Ujue ishu hii mimi baadaye nilikuja kugundua kwamba kuna namna ambayo Debora alikuwa akitengeneza mazingira ya kutafuta pesa kwani sheria ya Sweden siku zote ukilala na mwanamke bila ridhaa yake akishitaki unatuhumiwa kuwa umebaka na yeye analipwa kama dola elfu kumi na mbili (zaidi ya Sh. milioni 24 za Kitanzania)".
“Hata kama ni mkeo, ukifanya naye tendo la ndoa bila yeye kuridhia na akashitaki, basi wewe utakuwa umebaka na sheria inakufunga huku yeye akilipwa kiasi hicho cha fedha".
“Kilichotokea kwa Rommy Jones ni dhahiri kabisa kuwa Debora alitaka kujipatia pesa kwa njia hiyo kwani baada ya kuanza kung’aka kuwa amebakwa, mimi nilimtafuta na kumuomba msamaha maana Rommy Jones hakujua kama sheria ya huko iko hivyo na isitoshe wote walikuwa wamelewa.
“Pamoja na msamaha, Debora aliendelea kuomba afidiwe dola elfu kumi na mbili, mimi nikamwambia nimpatie dola elfu sita lakini aligoma na kutaka hiyo hivyo tukashindwa kuafikiana."