Diwani Athumani Msuya atenguliwa Ikulu

Mimi si mdau wa hiz mambo lakini huyo D-1 aelewe fika kwamba kuwa na siri za nchi si sababu ya kuwa na jeuri.Yeye hatakua DGIS mstaafu wa kwanza kustaafishwa pumzi zake.Anajua fika yaliyompata yule Lt.Gen kule Arusha mwaka 96.

Msimchonganishe na serikali na chama kwa vi thread vyenu hapa jukwaan kila uchwao aonekane hatii mamlaka za uteuzi
 



Hapana tumekataa utetezi huo wa kidhalimu.

Akipatikana mwenye kuleta fujo apelekwe kushtakiwa kwenye vyombo vya sheria na sio kumteka na kumpoteza au kumfanyia mateso,

Na hizi vurugu sheria iweke kipimo cha kujua kuwa ukifanyika hivi ni vurugu Au ni haki ya mwananchi.

Hata swala la uchochezi sheria iweke kipimo na isiwe ni mtazamo wa mtu Au kikundi cha watu fulani.

Usituambie Eti serikalini zote Duniani zinatesa na kuua watu , hapana unless iwe wamejiwekea kwenye sheria zao,

Kuua , kutesa ni kinyume na haki za kibinadamu,

Nchi yetu ni miongoni mwa nchi zilizo ridhia kuingia kwenye mikataba ya UN kuhusu kutunza na kuzingatia haki za binadamu.

Kwa hiyo usipotoshe kutaka ku-justify matendo maovu ya Viongozi wenye dhamana husika.
 
Mfano;

Katiba imetuhusu maandamo ya amani wazi kabisa,
Lakini ni ajabu kabisa tunapataga Viongozi ambao hawataki kusikia wala kuona jambo hilo,

Na cha ajabu wana apa kwa vitabu vitakatifu mbele za Mwenyezi Mungu na watu kuwa wataifuata Katiba ya JMT lakini kisha wanaenda kinyume?!

Imeandikwa; “Mwenyezi Mungu hadhihakiwi “

Tumuogope Mungu sana !
 
Tunataka uongozi wenye misingi ya sheria na Haki.

Actually ndio maana ya uongozi bora!

Kinyume chake ni uongozi dhaifu na dhalimu.
 
Are you sure with this nonsence?

Diwani Sasa hivi aitishe press conference unazani Nini kitatokea? Dont undermine that man.

Hata uchaguzi wa 2025 akiamua asimame upande wa mpanzani wa CCM na aongea any shit Raia wataamini tu.

Once a TISS is always a TISS.
 
Ewe mwanadamu, nimekuweka kuwa mlinzi wa taifa la Israel, Basi nikikwambia mlinde mtu huyu, na yule mtu akapotea nawe usijue alikokwenda, roho yako itakuwa mahali pa roho yake
 
Watu wenye mamlaka wanachukia sana vitu viwili, usaliti na dharau. Hivyo vitu viwili sio rahisi kusamehewa.
Mie nafikiri fikiri labda mkurugenzi alikuwa kemp iliyokuwa haimtaki Bi Mkora maana tunaona mshikaki kama vile bado upo jikoni?
 
Imrani Kombe RIP
 
Hata mkurugenzi wa TISS, IGP na CDF wanafanyiwa ujasusi pia ili kuwa na uhakika kuwa wakati wote wapo kwenye mstari.
Lakini si watajua tu kuwa wanachunguzwa, sababu hao wakurugenzi wa hizo Idara au taasisi nao si wamewaweka watu wao binafsi au wasaidizi wao kufuatilia nani anaewafuatilia!!


Kwani kukataa uteuzi ni lazima iwe expressly? Si inawezekana kabisa mtu kukataa impliedly kwa kufanya jambo la kukera au la ovyo ili aliyekuteua akutengue. Yeye aone amekufukuza na kumbe amefanya kile ulichotaka akifanye. Chukulia hii, kwamba kuna uwezekano kweli alifanya makosa akiwa Mkuu wa TISS akaondolewa hapo kama adhabu ila hajakubaliana na adhabu kaamua kuikataa kwa kufanya jambo lingine bovu ili aondokane na fedheha ya kukaa ikulu.
 
Nafikiri kitendo cha kulazimisha iwe awamu ya sita na sio ya tano kikatiba ndio kitaisumbua nchi sana mpaka kufika 2025
Mkuu, Katiba ya JMT haina mambo ya awamu. Hakuna awamu ya 1 au ya 6 kikatiba. Mambo ya awamu ni ya mazoea tu, sio ya kisheria (kikatiba)

Mkuu, Urais ni taasisi flaan kuuuuuubwa mno. Anaekaa kwenye kiti cha Urais hajiongozi mwenyewe katika maamuzi!
Siku ya kwanza, SSH kuwa 'Rais' alitangaza maombolezo ya siku 14 badala ya 21. Hii inatosha kukuaminisha kuwa ama Rais anajiongoza mwenyewe ama hiyo taasis flaani kuubwa inafanya makosa tu sababu ina binadamu na sio miungu. Kama inafanya makosa, kuna uwezekano wakawa hawajafikiri yote kama ulivyomuuliza mleta mada. Ni binadamu tu kama walivyo wengine
 
Hahahaha, Gereza la Ukerewe. Hivi unajuwa nini kilimleta mle Gerezani? Alikuja kiwatoa wale walioshikwa na dhahabu. Polisi hawakujua kuwa ni mchongo wake na Kagame wakawakamata. Ila wajinga wanasema Magufuli alikuwa mzalendo, nawadharau sana
Hivi mkuu Stuxnet baada ya kumjibu jiwe kuwa amekuinua siku ile pale butimba, alikupeleka wapi? maana sijakuona tena.
 
Nao unakua wewe. Eti umtemee mate.! Akili za vijana wa bavicha hizi
Fasihi haiko wazi kwa wote, mpaka uwe na akili ndiyo utaelewa sarcasm au satire iliyotumika kwenye "kutema mate". Nendeni shule UVCCM mtanishukuru baadaye
 
naamini hakuna baya litakalotokea, TZ kanyaga twende. kwani tangu uhuru hakuna mwenye cheo kama chake aliwahi kuondolewa?!?,kama yupo au wapo nini kilitokea?!?. KANYAGA TWENDE MAMA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…