Dj Majizo, Muasisi wa muziki wa Mchiriku, Mnanda, Singeli redioni!

Dj Majizo, Muasisi wa muziki wa Mchiriku, Mnanda, Singeli redioni!

Ila jichanganye siku uingie kwenye show ya singeli, utajuta kuzaliwa, napenda sana kusikiliza nyimbo zao na nilizipenda bila kupenda, huu mziko ni reflection ya maisha ya watoto wa maskani, wahuni na walioshindikana
 
...teh teh teh...mbagala umeme unakatika kuliko Snura!
(watu wanavuta bangi,moshi kwenye makalio!!)
 
Tune EFM kuanzia saa 2 hadi saa 5 usiku usikilize Genge..Na Kicheko..Ni Singeli kwa kwenda mbele na Kali za Kitambo..

Pia Sports HQ ya asubuhi ni Singeli kwa kwenda mbele

Muziki unaongea...
Naomba frequency mkuu
 
Washkaji karibuniii
Karibuni maskaniii
Na wala msione kimyaa
Saidi darban hamumuoni
Said darban amefariki
Kwa ajali ya gariii
Ambayo imetokea
Buguruniii
Said darban kaacha majonzi
Hata Kwa mzazi mwenzie
Pili mama Ali anabaki analia
Oooooooh
Ndio wimbo huu ua nimechanganya?
Daa nautafuta huu wimbo!
 
Naona kama kawaida wachawi hawakosekani kwenye hii mada, nawaita wenye wivu wa transgender (wivu mbaya sana huu).
Kibaya zaidi ni wanawake.
Kamsalimie rais wetu.
Nashangaa sijui kwanini watu wanachukia tukimsiifu Majizzo?
 
Nashangaa sijui kwanini watu wanachukia tukimsiifu Majizzo?
ndio tabia ya watu fulani fulani hapa JF, wana tabia ya kichawi sana, hawataki mtu asifiwe kwa mazuri yake.
Mtoa mada ameeleza ukweli na unaonekana kwa kila mwenye macho na kusikika kwa kila mwenye masikio, lakini mtu anakuja anatoa povu tuu! Dah!
 
Nakataa hadi Mwisho,Majizo hawezi kumiliki E-FM labda yeye ni GALASA wamiliki wapo nyuma,Kwa majizo alivyo hata fedha ya kupanga tu pale K-NET house hawezi lipa.
Mtoa mada aliongelea mada au ubunifu? Punguza wivu, ona na dada yako anavyosema hapa chini

Siongelei umiliki. Naongelea ubunifu. Huyo Majizzo mwenyewe radio hiyo siyo yake
wivu wa namna hii ni mbaya sana Jane, jirekebishe ungali kijana
Huyu kutwa kukimbizana na kina Lulu Insta halafu huo ubunifu atautoa wapi? It's only a matter of time before we see his radio station go down the drains. Huwezi ukaendesha biashara ya radio kwa uswahiliswahili. You got to have the needed talent.
Kwa hiyo hapa tatizo sio ubunifu, ni kwa vile tu Majizo kamega kwa Lulu na sio kwako, ila umezunguka tu!
 
View attachment 353220View attachment 353221View attachment 353222


Wasalaam wana jamvi!

Ni ukweli usio pingika kuna muziki fulani uliokuwa umezoeleka ndio unatakiwa kupigwa radioni na hii ilikuwa ni uniform za Radio zote kana kwamba ilikuwa ni sheria ambayo imewekwa!

ilikuwa ni vigumu na hakuna uthubutu wa miziki ya mnanda ,visingeli na mchiriku kusikia ukipigwa radioni na sio kwamba hauna mashabiki bali una mashabiki wengi sana sema radio muda mwingine hulazimisha walaji kula hata wasicho kitaka!

Dj Majizzo baada ya kuanzisha kutuo cha E-FM imekuwa kama mkombozi wa miziki yetu ya asili na wamekuwa wakiupa muda wa kutosha kuupromote kiasi kwamba hata walio kuwa hawajui uzuri wake sasa wanaelewa!

Mimi sikuwa mshabiki wa miziki wa namna hii lakini sasa nimekuwa kama teja maana kwakweli nyimbo hizi kuna zenye jumbe nzuri sana kiasi kwamba ukisikiliza una hamasika hakika!

Kupitia DJ majizzo (E-FM) leo hii sasa nyimbo za mnanda,mchiriku na singeli zimeanza kusikika kwenye radio nyingine na wasanii hao wanapata showa kitu ambacho hakikutegemewa!

Leo hii ukisikiliza East africa radio utasikia wakipiga nyimbo hizi na hata Clouds na kwenye matamasha tunaona wasanii wa minanda,mchiriku na visingeli wanapewa show tofauti za zamani wale wa bongo fleva ndio walikuwa wanakula hela peke yao!

Ni wazi kabisa Wasanii wa minanda ,mchiriku na visingeli wanapaswa kumshukuru Majizzo kwani amechangia sana kwenye mafanikio yao na mapinduzi yao!

Mimi nimshukuru tuu Majizzo kwa kuwasaidia vijana hawa na kuupa thamani mziki wao!

Karibuni Wana jamvi!
[emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122]
 
Mashabiki wengi wa singeli ni wahuni wa mtaani wavuta bangi na wabwia unga.
Majizzo naona kaamua kuwapa shavu "wateja wake" as per mange's dot dot.....
You are one arrogant and uncultured swine.
 
Back
Top Bottom