Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,236
- 10,774
Diwani wa kata ya Igumbilo Manispaa ya Iringa Jackson Chatanda ametoa msaada wa sahani 300 kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Ulonge, hatua iliyolenga kutatua changamoto kubwa ya ulaji iliyokuwa ikiikabili shule hiyo kwa muda mrefu.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka shuleni hapo, wanafunzi wengi walikuwa hawana sahani za chakula, hali iliyosababisha ugumu mkubwa wakati wa utoaji wa chakula cha mchana. Kutokana na uhaba huo, wanafunzi walilazimika kusubiriana kula kwa kubadilishana sahani chache zilizokuwepo.
Mwalimu mkuu wa shule Abas Mijinga alisema tatizo hilo halikuathiri tu lishe ya wanafunzi, bali pia liliathiri ratiba za masomo. Wanafunzi walikuwa wakichelewa kurejea darasani baada ya muda wa chakula, wakisubiri wenzao wamalize kula ndipo nao wapate sahani.
Mijinga ameeleza kuwa Hali hiyo ilisababisha upotevu wa muda wa masomo na kupunguza umakini darasani.
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya msaada huo, Chatanda alisema ameguswa na changamoto zinazowakabili wanafunzi hao na kuahidi kuendelea kushirikiana na wadau wengine wa elimu kuboresha mazingira ya kujifunzia.
“Watoto hawa wanahitaji mazingira bora ili waweze kusoma kwa bidii na kufikia ndoto zao. Ni wajibu wetu kama viongozi kuhakikisha wanapata mahitaji ya msingi, ikiwemo vifaa vya chakula,” alisema diwani huyo.
Baadhi ya wanafunzi walionyesha furaha yao baada ya kupokea sahani mpya, wakisema sasa hawatalazimika tena kusubiri wenzao ili wapate chakula. Walimu pia walieleza matumaini yao kuwa msaada huo utasaidia kurejesha nidhamu ya muda na kuongeza ufanisi wa masomo.
Hatua hiyo imepongezwa pia na wazazi pamoja na jamii ya Ulonge, wakieleza kuwa diwani huyo ni mfano wa uongozi unaojali ustawi wa watoto na maendeleo ya elimu kwa ujumla.
Kuna wakati tukubaliane kuwa 90% ya viongozi wetu haswa katika awamu hii wana utimamu mdogo sana haswa kwenye kutatua changamoto za wananchi. Yaani karne ya 21 leo Diwani anatuletea porojo kuwa anatoa msaada wa sahani? SAHANI? Sahani ambazo hata uongozi wa shule ukiwaambia wazazi wanaenda kununua mnadani au gulioni yaani SAHANI ya 1000? Seriously kabsa!
Ni nani ambaye ameturoga? Yaani sahani 300 ndizo zimekuwa mafanikio kwa diwani? Sidhani kama hata wazazi waliopongeza hii futuhi ni wazazi timamu, ila nina uhakika kuwa wazazi waliozungumza huu upupu ni wanachama wa CCM.
Yaani badala ya kuzungumza kuhusu masuala yanayohitaji utatuzi wa maana, watu wanazungumzia sahani? SAHANI? tena moja? Je hawa watoto wana vitabu vya kutosha vya kujifunzia na kusoma? Je mazingira na miundombinu ya shule za Iringa yapo vizuri kiasi kwamba leo Sahani zimekuwa ndio mafanikio?
Katika mahafali za darasa la saba, je risala za wahitimu wamewahi kusema kuwa kuna changamoto za sahani? Shule ya Msingi Ulonge ina changamoto kibao ambazo kwa hiyo laki 3 ingekwenda kusaidia pakubwa sana. Hawa wanafunzi wana changamoto nyingi ila tumeishia kuwapelekea sahani? outrageous! 😠 hiyo furaha ipo wapi kwa watoto? Ni kama wanajiuliza hivi kweli tunaletewa sahani kama msaada!? 😃
Mijinga amekuwa mjinga kweli, yaani mtu mzima unashukuru diwani kukuletea sahani? Aiseee tunahitaji kupimwa utimamu. Yaani tuna viongozi wa ajabu kupita maelezo. Kwa maana hiyo Shule ya Msingi Ulonge imefurahi kabsa kupokea Sahani kama Msaada? Sawa bhana ngoja tusubirie mikeka ya Lucas Mwashambwa 😃