GE2025 Dk. Nchimbi: CCM tutaongeza upatikanaji wa ruzuku ya mbolea vijijini

GE2025 Dk. Nchimbi: CCM tutaongeza upatikanaji wa ruzuku ya mbolea vijijini

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeahidi kuongeza ruzuku ya mbolea kwa wakulima, ikiwa ni mkakati wa kuongeza tija ya kilimo, kuinua kipato cha wananchi na kuboresha maisha ya wakulima hususan wa maeneo ya vijijini mkoani Iringa.

Mgombea Mwenza wa Urais wa chama hicho, Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, ametoa ahadi hiyo katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika Viwanja vya Nanenane, Jimbo la Isimani, wilayani Iringa Vijijini.

Dk. Nchimbi amesema mpango huo ni sehemu ya mkakati mpana wa serikali ya CCM wa kuchochea maendeleo ya uchumi wa ndani na kupanua upatikanaji wa huduma muhimu za kijamii.

"Tunataka kuona wakulima wa Iringa Vijijini na Tanzania kwa ujumla wakilima kwa tija zaidi. Kupitia ruzuku ya mbolea, mavuno yataongezeka na kipato cha wananchi kitaimarika, hivyo kuleta maendeleo ya kweli katika familia na jamii," amesema.

Akitaja mafanikio yaliyopatikana tayari katika wilaya hiyo, Dk. Nchimbi amesema miradi mikubwa ya maendeleo imeanza kubadili maisha ya wananchi, ikiwemo ujenzi wa vituo vipya vya afya saba, shule za sekondari nane na vyumba vya madarasa 390, vyote vikiwa na lengo la kuimarisha mifumo ya elimu na afya.

Aidha, amesema Hospitali ya Wilaya ya Iringa imepandishwa hadhi ili kutoa huduma bora zaidi, hatua inayolenga kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya zenye ubora na za uhakika.

Akizungumzia mipango ya miaka mitano ijayo, Dk. Nchimbi ameahidi kuchimbwa kwa visima vipya vitano vya maji katika Jimbo la Isimani, ili kupunguza changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi wa vijijini.

"Serikali ya CCM itaendelea kutekeleza miradi ya maji, elimu, afya na kilimo ili kuhakikisha kila mwananchi wa Iringa Vijijini anapata fursa sawa ya maendeleo," ameongeza.

Chanzo: Nipashe
 
CCM ndio wapo madarakani, ni kipi kiliwashinda kutekeleza hayo!
 
Back
Top Bottom