Mshahara wa dhambi ni mauti, itakufaidia Nini ukipata wanawake wote duniani, alafu ukatupwa kwenye ziwa la Moto, kifo kinakuja, ipo siku kila mmoja atatoa hesabu ya aliyoyatenda duniani!
Yakobo 4:4
Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu.
Mathayo 16:26
Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?
Mathayo 16:27
Kwa sababu Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake; ndipo atakapomlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.