Diwani Athumani Msuya atenguliwa Ikulu

Diwani Athumani Msuya atenguliwa Ikulu

Kukataa ni uhaini na adhabu ni inaweza kuwa kifo au kuishi kama marehemu jumbe... (RIP)

Hivyo msiwe mna andika ili mradi kuandika... una zani kwann wakina mbowe hawakatai wakiitwa kwenda kwa Mh. Ikulu? Ni uhaini kukataa wewe kama mtanzania kwa nchi yako
Hata jirani akiniita naenda, nikatae kwani nina ugomvi naye??
 
Huko ubalozini unazani ana ripoti mbinguni??

Sio kila anae ondolewa ktk teuzi amemgomea Mh.

Kumgomea ni kosa la uhaini... Uhaini sio kupindua nchi pekee...

Fahamu tafsiri sahihi ya kosa la uhaini na adhabu yake​


Fahamu tafsiri sahihi ya kosa la uhaini na adhabu yake
Uhaini ni kosa la jinai, kwa tafsiri nyepesi ina maana kwamba ni kosa kubwa ambalo mtu analifanya dhidi ya nchi yake na mtu anyefanya kosa hili anajulikana kama msaliti, mfano wa watu wasaliti wanaojulikana duniani ni Yuda ambaye kidini alimsaliti Yesu, mwingine ni Benedict Anold huyu jamaa aliisaliti nchi yake ya Marekani dhidi ya Mbritishi, wengine ni Vidkun Quisling, na Marshall Pe’tain.
Kisheria ukubwa wa kosa hupimwa kwa adhabu yake, kosa likiwa kubwa mtuhumiwa hutumikia adhabu kubwa vivyo hivyo kosa likiwa dogo mtuhumiwa huadhibiwa kiasi.


Kwa mujibu wa sheria ya Tanzania, mtu akifanya yafuatayo huhesabiwa kama amefanya kosa la jinai la uhaini hivyo huadhibiwa kulingana na ukubwa wa kosa hilo.

Kifungu cha 39 ( 1 ) cha kanuni za adhabu kinasema kuwa mtu yeyote ambaye yumo ndani ya Jamhuri ya Muungano au popote, kujaribu kumuua Rais, kuanzisha vita dhidi ya Jamhuri ya Muungano, kusababisha, kuwezesha, kuchochea, kushawishi, kushauri kuhusu kifo, kumlemaza, kumzuia, kufungwa kwa Rais. kumwondolea Rais heshima na jina la mkuu wa nchi, amiri jeshi mkuu, au kiongozi wa serikali, kupindua serikiali iliyo madarakani, kutishia serikali, bunge au mahakama kwa makosa haya na yale yaliyotajwa hapo juu mtu wa namna hiyo atakuwa ametenda kosa la jinai ambalo ni kosa la uhaini

Aidha ifahamike kuwa kwa mtu yeyote atakayekutwa na hatia ya kutenda kosa la uhaini adhabu yake ni kifo na sheria hiyo ya kifo imeelezwa katika kifungu cha sheria namba 39 na 40 cha kanuni za adhabu.
Hivyo watanzania kwa umoja wetu tunapaswa kuzijua sheria za nchi yetu ili kuweza kujiepusha kutenda makosa ya jinai dhidi ya nchi yetu.



Iwe kwa faida yako na wengine kama wewe ambao una hisi kila mtu akitenguliwa basi amekataa nafasi hiyo...

Jitahidi kusoma kwa makini kila mstali uweze kupata uelewa...

Wenzio wakina Mbowe, Lema nk walipanda ndege kutoka dar kwenda ktk sherehe mwanza kwa Magufuli, walikuwa wana elewa haya. Wangeweza kusema wana umwa lakini ndio hivyo haikuwezekana
Nimesoma kote niambie panaposema kukataa kuhudhuria sherehe ya rais au kukataa teuzi ni uhani .ujinga muwe mnaficha .kina mbowe hawakuwahi kuwa na kiburi dhidi ya magu walidhan labda ataacha ujinga wake kwa kujua anaheshimiwa mbona mwishoni walimkatia mguu kabisa .mbona huwa wanaalikwa kwa barua kwenye uapisho wa rais hawa3ndi .chadema walitoka nje alipoingia bungeni magu kutomtambua kama rais mbona hawakushikwa .ujinga wako uufiche
 
Uhaini ni kosa na sheria inayolizaa imelipa maana yake na ni kitendo gani kinaweza kuhesabiwa kuwa uhaini, acheni maneno ya mtaani.

Nyie ndio wale wale mnamkamata mtu Aishi Hotel anapanga mikakati ya kushinda uchaguzi halafu mnaenda kumshtaki kwa ugaidi.
Chadema walitoka nje akiingia magu bungeni mbona hawakupewa kesi ya uhaini
 
Hivi mkuu kutoka DGIS mpaka Chief of staff ni demotion kweli?[emoji848]
I think there must be something wrong au mama alipanga amshushe kiaina bila kelele.
Hawa wanawake wana ongozwa na visirani sometimes
 
Hii nchi bhana[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Mkuu wa TISS leo anamka hana pa kwendaaa...!! Hana wa kumpa amriii labda afanye biashara zakee kama alikumbuka kufungua miradi[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Sijachukia kabisa, ata wewe ungekuwa raisi unahaki ya kuweka watu unaodhani wanakuelewa unalenga nini katika nafasi sensitive za ushauri provided wana right qualifications.

Halikadhalika unapowatoa watu wenye nafasi nyeti ni muhimu kuzingatia heshima zao so tumia mbinu sahihi.

Kitendo cha kumtoa mtu kwenye nafasi yake, kumpeleka Ikulu; halafu kumtengua ni sawa na kusema nilisahau Ikulu utakuwa karibu na mimi wakati sitaki kufanya kazi na wewe kabisa.

Now that was disrespectful lakini raisi kuchagua anataka kufanya kazi na nani, jumlisha katiba inamruhusu ni haki yake kabisa.
Ninavyoona jamaa livutwa karibu iwe rahisi kumcontrol ila jamaa ana mambo yake so nahisi amegomra hiyo nafasii...! Ila kama hakugomea bhasi mama atamchapa ubaloziii ili asiwepo around kabisaa...
 
Appointments za hawa jamaa wakishaondoka au kuondolewa kwenye wadhifa, inakuwa very sensitive.
Wanaweza hata kupotea!
Wana siri nyingi mno.
Hapo hata wale wafuasi wake simu zao zinaunganishwa kuona Siri zinazotoka.

Hii ndio Ile tunayoanghalia kwenye movie za kijasusi.

Ila anajua kabisa kupotezwa ni nje nje
 
Hakuna mtu anayehudumu TISS na ambaye ni Member wa TISS akateuliwa kazi yoyote na Rais akagoma.

Rais atakuwa amestuka kuwa kumuweka Ikulu karibu yake mtu aliyekuwa anaendesha mission za kuonea wapinzani kutaathiri mipango yake ya zile R nne
Ina maana rais anateua bila kufanya vetting?
 
Umejuaje kama aliwahi kulima au umejuaje kama yuko interested na kilimo sasa hivi. Diwani pale Magu alipofariki alijua kabisa kile cheo hakai, surprisingly amekaa kaa kidogo tofauti na uzoefu wa medani ulivyoonyesha. Haijamshtua wala haijawashtua wenye medani yao kama alivyoondoka Modestus Kipilimba.

Na kwa common sense hapo ikulu huo ukatibu alikuwa amepewa kama stopgap
Mbona kama huyu jamaa alitumbuliwa na magu?
 
Hapo kuna shida katika kamati ya mapendekezo na teuzi. Vipi kuhusu washauri wa raisi hawakuliona hilo mapema?
 

Attachments

  • B49A3415-0062-47B6-85DA-B81B7DF3BA54.jpeg
    B49A3415-0062-47B6-85DA-B81B7DF3BA54.jpeg
    64.9 KB · Views: 8
Back
Top Bottom