Nzega pamechafuka sana. Nilikuwa naongea jana na fundi magari wa gereji moja ya Nzega kwa simu, anasema kwa kila siku wanazika watu kati ya 4 na 7. Na inaonesha ni kweli. Nilikuwa Nzega wiki iliyopita, nilishangaa kuona karibia kila siku kuna watu makaburini. Mwanzoni nilidhani wanajengea makaburi kumbe ni maziko.
Ukanda wote huo - Tabora, Nzega, Shinyanga, pamechafuka. Ukipita maeneo hayo chukua tahadhari ya hali ya juu. Kama unalazimika kulala maeneo hayo, pengine ni busara kulala kwenye gari lako kuliko huko kwenye nyumba za wageni. Wiki hiyo nilipokuwa Nzega, alifariki mganga msaidizi mstaafu ndugu Mgarula kwa tatizo la upumuaji. Huyu alikuwa na duka la Dawa kata ya Lusu, eneo la Mwaluzwilo. Pia kuna jamaa 3 waliwahi kufanya kazi kwenye mgodi wa dhahabu wa Resolute, Nzega, wote wamefariki kwa tatizo la upumuaji.
Kuna rafiki yangu amefiwa na ndugu 4 mjini Shinyanga ndani ya wiki 3, wote tatizo la upumuaji.
Mwanza napo siyo salama. Kinachosaidia Mwanza kutoonekana kuna hili tatizo, ni uwingi wa watu. Ukiwa pale mjini siyo rahisi kusikia kila msiba. Ukitaka kujua ukubwa wa tatizo, zungumza na wahudumu wa afya wa hospitali ya Seketure. Ninaowafahamu mimi wamefariki kwa tatizo la upumuaji mjini Mwanza kwa mwezi wa kwanza ni wawili. Wote miili yao ilisafirishwa kwenda Kilimanjaro.
Kila inapowezekana, chukua tahadhari.
Sent using
Jamii Forums mobile app