Kijakazi
JF-Expert Member
- Jun 26, 2007
- 7,093
- 10,469
Divide et impera (divide and Rule) Ni neno la Kirumi lililobuniwa na Mwanafalsafa Niccolo Machiavelli aliyeishi kwenye karne ya 16 huko Barani Ulaya!
Alichomaanisha ni kwamba wewe kama Mtawala ili uweze kufanikiwa kuwatala Watu ni lazima uwagawanye Watu ambao siku zote walikuwa pamoja kwenye makundi mengi madogo madogo...
Kama vile Himaya ya warumi ilivyokuwa inafanya kwenye makoloni yake yaani wale waliokuwa wanatawaliwa waliwekwa kwenye makundi madogo madogo na ushirikiano baina ya haya makundi ilikuwa ni marufuku, bali haya makundi yalikuwa tu kila moja kwa wakati wake wanaripoti moja kwa moja kwa watawala warumi na hivyo ikawa rahisi kuwatawala!
Na hiki ndicho kilichotokea nchini Kenya, Wazungu walijua ya kwamba ili waweze kuwatawala Waafrika (Wakenya) ni lazima wawagawanye kwenye makundi madogo madogo ambayo hapo mwanzo hayakuwepo ambayo leo hii tunayaita Makabila!
Wazungu walianzisha haya waliyoyaita Makabila wakasema ninyi mnaoishi hapa mtaitwa Wakikuyu, na ninyi Mtaitwa Wajaluo ninyi mnaoishi pale mtaitwa Waluya na nyote ninyi mnaripoti moja kwa moja kwangu na ni MARUFUKU kutengeneza UMOJA baina yenu mkiwa na tatizo mnakuja moja kwa moja kwangu na SIYO kulitatua ninyi wenyewe na ndio maana mpaka leo hii utasikia Kiongozi fulani wa Kenya kakimbilia Uingereza kushitaki kwamba Wakikuyu ama Waluo inategemea anatoka kundi gani wanataka kumuua na hawezi kwenda popote pale kushitaki isipokuwa Uingereza hawezi kwenda Tanzania, Afrika Kusini ama Uchina au hata India na Ujerumani au Uhispania bali atakwenda Uingereza kushitaki!
Kumbuka ya kwamba kabla ya kuja kwa Waingereza nchini Kenya kulikuwa hakuna kitu kama Mkikuyu ama Mluya na ndio maana hata hao wanaojiita Waluya kwa mfano hawaelewani wote ni mzumgu tu aliwaambia ninyi kuanzia hapa mpaka pale mnaitwa Waluya na ninyi kuanzia pale mpaka hapa ni Wajaluo na wa kule ni Wakalenjili na hamna Uhusiano na mkiwa na shida mnakuja kwangu!
Hivyo Amani ya kweli nchini Kenya itapatikana tu kama mkiacha kwenda kwa Mtawala kuripoti matatizo yenu bali mkianza kuongea wenyewe kwa wenyewe na kufuta neno Kabila katika Kamusi zenu na kuweka kwenye Katiba kabisa kwamba Kenya hakuna Kabila bali kuna Taifa la Wakenya!