Jannatul Firdaus
JF-Expert Member
- Aug 4, 2026
- 446
- 1,113
Mtangazaji mashuhuri wa habari na burudani, Diva the Boss , amejitokeza na kuishutumu waziwazi kampuni ya Wasafi Media kupitia ujumbe mzito alioochapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram mnamo Septemba 15, 2026 .
Diva amechukua hatua hiyo ya kuweka wazi hisia zake ili kupaza sauti na kuiomba serikali, ikiwa ni pamoja na kumtaja Mheshimiwa Mwigulu Nchemba na Ikulu Mawasiliano, imsaidie kupata haki yake baada ya kuvumilia ahadi hewa na kuzungushwa kwa muda mrefu bila kulipwa jasho lake.
Mtangazaji huyo ameeleza kuwa amefanya kazi hiyo kwa kujituma hadi usiku wa manane lakini amesalia bila kupata hata senti tano kwa miezi minne sasa, jambo lililomfanya alie kwa uchungu na kuamua kuwashirikisha Watanzania mitandaoni ili kumsaidia kushinikiza malipo hayo .