King klax
JF-Expert Member
- Jul 10, 2015
- 4,307
- 2,754
Tatizo tumboooooo a.k.a ulaji ulaji chezea chama changu pendwa chichiemu
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Loose talk at its best!Tatizo tumboooooo a.k.a ulaji ulaji chezea chama changu pendwa chichiemu
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu;Hapa kazi tu. Jamaa aliwachana ukweli wakam'piss off'.
Naona naye ameamua kwenda upande sahihi.
HAPA KAZI TU
Diwani wa Kata ya Ngarenaro kwa tiketi ya CHADEMA, Isaya Doita aliyemtuhumu Godbless Lema kuwa hajui kazi na majukumu yake kama kiongozi wa juu wa CHADEMA na pia kama Mbunge amefukuzwa uanachama kwa kosa la kukiuka kanuni na misingi ya uanachama wa chama.
Kufukuzwa Uanachama kunamfanya kupoteza hata Udiwani wa Kata ya Ngarenaro kwa sababu Diwani lazima awe na udhamini kutoka chama cha siasa.
Ikumbukwe kuwa Juzi kupitia vyombo vya habari, Diwani Isaya alimtuhumu vikali Mbunge Godbless Lema kuwa hajitambui na hajui majukumu yake kama Mbunge, Mwenyekiti wa Kanda na Mjumbe wa Kamati Kuu ambapo imesababisha chama kudhoofika na kukimbiwa na baadhi ya Madiwani wa Jiji la Arusha.
Kufukuzwa kwa Diwani Isaya Doita kunafanya awe Diwani wa 14 katika Jiji la Arusha kwa tiketi ya CHADEMA aliyeondoka CHADEMA baada ya Uchaguzi Mkuu 2015.
Ukitaka kusoma na kuangalia video ya tuhuma unaweza kugonga Link hii:
Link > CHADEMA Arusha ‘’kwafuka moshi’’; Godbless Lema aambiwa hajitambui na hajui majukumu yake
Barua ya kumvua uanachama
![]()
Video ya tuhuma kwa Godbless Lema
Mwenyewe nimeshangaa mbona huu uzi wa zamani umepandishwa huku, kumbe kaleta habari ya muendelezo wa mtu yule yule halafu akachanganya na visababu vyake vitatu anajidanganya kaleta uzi mpya, ooh Chadema Arusha kuna matatizo makubwa, mbona kila siku wanaimba huu wimbo!, hao watu wote wanafahamika, huyo Doita, alitongozwa na CCM halina mjadala, huyo Bananga nae anasumbuliwa na wivu wa madaraka anapewa support na yule wakili wa CCM, Kisandu; nothing new, km ambavyo alichokileta hapa hakina jipya, ndio maana kimeunganishwa.Alichofanya modereta ni sahihi kabisa,ulichokiandika hakuna jipya bali ulitaka kukumbusha yaliyojiri kwa madiwani walioamua kusaliti kazi waliyotumwa na wapiga kura wao.
Kwamaana nyingine na wewe unaunga juhudi mkono kwa njia ya kukoleza kile walichokisema kila diwani aliyeunga juhudi.Hivyo kuwa mpole,watanzania wameelimika na wanaelewa nguvu kubwa mnayotumia kutukoroga kisiasa,huku lengo la msingi la kituletea maendeleo ikiwa imewashinda.
Kiboko yenu ni tume huru ya uchaguzi.
Please Moderator;
Thead yangu ambayo mmeiweka kwenye namba 221 kwa nini mmeileta kwenye thread nyingine wakati habari zake ni tofauti?
Hata common sense inakataa kama hizi thread mbili zinaweza kuwa na ujumbe mmoja.
Acheni kufanya kazi nje ya spirit ya Jamiiforums!
Hamjaitendea haki Thread yangu ambayi mmeiweka kwenye namba 221.
Hivi kweli kuna Maendeleo yoyote yamefanyika kwenye miaka mitano ya JPM? Mimi nasikia Mapambio ya nyimbo za kusifu Maendeleo tu! No new job, no salary increment, Mazao ya biashara wakulima wanalipwa malipo duni. Serikali inaenda kwa mtindo wa teua tumbua, kuwapa ulaji waimba mapambio. Dereva anakotupeleka hata maCCM hakujui ndo maana nafasi za Teuzi zao zinachukuliwa na waunga Juhudi kutoka CHADEMA waweza kuzani maCCM wote wana akili kama za Magonjwa Mtambuka.Uwa najiuliza ni kwa nin kila anayeondoka Chadema miaka hii ni lazima ajiunge na Ccm,,Mana kila utakayemsikia najiunga na Ccm kuunga juhudi. Kwa uelewa wangu ni kwamba maendeleo hayataletwa na chama Ila yataletwa na wananchi wenyewe wakiwa na mioyo thabiti ya kimaendeleo.
Huyo jamaa anaishi kwenye ile kauli "uongo ukirudiwa mara nyingi hugeuka ukweli"Hapo hapo kwenye post yako namba 221, huwa ninacheka sana ninaposikia kiongozi amehama cdm kwakuwa kuna matatizo makubwa sana, kisha anahamia ccm! Huyo kiongozi inaonyesha amehamia ccm kwakuwa hakuna matatizo kabisa, na yeye hawezi kukaa kwenye matatizo maana sio mtu wa kutatua matatizo. Huu mtindo wa kuhama viongozi sehemu kubwa unsongozwa na maslahi binafsi, na ndio maana kiongozi anahama, lakini wananchi hawafuati. tumeushudia sana kwenye chaguzi za marudio.
Tulishuhudia kwa macho yetu, kote kulikofanyika chaguzi za marudio baada ya wapinzani kuhamia ccm, ukiachia uhayawani, rafu na ukatili wa wazi ili kiongozi aliyehamia ccm atangazwe mshindi kwa maelekezo ya rais, wapiga kura walikuwa chini ya asilimia 20 ya waliopiga wakati wa uchaguzi mkuu. Hiyo inaonyesha hao viongozi wanahama kwa kuhongwa, na wengine ni bendera fuata ili kulinda maslahi yao binafsi, na sio kutokana na sababu wanazohadaa nazo wananchi ili kuhamia ccm. Ila uzuri uchaguzi ni mwaka huu, iwapo kutakuwa na tume huru ya uchaguzi tutajua ukweli wa hao wanaohama kuwa ni itikadi wanafuata au mlo. Huu uhamaji naufananisha na muumini wa kikristo anapoona tatizo kwa uongozi wa dhehebu lake, anahamia kwenye uisilamu!
Alimwambia Lema ukweli juu ya mapungufu yake kama kiongozi wa kanda.Mkuu;
Una maana unaposema aliwachana?
Mojawapo ya tatizo kubwa ambalo chama cha kisiasa hukumbana nalo ni pale kinapoanza kujikusanya kuwa kundi moja lenye lengo moja. CHADEMA kwa sasa inapitia kwenye tatizo hili.
Historia inaonyesha NCCR-Mageuzi ilipoanza kujikusanya kama kundi moja ilijikuta ikiwa nje kama chama kikuu cha upinzani. CUF pia wakaanza kujikusanya lakini nao pia wakajikuta wakiwa nje kama chama kikuu cha upinzani. Kuna uwezekano pia CHADEMA wakapitia njia ileile na kujikuta nje kama chama kikuu cha upinzani.
Chama cha siasa kinapokuwa hakina lengo halisi huwa ni rahisi sana kwa baadhi ya wanachama kuficha malengo yao halisi.
Kujikusanya huku kwa chama kuwa kundi moja huibua makundi matatu kama ifuatavyo;
Kundi la kwanza ni baadhi ya wanachama ambao ama wanakuwa wakubwa zaidi ya chama na kutaka kunyenyekewa au kila wanaloliamua wao lazima na wengine walifuate hata kama ni kwa maslahi binafsi.
Kundi la pili ni kuibuka kwa wanachama ambao malengo yao ni maslahi binafsi ambayo yamejificha na sio lengo halisi kama chama cha kutaka kushika dola.
Kundi la tatu ni wanachama ambao wanaamini lengo kuu la chama na kulifuata lakini hawako tayari kuishi katika unafiki wa kukubali kuendeshwa na kundi la kwanza na kuwa ‘’bendera fuata upepo’’.
Kwa mtu anayemfahamu huyu Diwani wa Kata ya Ngarenaro kwa tiketi ya CHADEMA, Isaya Doita atakubaliana na mimi kuwa alikuwa ni kati ya wanachama wa kundi la tatu nililolitaja. Ni Diwani ambaye aliheshimiwa sana na wananchi wa Jiji la Arusha lakini kikubwa zaidi alikuwa mtetezi mahili wa lengo kuu cha chama cha siasa.
Kuondoka CHADEMA kwa Diwani Isaya Doita kunatoa picha kubwa kuwa CHADEMA katika Jiji la Arusha kuna tatizo kubwa na muda wa kulitatua unazidi kuwa mfinyu kabla ya Uchaguzi Mkuu mwaka huu.
Ninajua kuna baadhi ya watu hujenga fikra kwa kutumia hoja za kihemko (emotion reasoning) lakini ukweli hauwezi kudharauliwa kuwa CHADEMA katika Jiji la Arusha kuna tatizo kubwa.
Nakumbuka Mwezi January 2020, Diwani Isaya Doita alitoa tuhuma nzito zinazomuhusu Godbless Lema.
Kama unataka kusoma shutuma hizo unaweza kugonga;
LINK>>>CHADEMA Arusha ‘’kwafuka moshi’’; Godbless Lema aambiwa hajitambui na hajui majukumu yake
Baadaye aliibuka tena Diwani wa Kata ya Sombetini Katika Jiji la Arusha kwa tiketi ya CHADEMA, Ally Bananga na kutoa shutuma nyingine kwa Godbless Lema.
Kama unataka kusoma shutuma hizo unaweza kugonga;
LINK>>>Diwani wa CHADEMA, Ally Bananga amwambia Godbless Lema aache ndoto na kumpangia marafiki!
Jana Diwani Isaya Doita amejiunga CCM akiambatana na baadhi ya Madiwani wengine wa tiketi ya CHADEMA katika Jiji la Arusha.
VIDEO kuhusu alichokisema Diwani Isaya Doita baada ya kujiunga CCM.