Maulaga59
JF-Expert Member
- Feb 1, 2021
- 2,984
- 2,971
Kama aliweza kushughulikiwa Lt Gen Imran... atakuwa Kamishna wa Polisi
Kombe hakufikia cheo cha Lt General, wacha kudanganya watu hapa!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kama aliweza kushughulikiwa Lt Gen Imran... atakuwa Kamishna wa Polisi
Tatizo nyinyi mmejiaminisha matatizo ya watu kutekwa na kupotea yameanzia kwenye utawala wa Magufuli na Diwani, mambo ya Watu kupotea au kufa yapo tokea enzi za Nyerere tena enzi za nyerere hata mitandao vyombo vya habari,hakukuwepo kama Sasahivi, hivyo walifanya walivyotaka enzi hizo tunasikiliza redio Tanzania (tbc)hata mtu wako akipotezwa hauwezi fungua mdomo kusema, Hata Sasahivi bado watu wanapotea tu sema bado mna mahaba na mama, kwenye utawala kuko hivyo kuna watu lazima waminywe ndipo unaweza kuendesha mchi maana wengine wako kwa ajili ya vurugu tu.
Kiutani utani, ndiye yeye 2025Hivi niguse ninuke Yuko WAPI!!?
Are you sure with this nonsence?Mamba anatisha akiwa ndani ya maji, nje ya maji màmba ni sawa na mjusi tu.
Saa hizi ukimkuta Diwani Athman hata ukimtemea mate anaweza kukuomba wewe msamaha.
Mtoa mada umem over estimate Diwani bila sababu, I assure you he is nobody in this country.
Tatizo hakuna usaili kabla ya teuzi.Tatizo nini
Kombe hakufikia cheo cha Lt General, wacha kudanganya watu hapa!
Mie nafikiri fikiri labda mkurugenzi alikuwa kemp iliyokuwa haimtaki Bi Mkora maana tunaona mshikaki kama vile bado upo jikoni?Watu wenye mamlaka wanachukia sana vitu viwili, usaliti na dharau. Hivyo vitu viwili sio rahisi kusamehewa.
Imrani Kombe RIPAmeukataa uteuzi na siyo kutenguliwa, niliandika hapa juzi! Iweje Mkurugenzi TISS kupelekwa Ikulu?
Diwani ni mwenye kujitambua, ameukataa uteuzi ule. Diwani ana uzoefu na serikali zaidi ya nne za CCM.
Diwani ni afisa aliehudumu idara mchanganyiko za nchi hii kwa kiwango cha juu. Diwani anaijua michezo yote ya CCM na magenge yake. Diwani sio Kabudi au Lukuvi!
Diwani ndiye afisa mwenye siri nzito za kilichojiri kati ya serikali hizi mbili. Serikali ya Magufuli na hii ya Samia!
Pia ieleweke yeye ndiye alikuwa madarakani wakati JPM anafariki Dunia. Yote yaliyojiri katikati hapo, ni Diwani ndiye anaeyajua!
Diwani sio wa kubezwa! Diwani anastahili kupewa ulinzi kwa usalama wake! Kitendo cha kuikataa safe house, ina maana amekataa ku surrender mawasiliano yake yote ili kuanza kutumia mapya ya Safe House!
Na mengi bado yanakuja, maana kadri inavyonyesha ndio matobo yanavyozidi kuonekana.
"Rais Samia atengua uteuzi wa Diwani Athumani"
Mwananchinewspaper
Alhamisi, 05/01/2023.
Rais Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Katibu Mkuu wa Ikulu, Kamishna Diwani Athumani uliodumu kwa siku mbili baada ya kuteuliwa akitokea Idara ya Usalama TISS.
Kamishna Diwani aliteuliwa Januari 3, 2023 kuwa Katibu Mkuu wa Ikulu, akitokea katika wadhifa wa Mkurungezi Mkuu wa TISS, nafasi aliyohudumu kwa siku 1,210 tangu alipoteuliwa na Rais wa awamu ya tano, Hayati John Magufuli.
Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi Januari 5, 2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus, imeeleza kuwa nafasi ya Diwani imechukuliwa na Mululi Mahendeka aliyekuwa ofisa mwandimizi wa Ofisi ya Rais, Ikulu.
Alamsikhi
10101.
Lakini si watajua tu kuwa wanachunguzwa, sababu hao wakurugenzi wa hizo Idara au taasisi nao si wamewaweka watu wao binafsi au wasaidizi wao kufuatilia nani anaewafuatilia!!Hata mkurugenzi wa TISS, IGP na CDF wanafanyiwa ujasusi pia ili kuwa na uhakika kuwa wakati wote wapo kwenye mstari.
Kwani kukataa uteuzi ni lazima iwe expressly? Si inawezekana kabisa mtu kukataa impliedly kwa kufanya jambo la kukera au la ovyo ili aliyekuteua akutengue. Yeye aone amekufukuza na kumbe amefanya kile ulichotaka akifanye. Chukulia hii, kwamba kuna uwezekano kweli alifanya makosa akiwa Mkuu wa TISS akaondolewa hapo kama adhabu ila hajakubaliana na adhabu kaamua kuikataa kwa kufanya jambo lingine bovu ili aondokane na fedheha ya kukaa ikulu.Huyu bila shaka kuna makosa amefanya, akashushwa na kupelekwa karibu ili achunguzwe zaidi mienendo yake. Huenda ndani ya muda mfupi wa uteuzi kuna taarifa mbaya zaidi zimemfikia mkuu wa nchi kiasi cha kuonekana kuwa hafai hata kwa nafasi hiyo au pengine anafikiriwa kwa nafasi tofauti na hiyo.
Mkuu, Katiba ya JMT haina mambo ya awamu. Hakuna awamu ya 1 au ya 6 kikatiba. Mambo ya awamu ni ya mazoea tu, sio ya kisheria (kikatiba)Nafikiri kitendo cha kulazimisha iwe awamu ya sita na sio ya tano kikatiba ndio kitaisumbua nchi sana mpaka kufika 2025
Siku ya kwanza, SSH kuwa 'Rais' alitangaza maombolezo ya siku 14 badala ya 21. Hii inatosha kukuaminisha kuwa ama Rais anajiongoza mwenyewe ama hiyo taasis flaani kuubwa inafanya makosa tu sababu ina binadamu na sio miungu. Kama inafanya makosa, kuna uwezekano wakawa hawajafikiri yote kama ulivyomuuliza mleta mada. Ni binadamu tu kama walivyo wengineMkuu, Urais ni taasisi flaan kuuuuuubwa mno. Anaekaa kwenye kiti cha Urais hajiongozi mwenyewe katika maamuzi!
Hivi mkuu Stuxnet baada ya kumjibu jiwe kuwa amekuinua siku ile pale butimba, alikupeleka wapi? maana sijakuona tena.
Fasihi haiko wazi kwa wote, mpaka uwe na akili ndiyo utaelewa sarcasm au satire iliyotumika kwenye "kutema mate". Nendeni shule UVCCM mtanishukuru baadayeNao unakua wewe. Eti umtemee mate.! Akili za vijana wa bavicha hizi
Nina utefu wa Ft 5,11", yaani karibu ft 6,sijui kama kwa Watanzania Mimi naitwa mfupiAkili zako fupi kama ulivyo