n00b
JF-Expert Member
- Apr 10, 2008
- 1,015
- 2,680
Umati Mkubwa ulijitokeza kumlaki Dk. Slaa katika eneo la Haydom, jimboni Mbulu
Dk Slaa anamtambulisha mgombea ubunge wa Hanang, Rose Kamili, katika eneo la Endosak, jirani na nyumbani kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye.
Ilikuwaje?
Kwanza, walijaa katika mikutano yake katika majimbo ya Hanang na Mbulu.
Pili, walizuia misafara yake kokote alikopita wakitaka awahutubie, walau kwa dakika moja tu!
Tatu, walimwahidi kufanya mabadiliko makubwa mwaka huu kwa kuchagua wabunge na madiwani wa Chadema, ili kukifanya CCM kuwa chama cha upinzani.
Kipya ni kwamba alitumia usafiri wa Kipanya (Hiace) badala ya helikopta kutoka Babati hadi Mbulu, kwa sababu helikopta ilipata hitilafu kidogo Jumatano mara baada ya kutua mjini Babati ikitokea eneo la Bashnet.
Habari na Picha na Mdau Asbert Ngurumo