Diwani Isaya Doita aliyemtuhumu Godbless Lema afukuzwa Uanachama

Please Moderator;
Thead yangu ambayo mmeiweka kwenye namba 221 kwa nini mmeileta kwenye thread nyingine wakati habari zake ni tofauti?

Hata common sense inakataa kama hizi thread mbili zinaweza kuwa na ujumbe mmoja.

Acheni kufanya kazi nje ya spirit ya Jamiiforums!

Hamjaitendea haki Thread yangu ambayi mmeiweka kwenye namba 221.
 
MsemajiUkweli,
Tatizo mode wanajifanya wanajua Sana kuunganisha news , sku hzi hii platform inaongozwa na watu back Sana , wapo kisiasa siasa tu na uchama mwingi , mtu akikosoa chadema anapigwa Ban , chama chenyewe kinaenda kujifia ...
 
MsemajiUkweli,
Alichofanya modereta ni sahihi kabisa, ulichokiandika hakuna jipya bali ulitaka kukumbusha yaliyojiri kwa madiwani walioamua kusaliti kazi waliyotumwa na wapiga kura wao.
Kwamaana nyingine na wewe unaunga juhudi mkono kwa njia ya kukoleza kile walichokisema kila diwani aliyeunga juhudi.

Hivyo kuwa mpole, watanzania wameelimika na wanaelewa nguvu kubwa mnayotumia kutukoroga kisiasa,huku lengo la msingi la kituletea maendeleo ikiwa imewashinda.
Kiboko yenu ni tume huru ya uchaguzi.
 
Kiukweli Lema ni mbunge duni sana nadhani pia ameshiba mishahara na posho miaka kumi aliyoipata,alipaswa kuheshimu watu wake at least awaachie alama kwa utendaji na kujali matatizo yao!

Anachojua nikupost familia yake insta kila uchao badala ya kuhangaika na wenye uhitaji,sijawahi muona amepost anafanya kazi za kijamii,kusaidia vyoo mashuleni,hospitalini au hata yatima. Hata kuchukua yatima mmoja akamlea?!?

Kiufupi Lema sio mheshimiwa nikijana mhuni aliyetake advantage ya upinzani arusha kujineemesha na tatizo ni chama kinamkuza wakati hana lamaana afanyalo. Anajidai mpambanaji lkn Hanna anachopambania ni kutafuta sifa za kuonekana jasiri kwa kuropoka badala ya ujasiri wa kazi.

Hivi viongozi chadema hawawafuatilii wabunge wake kama tuonavyo kwa ccm? Katibu Ccm anaheshimika mmna hats mwenezi lkn kwa chadema mambo ni hovyo kabisa,wabunge wote wakuchaguliwa na wa viti maalumu wanakula tuu maisha hamna lolote lakiubunifu, stupid kabisa na lazma tuwapige chini
 
Uwa najiuliza ni kwa nin kila anayeondoka Chadema miaka hii ni lazima ajiunge na Ccm,,Mana kila utakayemsikia najiunga na Ccm kuunga juhudi. Kwa uelewa wangu ni kwamba maendeleo hayataletwa na chama Ila yataletwa na wananchi wenyewe wakiwa na mioyo thabiti ya kimaendeleo.
 
Mwenyewe nimeshangaa mbona huu uzi wa zamani umepandishwa huku, kumbe kaleta habari ya muendelezo wa mtu yule yule halafu akachanganya na visababu vyake vitatu anajidanganya kaleta uzi mpya, ooh Chadema Arusha kuna matatizo makubwa, mbona kila siku wanaimba huu wimbo!, hao watu wote wanafahamika, huyo Doita, alitongozwa na CCM halina mjadala, huyo Bananga nae anasumbuliwa na wivu wa madaraka anapewa support na yule wakili wa CCM, Kisandu; nothing new, km ambavyo alichokileta hapa hakina jipya, ndio maana kimeunganishwa.

Halafu mtu mzima kulia kisa uzi umeunganishwa ni aibu kwa taifa, anaonesha ni kwa jinsi gani anapenda kuripoti umbea kuhusu Chadema.



Sent using Jamii Forums mobile app
 

Hapo hapo kwenye post yako namba 221, huwa ninacheka sana ninaposikia kiongozi amehama cdm kwakuwa kuna matatizo makubwa sana, kisha anahamia ccm! Huyo kiongozi inaonyesha amehamia ccm kwakuwa hakuna matatizo kabisa, na yeye hawezi kukaa kwenye matatizo maana sio mtu wa kutatua matatizo. Huu mtindo wa kuhama viongozi sehemu kubwa unsongozwa na maslahi binafsi, na ndio maana kiongozi anahama, lakini wananchi hawafuati. tumeushudia sana kwenye chaguzi za marudio.

Tulishuhudia kwa macho yetu, kote kulikofanyika chaguzi za marudio baada ya wapinzani kuhamia ccm, ukiachia uhayawani, rafu na ukatili wa wazi ili kiongozi aliyehamia ccm atangazwe mshindi kwa maelekezo ya rais, wapiga kura walikuwa chini ya asilimia 20 ya waliopiga wakati wa uchaguzi mkuu. Hiyo inaonyesha hao viongozi wanahama kwa kuhongwa, na wengine ni bendera fuata ili kulinda maslahi yao binafsi, na sio kutokana na sababu wanazohadaa nazo wananchi ili kuhamia ccm. Ila uzuri uchaguzi ni mwaka huu, iwapo kutakuwa na tume huru ya uchaguzi tutajua ukweli wa hao wanaohama kuwa ni itikadi wanafuata au mlo. Huu uhamaji naufananisha na muumini wa kikristo anapoona tatizo kwa uongozi wa dhehebu lake, anahamia kwenye uisilamu!
 
Hivi kweli kuna Maendeleo yoyote yamefanyika kwenye miaka mitano ya JPM? Mimi nasikia Mapambio ya nyimbo za kusifu Maendeleo tu! No new job, no salary increment, Mazao ya biashara wakulima wanalipwa malipo duni. Serikali inaenda kwa mtindo wa teua tumbua, kuwapa ulaji waimba mapambio. Dereva anakotupeleka hata maCCM hakujui ndo maana nafasi za Teuzi zao zinachukuliwa na waunga Juhudi kutoka CHADEMA waweza kuzani maCCM wote wana akili kama za Magonjwa Mtambuka.
 
Huyo jamaa anaishi kwenye ile kauli "uongo ukirudiwa mara nyingi hugeuka ukweli"

Hajui wanaodanganywa ni wajinga tu, na wajinga hawawezi kuwa wote!.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu;
Una maana unaposema aliwachana?
Alimwambia Lema ukweli juu ya mapungufu yake kama kiongozi wa kanda.
Badala ya kuzifanyia kazi hoja zake wakamfukuza uanachama.
Matokeo yake ameenda upande ambao hauna majigambo na wanajisahihisha pale wanapokosea.
Angalizo kwa chadema, muda huu watatue kero zao ndani ya chama vinginevyo wasijekusingizia wameibiwa kura.
 
Kumbe kawahiwa. Now the value of the bargain will be drastically reduced by 95%.
 
Huyo katibu wa Muriet si anajitafutia kesi? Anakabidhi vipi bendera, mihuri na makabrasha mengine kwa watu wasio husika? Huo si wizi kwa sababu havikuwa vyake? Na hao wanaopokea mali ya wizi hadharani wanaamini nini? Hivi kweli mwaka mmoja aliotumikia huyu kijana kama Katibu unatosha kufikia maamuzi kama haya? Kwa nini watu wasihisi alikuwa na agenda yake toka mwanzo ya kuiba mali ya chama chake? Huu kweli ni upuuzi wa kupitiliza. Ofisi inakabidhiwa kwa mrithi wa ofisi hiyo na si mwengine. Inasikitisha sana.

Amandla........
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…