Chiwaso
JF-Expert Member
- Oct 21, 2009
- 5,726
- 3,778
Umesahau jina moja ................MNANDA....................Kwa wapenzi wa lugha ya Kiswahili, kama nilivyo mimi wenu mtiifu, hizo aina za muziki ni njia nzuri sana za kujifunzia hii lugha yetu.
Ndiyo maana mimi, tena kwa fahari kubwa sana, huwa najivunia upenzi wangu wa aina hiyo ya muziki zikiwemo Taarab asilia, Taarab ya kileo, pamoja na chakacha.
Nimejifunza mengi mno yahusuyo lugha ya Kiswahili na lahaja zake kupitia hizo aina za muziki.