@ENZO
Don't take it too personal ndugu yangu! Diamond na wengine wote kama yeye muziki ndo kazi yao! Haiwezekani, narudia haiwezekani mtu apate mchongo wa millions of t shillings halafu auache kwa sababu za kisiasa! Na kama anapewa mchongo kama huo na kisha anauacha ndo angekuwa mpumbavu zaidi! Haya mambo tusiongelee kiushabiki na badala yake tuwe realistic! Hata wewe usingeweza kuacha mchongo kama huo coz' hata hao viongozi wenu linapokuja suala la kazi na biashara, siasa wanaweka pembeni! Na ndio maana hata viongozi wenu linapokuja suala la posho bungeni, wote wanaongea lugha moja na CCM.... haya mambo tuweke ushabiki pembeni, hayawezekani!
Reginald Mengi, Bakheresa, Channel Ten na wengine kama wao; hao pia ni wafanyabiashara... tofauti yao ni kwamba wao biashara yao ni media na Diamond biashara yake ni muziki! Sasa mbona hatuoni mkiwalaani akina Bakheresa ambao wanatumia media zao kuitangaza CCM? Mbona hatuwasikii kuwalaani wafanyabiashara wengine ambao tena ndo ambao hasa wanawawezesha CCM kwa ari na mali na badala yake mnahangaika ma hustlers wenzenu? Kuna mahali nimekuuliza hivi kwa wanasiasa gani Tanzania hii wa kuwafanya muwe mnatoka povu na kutukana watu kiasi hicho? Yaani hawa hawa ambao hata wao linapokuja suala la maslahi yao hawataki kuongea lugha moja na nyinyi? Mbona hamkumlaani Ndesamburo pale alipomkodishia chopper kada wa CCM wakati wa kampeni? Hivi kweli unaamini kabisa leo hii CCM watake kukodi ukumbi wa Billicanas MBowe atakataa?
Nimalizie tu kusema kwamba, watu wengi wanaochukia wengine wanapenda kuchanganya mambo! Akimpenda msanii basi atataka hata demu au bwana wa msanii awe ni yule anayempenda yeye (shabiki), chama cha siasa kiwe ni kile anachokipenda yeye, n.k.... haya mambo hayaendi hivyo!!
Acha kuchanganya siasa na kazi coz' hata hao viongozi wako linapokuja suala la kazi/biashara; siasa wanaweka pembeni! Narudia, ni mwanamuziki mpumbavu tu ambae angeweza kukataa mchongo wa kampeni wakati muziki ndo kazi yake! Kwanza hata huyo Diamond wakati anahojiwa alishasema wazi kwamba yeye muziki ni kazi kwahiyo haangalii nani amempa tenda bali anachoangalia yeye nani amekata kisu kikali!!!! Na kwa staili yenu hii ya kujifanya kama nyinyi ndo wenye uchungu sana na nchi hii, nyinyi ndo mnaojua sana suala la mabadiliko kwenye nchi hii... trust me, mtakuwa mnatukana hata ndugu zenu wa damu! Ukimya wa Dr. Slaa kwenye kipindi kigumu kama hiki na kujichomoa kwa Lipumba kulitosha sana kuwapa somo kwamba kumbe hata hawa viongozi wetu wamekalia sana maslahi... sasa ikiwa hata waendesha usukani tu, maslahi kwanza na mambo mengine baadae halafu uje kuwashangaa wasanii??!!!