PreGE2025 Division zero inatosha kabisa kuelewa ujumbe wa Askofu Gwajima kuhusu utekaji

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Naungana mkono hoja yako, ni kweli kabisa msingi mama wa matatizo haya ya utekaji ni katiba mbovu inayotoa mwanya kwa kumpa madaraka makubwa mtu mmoja tu, but kwa katiba hii hii, angalau mambo haya ya wasiojulikana na uteswaji na upotezwaji wa watu yamejitokeza sana kipindi cha magu, hii inampa picha aliyepo kusema , kama mtangulizi wangu kafanya kwa nini mimi nisifanye?
 
Desert mission=mission ya Tanganyika nchi kavu!!

Hiki kikundi ndio kitafanya waliomtuma kutokua na imani na mwenyekiti na kusema wazi hatuna Imani na mwenyekiti,coz anatesa watu kupitia kikundi Cha mauaji!!

Patachafuka na ataambiwa achia mama achia!!

Nawaza nafikiria!!
 

Mwl. Nyerere aliwahi kusema kwamba " kwa Katiba hii ningeweza kuwa hata dikteta kama ningependa."
 
Kuna kitu waliotangulia kutoa comment wanakijua lkn hawakisemi. Yaani wamepapasa kisimi lakini G spot bado hawajaigusa.
 
Hayo mambo waliposema chadema waliambiwa kama wanataarifa wazipeleke Polisi na Jeshi litashughulikia.

Sasa Gwaji Boy kasema, Polusi wakachukue Taarifa kutoka kwa Gwaji Boy wazifanyie kazi?
 
sasa kama kikundi hiki ni kidogo na kinachafua nchi na idara za usalama zote zinashindwaje kuwadhibiti kwa kuipa afya nchi.huu ndio ujinga ninaoulalamikia hapa.watu wana silaha,wana mamlaka ,wanashindwa nini kudhibiti kikundI hiko.
hao ote lao moja.kulinda ccm na matumbo yao.
 
Hayo mambo waliposema chadema waliambiwa kama wanataarifa wazipeleke Polisi na Jeshi litashughulikia.

Sasa Gwaji Boy kasema, Polusi wakachukue Taarifa kutoka kwa Gwaji Boy wazifanyie kazi?
Kwa hiyo kwa akili zako timamu, unaamini kuwa jeshi letu ni vilaza na hawana intelejensia ya kutambua kuwa haya matukio ya utekaji chanzo chake ni nini? Basi kama ndivyo watendaji katika hili jeshi wafukuzwe wote, maana hawajui wajibu wao kwa raia
 
Saa100 form 4, alipata division Gani?
 
Na kila mwenye akili timamu, amejiuliza haya maswali, na jibu ni moja tu, kuna kitu nyuma ya pazia
 
Wewe peke yako ndiye humuamini alichokisema.

Hatutaki utupoteze, sisi tumeamini alichokisema 100%
 
Kwa hiyo kwa akili zako timamu, unaamini kuwa jeshi letu ni vilaza na hawana intelejensia ya kutambua kuwa haya matukio ya utekaji chanzo chake ni nini? Basi kama ndivyo watendaji katika hili jeshi wafukuzwe wote, maana hawajui wajibu wao kwa raia
Kutokujua sio ukilaza, wanajitoa ufahamu/wanafunika kombe tu kupisha mwana haramu apite.

SSH aliunda tume kuchunguza mauwaji ya ALI KIBAO akaahidi tungepewa taarifa, umewahi kupewa taarifa ya uchunguzi ule au alikuwa ana funika kombe?

Polisi mchana kweupe waliwabeba wafuasi wa Chadema na video zipo wakawavunja miguu, polisi wakakanusha unadhani walikuwa vilaza?

Uchawa utawaua acheni kujidharirisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…