Hebu tupe history ya bongo hip hop
Kumbe ndo maana uko na uwezo Wa kupambanua mambo due to old skull hip hop +vitabu(literacy)
Wakati huo tunarekodi ama Mawingu Mwenge, ama Don Bosco Upanga ama Temeke Soundcrafters.
Halafu hapo ITV na Radio One ndiyo zinaanzishwa, tunaongea nao wanarekodi music video.
Videos kama za "Oya Msela" Mawingu Band/ O Juice, "Usiige Mambo ya Mjini" wa Hard Blasterz, "Pilika Pilika" wa Sossy B na "Cheza Mbali na Kasheshe" wa GWM zilikubalika sana.
Halafu tulifanya sana parties, mara nyingi za Beach, hususan Oysterbay. Beach ilikuwa inafunga watoto wa pande zote za Dar tunakutana, tunachanganyika, one love.
Baada ya hapo yakawa mashindano kama ya Kim Mgomelo "Yo Rap Bonanza" na ya Don Bosco Youth Festival. Vikundi vilikuwa vinajiandaa mwaka mzima kwa mashindano haya.
I was there when Mr 2 came to Dar from Mbeya, and Dar Young Mob took him in.
I was there with him at Don Bosco Studios, when he was recording one of his early albums.
Concerts za Korean Cultural Centre, Empire Cinema, ma beach parties zilifana sana. Lakini watu wengi walichukulia muziki kama sehemu ya kufurahia maisha tu, ulikuwa haujawa biashara bado.
Mtu aliyekuja kuanza kufanya kweli kwenye biashara alikuwa Mr. 2. Alideal na wahindi wa Dar, wakamtengenezea kaseti na kuziuza nchi nzima, baada ya yeye kupewa chajuu. Lakini alidhulumiwa sana kwa sababu alikuwa hana control baada ya kuwapa masters zake wahindi.
Mr. 2 alianza kupata mafanikio ya kibiashara, ingawa alikuwa si mtoto wa Dar, na alivyokuja alikuwa anafanya kazi kwenye petrol station kabla hajawa maarufu.
Kuna watoto wa Dar waliokuwa wameanza kufanya Hip Hop (enzi hiyo jina Bongofleva halikuwepo) kabla ya Mr. 2 wakina Kwanza Unit, Hard Blasterz, Dar Young Mob (ambao Mr. 2 alijiunga nao) na hata kabla zaidi, Saleh Jabri alijirekodi kwenye instrumental ya Vanilla Ice "Ice Ice Baby".
Kitu kingine kikubwa kilikuwa kupeleka Chrome tapes Radio One, zipigwe redioni. Taji Liundi alikuwa Radio DJ aliyepokea tapes za wasanii wengi sana na kupiga nyimbo zao redioni.
Siku hizo Taji akikuchagua na kupiga nyimbo zako katika kipindi cbake cha DJ Show, unakuwa maarufu sana, kwa sababu kipindi kinasikilizwa na watu wengi sana.
Baadaye kipindi hiki kikaja kuendeshwa na Mike Muhagama, ambaye nafikiri ndiye aliyeanza kutumia neno "Bongo Fleva"