Mwakaboko King
JF-Expert Member
- Apr 22, 2015
- 1,099
- 207
Kati ya mambo ambayo yananishangaza ni baadhi ya viongozi wa Asasi na Taasisi za Kiraia kusahau majukumu yao na kuanza kuwa wasemaji wa vyama vya Siasa, hili la Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC kugeuka mtoa matamko ya UKAWA kwa kujipa majukumu yasiyo yake kutoa matamko ya kuikataza Serikali kutokujihusisha na shughuli ya upatikanaji wa Katiba mpya halipaswi kuungwa mkono.
Kiongozi huyu ameigeuza taasisi hiyo jukwaa la Siasa na kusahau kabisa kuwa taasisi anayoiongoza pamoja na mambo mengine haitakiwi kufanya siasa la sivyo aende kwa msajili akakisajili kuwa chama kipya. Kwa namna yoyote ile huwezi kuitenga Serikali katika kutimiza wajibu wake katika hili ili hatimaye Tanzania tupate Katiba mpya!Mchakato huu hauwezi kusimama peke yake bila Serikali kuhusika hilo alijue na si kama anavyofikiri yeye. Na kama basi anataka kuwatumikia wananchi kwenye masuala ya siasa ajiunge na Chama kimojawapo cha siasa tujue moja ili aache kufanya Siasa ndani ya LHRC!
Mungu Ibariki Tanzania!
