Dizasta vina - Hatia V

Dizasta vina - Hatia V

Kama haiwashiki basi hawahusiki na haitowasaidia~ (One -Kivyovyote)

Point yangu ni kwamba, kama mtu ni mdau wa hip hop hawezi kupitwa na ngoma yoyote ya huyu jamaa. Ukiona mtu anasubiri hit song basi huyo ni "Shabiki rukia rukia"/ "Shabiki waru waru".
Sure..
 
namsikiaga sikiaga hususani ngoma yake ya mwanajua kupitia kwa bro wangu mmoja hivi,mpenda hiphop kiukweli jamaa anajua yaani inahitajika akili kubwa sana kumwelewa
 
Scars unakwama sana kijana wangu. Yani mpaka comment ya 20, bado hujafika na uzi unamuhusu Disaster?

Hebu leta lyrics hizo!
Mkuu huu uzi sikuuona kabisa nashukuru kwa tag

Japo siku hizi nimekuwa mvivu sana kuchangia uzi wenye maudhui ya Hip Hop kutokana na kukatishwa tamaa na members wengi wanaoonekana kutoujua huu mziki

Post za juu kuna mdau nimeona kasema Dizasta sio mkali kwasababu hana hitsong

Kumbuka hii platfom ndio kuna ile title ya home of great thinkers
 
Kama haiwashiki basi hawahusiki na haitowasaidia~ (One -Kivyovyote)

Point yangu ni kwamba, kama mtu ni mdau wa hip hop hawezi kupitwa na ngoma yoyote ya huyu jamaa. Ukiona mtu anasubiri hit song basi huyo ni "Shabiki rukia rukia"/ "Shabiki waru waru".
Nazani unajua kusoma tatizo ni kuelewa
 
Mkuu huu uzi sikuuona kabisa nashukuru kwa tag

Japo siku hizi nimekuwa mvivu sana kuchangia uzi wenye maudhui ya Hip Hop kutokana na kukatishwa tamaa na members wengi wanaoonekana kutoujua huu mziki

Post za juu kuna mdau nimeona kasema Dizasta sio mkali kwasababu hana hitsong

Kumbuka hii platfom ndio kuna ile title ya home of great thinkers
Kwenye kila jamii, lazima kuna chizi mmoja. Hatuwezi kua na uelewa sawa. Wala hatuwezi wote kupenda kitu kimoja.

Puuza hizo mburula, alafu tufanye kile kitu roho inapenda. Hebu tuletee punch za hatia V.

Moja ya sababu ya kuipenda hip hop, ni kwa sababu sio kila mtu anaelewa kinachoimbwa. Inahitaji upeo wa kutosha. Ndio maana mimi sishangai kukutana na mtu au watu wanaoiponda hii tasnia!
 
Kwa wapenzi wa hiphop hivi mmepata na nafasi ya kusikiliza hii nyimbo mpya dizasta vina hatia V aisee kuna ubunifu mkubwa umetumika sana humo hata akifa leo nyimbo zake zitasikilzwa milele jamaa anajua sana. Vipi maoni yako mwana #JF #DIZASTAVINA #HATIA View attachment 2459885
Dizasta vina ndiyo nani?
Ngoja nitafute vibao vyake nisikilize labda nitakuelewa
 
Binafsi sijaona Kama dizasta n msanii mkali wa hip-hop Kama inavojaribu kutajwa humu.
Kwani Hana hit song ambayo imetoboa nje ya jamii ya wapenda hip-hop yaani kwa wale wasiokua mashabiki Lia Lia wa hip-hop...
Ngoma ambayo ilifanya vizuri kwenye platform mbalmbali Ni kanisa tu. Hizo zingine bado ziliishia kwetu tu wapenda hip-hop nazani Ni Muda Sasa ajitafute afanye muziki unaopenya kila angle...
Angalie kina Nikki mbishi, young killer, nash-mc, one hata stereo waliwezaje...
Huwezi kuelewa kama ww n bongo lala
 
Mbio nyingi sana YouTube kuskia kitu kipya cha Professor Tungo, maana huyu jamaa waga haandiki nyimbo bali waga anaandika Movie

"Alifanya Mema zaidi ya kumi, haikutosha awe Yesu, ila baya Moja aliitwa Shetani"

Huyu Mwamba hii miaka miwili kaitendea haki sana, kuanzia kwenye The verteller, tukaja kwenye SHAIDI na sasa Hatia V

Itoshe tu kusema huyu ndio msanii Bora wa hip-hop kwa miaka hii miwili, kama Fid kakubali, Professor Jay amekili me ni Nani?

NB: nimesema msanii bora wa hip-hop kwa kuzingatia content zake na sio msanii wa hip-hop mwenye hits nyingi wala stream nyingi
 
Dizasta ni genius, ni Messi wa Rap.

Hatia V ni Masterpiece,
lakini kwa mtazamo wangu katika mfululizo wa hizi Hatia (Hatia 1-5), hatia 4 itabaki kuwa kali zaidi.
 
Binafsi sijaona Kama dizasta n msanii mkali wa hip-hop Kama inavojaribu kutajwa humu.
Kwani Hana hit song ambayo imetoboa nje ya jamii ya wapenda hip-hop yaani kwa wale wasiokua mashabiki Lia Lia wa hip-hop...
Ngoma ambayo ilifanya vizuri kwenye platform mbalmbali Ni kanisa tu. Hizo zingine bado ziliishia kwetu tu wapenda hip-hop nazani Ni Muda Sasa ajitafute afanye muziki unaopenya kila angle...
Angalie kina Nikki mbishi, young killer, nash-mc, one hata stereo waliwezaje...

'Kwani hana hit song ambayo imetoboa nje ya jamii ya wapenda hip hop'
Unaelewa unachoongea we jamaa!? Jamii gani ya hip hop unayoongelea tofauti na hii iliyopo hapa maana ndio hiyo hiyo iliyopo huko mtaani.
Kumbe kuna mashabiki lia lia wa hip hop na wapenda hip hop!!! Naomba kujua tofauti yao tafadhal mana nachojua hip hop heads hatuangalii hit song tunaangalia contents na flows.
 
Hebu Soma ulichoandika jibu lipo humo humo
 
Dizasta ni genius, ni Messi wa Rap.

Hatia V ni Masterpiece,
lakini kwa mtazamo wangu katika mfululizo wa hizi Hatia (Hatia 1-5), hatia 4 itabaki kuwa kali zaidi.
Hata mimi hatia iv naona ni habari nyingine, ila hii hatia v ni kali sana na yenyewe sema kaweka chakula cha ubongo zaidi
 
Back
Top Bottom