Khantwe
JF-Expert Member
- Dec 20, 2012
- 59,415
- 119,473
A. Nusu ya pesa hizo ilipitishwa kwenye bajeti ya serikali. Hata hivyo wakati bajeti ishapita JK akasema anaongeza kiasi kingine kama hicho kwani ameona mahitaji ni makubwa. Wengine wakauliza hiyo nyongeza itatoka bajeti ipi? Mpaka leo kimya. Labda ndiyo hiyo ya Boston!
B. Mtu yeyote anastahili ili mradi atimize yatakayokubaliwa benki. Walengwa ni wajasiriamali wadogo wadogo. Inaweza ikawa kikundi (SACCOS) pia, ambayo nayo itaenda kukopesha wanachama wake. CRDB imejikita kukopesha SACCOS, wakati NMB inalenga watu binafsi.
C. Mchanganuo wako ndiyo utahalalisha kupata pesa hizo. Inatarajiwa kuwa mkopo huo ni wa kuendeleza biashara/mradi badala ya kuwa start up capital.
D. Mchanganuo unapaswa uoneshe mafanikio yatakavyopimwa. Benki pia ndiyo wajuzi na wana vigezo vya kupima mafanikio.
E. Huo ni mkopo unaopaswa urudishwe ili wengine wakope pia (revolving fund)
ANGALIZO: Kugongana? JK kaanza kumshtukia EL kuwa anataka kumtumbukiza?
Unaweza kumhoji Chiligati ukipenda.
Inakuhusu?