapewe ruhusa ya kuandika barua nakuachiwa.
wapelekeni, utawapeleka saa nne saa nne na nusu wameachiwa na unaamuliwa uwalipe fidia
 
Back
Top Bottom