Mimi kinachonisikitisha Kwa sasa, ni kuona Watanzania wengi wakiongezeka Kwa Kasi kuwa na chuki na Mzee Mbowe,
Na chuki Yao ikihusisha maswala magumumagumu Sana, Jambo la Kwanza unajiuliza
Je, Watanzania wamekumbwa na nini kiasi cha kumchukia hivi mh Mbowe?
Je, Mbowe Kwa sasa amekumbwa na gundu ghafla kiasi cha kukaa akisemwa semwa na kuchukiwa
Au, ni kweli kwamba yanayosemwa yanaukweli, na Kwa nini iwe nyakati hizi ambazo ukizipima zimekuwa ni nyakati ambazo joto la siasa limekuwa liko juu Sana?
Ni Kwa sababu aliokuwa akifanya nao mambo Kwa Siri wengi wao wemeamua Kuokoka na wengine wao kufukuzwa?
Kwa kuwa kazi ya shetani ukiamua kumtumikia ni lazima tu siku moja akuaibishe,Je shetani sasa ameamua aanze kumdharilisha mh.?
Lakini swali langu gumu hasa Kwa hao wanaotangaza maasi ya Mh!
Mnadhani kwamba yeye Mh, ameamua kujichoka ili Hali akijua kwamba Kwa namna yoyote iwavyo hawezi kuanza kujiingiza kwenye Moto huku akijiona, Mnadhani kwamba, ni rahisi kwake kukorofishana na watu wenye Siri zake ili ajikamatishe police?
Hizi sio mihemko tu ya kisiasa?
Na Kwa nini ninyi mnaomshambulia Mh, Kwa dhambi kubwa hizi zisizovumilika Kwa namna yoyote Ile, Kwa Taifa na Jamii, Kwa nini sasa mkajitokeza hadharani kutafuta wadhamini kama mtahitaji hivyo ili Mbowe afikishwe mahakamani mkiwa na ushahidi huu mnaoendelea kuandika humu
Na la sivyo, Chadema sasa mfike pahala muwafungilie mashitaka watu hawa, Kwa sababu tuhuma hizi zinaendelea kukichafua Chama na m/kit wenu,
Ama mh Mbowe sasa aingie mahakamani mwenyewe, Kwa Maana akinyamaza watu wataamini hivyo