carbohydates
JF-Expert Member
- Oct 13, 2026
- 260
- 607
Taharuki imezuka nchini Kenya baada ya polisi kumkamata Cyrus Kisavi Musyoka, diwani wa wadi ya Ikanga/Kyatune, Kaunti ya Kitui, akihusishwa na msururu wa visa vya wizi wa simu katika Jiji Kuu la Nairobi (CBD).
Maafisa wa Kituo cha Polisi Kamukunji walimnasa mtuhumiwa katika Mtaa wa Mfangano kufuatia uchunguzi wa kina na matumizi ya kamera za CCTV, ambazo zilimhusisha moja kwa moja na matukio matatu yaliyoripotiwa mwezi Agosti na Septemba 2026.
Aidha, imebainika kuwa Musyoka alikuwa na kesi ya awali yenye hati ya kukamatwa, baada ya kushindwa kufika mahakamani katika Kesi ya Jinai Na. 112/303/2024 iliyokuwa ikisikizwa katika Mahakama ya Makadara, ambapo alishitakiwa kwa kosa la wizi.
Kwa sasa yupo rumande akisubiri kufikishwa mahakamani, huku Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) ikisisitiza kuwa “hakuna aliye juu ya sheria” na kwamba uchunguzi utaendelea bila kujali hadhi au nafasi ya kijamii ya mtuhumiwa.
Tukio hili limeibua mshangao na maswali mazito kuhusu uadilifu wa viongozi wa umma, kwani kiongozi aliyechaguliwa na wananchi sasa anahusishwa na vitendo vya uhalifu wa mtaani.
Chanzo : Mwanzo tv Plus