Dk. Kijo bisimba ageuka kuwa msemaji wa ukawa!!!

Dk. Kijo bisimba ageuka kuwa msemaji wa ukawa!!!

Mwakaboko King

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2015
Posts
1,099
Reaction score
207
image.jpg

Kati ya mambo ambayo yananishangaza ni baadhi ya viongozi wa Asasi na Taasisi za Kiraia kusahau majukumu yao na kuanza kuwa wasemaji wa vyama vya Siasa, hili la Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC kugeuka mtoa matamko ya UKAWA kwa kujipa majukumu yasiyo yake kutoa matamko ya kuikataza Serikali kutokujihusisha na shughuli ya upatikanaji wa Katiba mpya halipaswi kuungwa mkono.

Kiongozi huyu ameigeuza taasisi hiyo jukwaa la Siasa na kusahau kabisa kuwa taasisi anayoiongoza pamoja na mambo mengine haitakiwi kufanya siasa la sivyo aende kwa msajili akakisajili kuwa chama kipya. Kwa namna yoyote ile huwezi kuitenga Serikali katika kutimiza wajibu wake katika hili ili hatimaye Tanzania tupate Katiba mpya!Mchakato huu hauwezi kusimama peke yake bila Serikali kuhusika hilo alijue na si kama anavyofikiri yeye. Na kama basi anataka kuwatumikia wananchi kwenye masuala ya siasa ajiunge na Chama kimojawapo cha siasa tujue moja ili aache kufanya Siasa ndani ya LHRC!

Mungu Ibariki Tanzania!
 
Kwa taarifa yako, hakuna mtetezi yoyote wa haki za binadamu au mwanaharakati, anayeweza kuwa upande wa wanyonyaji hata siku moja, tena serikali yenyewe hiii?!!! mtawapata hao wakina mpanju tu, ambao wanaishi kwa kujipendekeza kwa watawala, timu nzima ya LHRC, JUKWAA LA KATIBA, kazi wanayofanya ni nzuri sana, najua kinachowauma ni hii elimu juu ya katiba pendekezwa kwani wanamwaga nondo huko kijijini c mchezo.
 
He! Dkt.kijo bisimba si yuko kituo cha sheria na haki za binadamu? Au nimekosea?sasa anauhusiano gani na ukawa,amehamia huko? Nisaidieni jama sijaelewa kama huyu dkt amekuwa msemaji wa ukawa?
 
Kwa taarifa yako, hakuna mtetezi yoyote wa haki za binadamu au mwanaharakati, anayeweza kuwa upande wa wanyonyaji hata siku moja, tena serikali yenyewe hiii?!!! mtawapata hao wakina mpanju tu, ambao wanaishi kwa kujipendekeza kwa watawala, timu nzima ya LHRC, JUKWAA LA KATIBA, kazi wanayofanya ni nzuri sana, najua kinachowauma ni hii elimu juu ya katiba pendekezwa kwani wanamwaga nondo huko kijijini c mchezo.

Nachojua mimi LHRC ni taasisi isiyoendeshwa kwa lengo la kupata faida wala isiyojihusisha na siasa hata ukitembelea tovuti yao utaona wameweka wazi sasa huyu mama kujiingiza kwenye siasa anaifedhehesha taasisi anayoiongoza!nimemsikia leo asubuhi redioni anaponda Serikali huyo!!
 
Katiba pendekezwa imepatikana kimezengwe kwa kutupa maoni ya wananchi....haki ya mwananchi inaanza kuonekana kwenye katiba na imeonekana kuporwa kwa kiwango cha juu kabisa....Kisimba kama mtetezi wa haki za Raia unataka afanye nini zaidi ya kukemea kupitia legal forums?
 
Huyu na yule mwenzake anayeitwa Ananilea Nkya ni makada watiifu wa CHADEMA.
 
Nachojua mimi LHRC ni taasisi isiyoendeshwa kwa lengo la kupata faida wala isiyojihusisha na siasa hata ukitembelea tovuti yao utaona wameweka wazi sasa huyu mama kujiingiza kwenye siasa anaifedhehesha taasisi anayoiongoza!nimemsikia leo asubuhi redioni anaponda Serikali huyo!!

kwa hiyo kuwasemea wanyonge, nayo ni siasa, ingekuwa ni taasisi inayojishughulisha na labda TEZI DUME/MARALIA, hapo ungekuwa sahihi, lakini ya haki za binadamu?? unashangaa kuwa against na serikali? kipindi kile sakata la ulimboko hawakuwa mbele? hadi serikali ikawachukia? uhuni uliofanyika kwenye rasimu ya warioba wakae kimya? wakati maoni ya wanainchi yametupwa huko! we vipi bwana umekula maharage ya wapi? juzi huko njombe kwenye BVR, kuna baadhi ya watetezi wa haki za binadamu walivamiwa na kupigwa, kisa wanajifanya viherehere!! narudia kusema kamwe mtetea haki za binadamu wa ukweli duniani kote hawezi kuwa upande wa mnyonyaji, hususani kwa Afrika! mfano hai angalia kinachoendelea huko BURUNDI, juzi kuna mtetezi wa haki za binadamu, alikamatwa kuwa ndio anayechochea maandamano!! huyu naye anaitwa mpinzani!! nyie kaeni na huyo mpanju wenu ambaye anatumia ulemavu wake kujinufaisha na kuwasahau wenzake, wanao mtegemea, safi sana majembe ya LHRT, Kwani kazi mliyoifanya juzi shy, juu ya elimu ya katiba pendekezwa,si mchezo!! wao wanadhani eti vifungu vya katiba ni ku vi display kwenye TBC, tu, imetoka!! watu wanafafanua hadi kiziwi anaelewa!! huko field unafanya mchezo!!
 
Mwakaboko King ww ni muongo mkubwa, ni wapi huyo mama Kijo ametaja chama? Acha upimbi jamani, katiba inayopendekezwa haifai hata kidogo, ni mbayaaaaa
 
Last edited by a moderator:
Huyu mama fyatu kweli sijui ukawa wanamlipa kiasi gani kuwa mseamji wao.
 
Kati ya mambo ambayo yananishangaza ni baadhi ya viongozi wa Asasi na Taasisi za Kiraia kusahau majukumu yao na kuanza kuwa wasemaji wa vyama vya Siasa, hili la Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC kugeuka mtoa matamko ya UKAWA kwa kujipa majukumu yasiyo yake kutoa matamko ya kuikataza Serikali kutokujihusisha na shughuli ya upatikanaji wa Katiba mpya halipaswi kuungwa mkono.

Kiongozi huyu ameigeuza taasisi hiyo jukwaa la Siasa na kusahau kabisa kuwa taasisi anayoiongoza pamoja na mambo mengine haitakiwi kufanya siasa la sivyo aende kwa msajili akakisajili kuwa chama kipya. Kwa namna yoyote ile huwezi kuitenga Serikali katika kutimiza wajibu wake katika hili ili hatimaye Tanzania tupate Katiba mpya!Mchakato huu hauwezi kusimama peke yake bila Serikali kuhusika hilo alijue na si kama anavyofikiri yeye. Na kama basi anataka kuwatumikia wananchi kwenye masuala ya siasa ajiunge na Chama kimojawapo cha siasa tujue moja ili aache kufanya Siasa ndani ya LHRC!

Mungu Ibariki Tanzania!

Ndugu si kila mtu amesikia alichokisema huyo mama, hivyo hatuwezi kukurupuka kumlaumu kwamba alichokifanya sio sahihi bila kujua tamko lake likoje. Hebu tuwekee hilo tamko hapa na sisi tujiridhishe kwamba huyo amekosea la sivyo utakuwa unaimba wimbo ule ule wa kufikiri siasa inapashwa izungumzwe na Nape na Kinana tu.

Tiba
 
kumbe siku hizi ukisema ukweli na kusimamia misimamo yako vizuri yenye masirahi kwa wananchi tayari watawala wanakubambika kuwa msemaji wa UKAWA nilikuwa silijui hilo nashukuru kwa kunijulisha
 
Nchi inasambaratika katika elimu, afya, ajali, nk, nk ..karibu kila kitu naq hakuna anayejitokeza kusema na kuutahadharisha umma. Sasa kama yeye anaamini katika kitu fulani ni kwa nini asikiseme!?

Nchi inasambaratika wapi?afu wewe unaishi wapi usijifariji jenga hoja la mtu mwenye dhamana ya taasisi ambayo kwenye msimamo wake imewekwa wazi kabisa kuwa mbali na siasa anapogeuka kiongozi wa siasa achukue kadi tu tujue moja kazi yake ni kupinga kila kitu.
 
Ndugu si kila mtu amesikia alichokisema huyo mama, hivyo hatuwezi kukurupuka kumlaumu kwamba alichokifanya sio sahihi bila kujua tamko lake likoje. Hebu tuwekee hilo tamko hapa na sisi tujiridhishe kwamba huyo amekosea la sivyo utakuwa unaimba wimbo ule ule wa kufikiri siasa inapashwa izungumzwe na Nape na Kinana tu.

Tiba

We TOMASO Tu ndo uwe makini kufuatilia taarifa za nchi yako kama kakutuma mwakbie watanzania tumesikia!
 
Si Wa Kule Kule MILIMANI She! Yeye Na TAMWA Zamani ANANILEA NKYA, Na TGNP USSU MALLYA Na SIKIKA IRENEI KIRIA, Mwenye Macho Huambiwi Tizama Na Ile TV "YETU"
So Usishangae ANKAL😀😀😀
 
kumbe siku hizi ukisema ukweli na kusimamia misimamo yako vizuri yenye masirahi kwa wananchi tayari watawala wanakubambika kuwa msemaji wa UKAWA nilikuwa silijui hilo nashukuru kwa kunijulisha[/QUOTE

NDIYO KWANI HUJUI KUWA KAZI YAO NI KUPINGA KILA KITU NA SASA WANAPINGANA WAO KWA WAO NDO UTAJUA SASA KATI YA YAI NA KUKU KIPI KILIANZA, HUYO NI KADA MTIIFU WA UKAWA BADO KIDOGO ANAIGEUZA TAASISI YAKE AMBAYO AMESEMA HAIFUNGAMANI NA SIASA KUWA CHAMA CHA SIASA AND FROM NON PROFIT ORGANISATION KUWA SACCOS!
 
Back
Top Bottom