Ninakumbuka zamani kidogo ndani ya UVCCM niliambiwa kuwa kuna prapaganda nyeusi (uongo kwa 100%), kijivu (mchanganyiko wa ukweli na uongo, 50% kwa 50%) na nyeupe (ukweli tupu). Kwa jinsi ilivyotangazwa kwenye TV hii ni propaganda nyeusi. Kama CCM bado tunaamini kuwa propaganda nyeusi za kuchafua wengine (Watu au Chama) kwa kusingizia na hata kutoa taarifa za uongo na za hatari kama hizi, nina wahakikishia gamba tunalodai tumejivua lilikuwa la kuzirai na sasa tumejivika gamba la mauti.
Shida mliyonayo nyie viongozi wa Chama changu (CCM) ni moja tu; hakuna kati yenu ambaye anauwezo wa kufanyia kazi madai ya Watanzania kwa sasa. Mmezoea vitu vya bure na kutumia wengine kwa faida yenu. Watanzania wa sasa hivi wamekwishachoka bla bla na usanii. Ninachoweza kuwaambia CCM itakufa amini msiamini kama tutaendelea kuwa wasanii na kutumia propaganda nyeusi eti kukirudishia chama "uhai". Watanzania tuliwavumilia kwa muda mrefu sana tukifikiri kuwa mtaamka lakini naona mnazidi kulala usingizi kuzidi ule wa pono.
Only The Truth will Set You (CCM) Free!! No more lies nor Tricks Will Make A Better, Healthier and Livable Tanzania. Wake up CCM!!!