Dk Muchunguzi: Mwaka 2020 Polepole alisimamia mgombea mmoja CCM, waliotaka kugombea walifukuzwa

Elias Msuya

Platinum Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
267
Reaction score
1,014
Mchambuzi wa masuala ya siasa, Dk Dennis Muchunguzi amekosoa kauli za aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole kuhusu uteuzi wa Rais Samia kuwa mgombea pekee aliyepitishwa na mkutano mkuu wa CCM, Januari 19, akisema ni utaratibu wa CCM kwa rais anayegombea awamu ya pili kuwa mgombea pekee.
Amesema hata Rais Magufuli alipogombea kwa mara ya pili, alikuwa mgombea pekee na waliojaribu kuchukua fomu walifukuzwa.

View attachment 3413050

Polepole alikosoa uteuzi huo katika barua yake ya kujiuzulu zliyotoa Julai 13 na baadaye kwenye mkutano na waandishi wa habari wa Julai 18 uliofanyika mtandaoni.
Polepole: Mchakato wa CCM kumpitisha Samia kuwa Mgombea Urais 2025 haukuwa halali

Aidha, Dk Mchunguzi amesema mkutano mkuu wa Januari 18, 19, 2025 ulikuwa halali.

View attachment 3413049
 
CCM itasambaratika muda mfupi ujao,kama hawataheshimu katiba yao na kutumia utashi wao kuongoza Gen Z
 
Mchambuzi wa masuala ya siasa, Dk Dennis Muchunguzi amekosoa kauli za aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole kuhusu uteuzi wa Rais Samia kuwa mgombea pekee aliyepitishwa na mkutano mkuu wa CCM, Januari 19, akisema ni utaratibu wa CCM kwa rais anayegombea awamu ya pili kuwa mgombea pekee.
Amesema hata Rais Magufuli alipogombea kwa mara ya pili, alikuwa mgombea pekee na waliojaribu kuchukua fomu walifukuzwa.

View attachment 3413050

Polepole alikosoa uteuzi huo katika barua yake ya kujiuzulu zliyotoa Julai 13 na baadaye kwenye mkutano na waandishi wa habari wa Julai 18 uliofanyika mtandaoni.
Polepole: Mchakato wa CCM kumpitisha Samia kuwa Mgombea Urais 2025 haukuwa halali

Aidha, Dk Mchunguzi amesema mkutano mkuu wa Januari 18, 19, 2025 ulikuwa halali.

View attachment 3413049
Huyu ni mchunguzichawa!

Traditionally, Rais wa kuchaguliwa akitaka kugombea kwa mara ya pili huwa hapitii tena ile mikiki mikiki kama ile aliyoipitia wakati anagombea term yake ya kwanza. Kila Rais aliyepita alipatikana kwa kushindanishwa na wanachama wenzake (kabla ya kuchaguliwa kwa mara ya kwanza).

Samia The Killer amewahi kushindanishwa na nani?
 
Kama alifanya hivyo alikosea sana.

Na kama kaona leo hayo makosa yana athari hasi kwa taifa na kaamua kutoka hadharani kukemea nadhani huyu mtu tumsamehe ya nyuma sasa tupime hoja yale ya leo kama ina afya kwa taifa bila kujali alifanya nini miaka kadhaa nyuma.

Tunaamini kuwa Bwana kama wewe ungehesabu maovu yetu nani angesimama mbele yako.

Kwakuwa wote ni wadhambi nadhani toba ya Polepole imekuja wakati mwafaka na huenda imemfanya asamehewe madhambi yake yote ya nyuma bila kujali yalikuwa na ukubwa gani.
 
hapo ndipo madokta wetu wanafeli kwamba asiseme Leo kwa kuwa Jana hakusema daktari muchunguzi unaona sawa hiyo?.
 
Huyu ni mchunguzichawa!

Traditionally, Rais wa kuchaguliwa akitaka kugombea kwa mara ya pili huwa hapitii tena ile mikiki mikiki kama ile aliyoipitia wakati anagombea term yake ya kwanza. Kila Rais aliyepita alipatikana kwa kushindanishwa na wanachama wenzake (kabla ya kuchaguliwa kwa mara ya kwanza).

Samia The Killer amewahi kushindanishwa na nani?
Kikatiba Samia hii ni awamu yake ya pili. alianza kuwa Urais 2021 Kikatiba. Msindania wake 2021 alikuwa Katiba. Hivyo, awamu hii kwa utamaduni wa CCM hatakiwi kupitia mikikimikiki maana anaenda kukamilisha muhula wake wa pili.
 
Mchambuzi wa masuala ya siasa, Dk Dennis Muchunguzi amekosoa kauli za aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole kuhusu uteuzi wa Rais Samia kuwa mgombea pekee aliyepitishwa na mkutano mkuu wa CCM, Januari 19, akisema ni utaratibu wa CCM kwa rais anayegombea awamu ya pili kuwa mgombea pekee.
Amesema hata Rais Magufuli alipogombea kwa mara ya pili, alikuwa mgombea pekee na waliojaribu kuchukua fomu walifukuzwa.

View attachment 3413050

Polepole alikosoa uteuzi huo katika barua yake ya kujiuzulu zliyotoa Julai 13 na baadaye kwenye mkutano na waandishi wa habari wa Julai 18 uliofanyika mtandaoni.
Polepole: Mchakato wa CCM kumpitisha Samia kuwa Mgombea Urais 2025 haukuwa halali

Aidha, Dk Mchunguzi amesema mkutano mkuu wa Januari 18, 19, 2025 ulikuwa halali.

View attachment 3413049
1753353501793.png
 
Back
Top Bottom