Mara baadae ya kuchaguliwa kuna form maalum unatakiwa kuijaza online inaitwa DS-260,mara baadae ya hapo utatumiwa barua itakayokuonyesha tarehe ya interview. Kabla ya interview utatakiwa kwenda kufanya vipimo hospitali pamoja na kupata Police clearance certificate, baada ya hapo ndio utaenda ubalozi kufanya interview.
GHARAMA UTAKAZO TUMIA.
1.Medical gharama yake ni kama milioni 1.
2.Interview ni dollar 330
3.Police clearance certificate ni sh.2500.
Note: Mara baada ya kufaulu interview ubalozini kuna form utapewa unatakiwa kulipia kiasi cha dollar 220 hii ni kwaajili ya kuprocess green card yako.
Kuhusu nauli na gharama nyinginezo utatakiwa kujilipia mwenyewe, serikali ya Marekani haikulipii chochote.
Hii fursa inayotolewa na Serikali ya Marekani kusaidia watu wenye ndoto za kuishi, kufanya kazi, kufanya biashara na kusoma Marekani pasipo kutumia mlolongo mrefu. Kama kuna mahali hujanielewa unaweza kuniuliza.