Elections 2010 Dk Slaa Afunika Hanang', Mbulu na Haydom

Elections 2010 Dk Slaa Afunika Hanang', Mbulu na Haydom

n00b

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2008
Posts
1,015
Reaction score
2,680
25ssmcg.jpg


Umati Mkubwa ulijitokeza kumlaki Dk. Slaa katika eneo la Haydom, jimboni Mbulu

34pjkaw.jpg

Dk Slaa anamtambulisha mgombea ubunge wa Hanang, Rose Kamili, katika eneo la Endosak, jirani na nyumbani kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye.

Ilikuwaje?

Kwanza, walijaa katika mikutano yake katika majimbo ya Hanang na Mbulu.

Pili, walizuia misafara yake kokote alikopita wakitaka awahutubie, walau kwa dakika moja tu!

Tatu, walimwahidi kufanya mabadiliko makubwa mwaka huu kwa kuchagua wabunge na madiwani wa Chadema, ili kukifanya CCM kuwa chama cha upinzani.

Kipya ni kwamba alitumia usafiri wa Kipanya (Hiace) badala ya helikopta kutoka Babati hadi Mbulu, kwa sababu helikopta ilipata hitilafu kidogo Jumatano mara baada ya kutua mjini Babati ikitokea eneo la Bashnet.

Habari na Picha na Mdau Asbert Ngurumo
 
Chanja mbuga baba tupo pamojaaaa........
Chadema (chama cha demokrasia na maendeleo)=penye demokrasia pana maendeleo
ccm (chama cha mapinduzi)=jembe na nyundo miaka hamsini baada ya kujitawala/kuwa huru
cuf (civic united front)=maandamano na udini zaidi/wakati huo huo haki sawa kwa wote
 
Huu ni uttitiri wa watu............... kama kweli wanamapenzi naye na wamejiandikisha basi wampigie kura.

25ssmcg.jpg
 
Ata farasi tumia baba ili mradi haudhuriki tuu!
 
rose kamili anauvumilivu na ni mwanamke wa kuigwa
Hapa imekata kabisa maneno ya yule mropokaji Makamba kuhusu ndoa ya Slaa. Kasoro anazoziona Makamba ziko wapi tena? Mambo yao ya ndani wanayamaliza wenyewe lakini katika upambanaji wako wote na wananchi. Safi sana na ni mfano wa kuigwa huu.
 
Tupo pamoja mzee wa umakini Dr Slaa. Gooo.... Gooooooo dr
 
Huu ni uttitiri wa watu............... kama kweli wanamapenzi naye na wamejiandikisha basi wampigie kura.

25ssmcg.jpg

Inawezekana hao wote wana mapenzi na Dr Slaa lakini pia inawezekana ndio sinema za kule vijijini. Kukiwa na kitu chochote watu wanajazana kwenda kusafisha macho.

Hatuwezi kujua ukweli mpaka tarehe 31 Oktoba.
 
Nenda Slaa neda...sisi Vijana tupo na tutakupigania daima..2010 hatudanganyiki...!Hakuna kulala mpaka kieleweke...!
 
Aaahh,haiogopeshi hiyo!
Rejea enzi za Mrema mwaka 1995,alibebwa na kusukumwa kwenye gari,lakini akalamba patupu.
Je Mrema wa kipindi hicho na Dr. Slaa nani zaidi?
 
Katika sehemu zote alizopita watu walikuwa wengi sana. Japo umeme kwa ajili ya matangazo ya Dr Slaa uliounganishwa kutoka ofisi ya CCM ulikatwa mara tu alipoanza kuzungumza. Watu wanajiuliza ni nani aliyetoa agizo hilo kwani makubaliano yalikuwa yamesha fanywa? Wengine walikuwa wanasadiki kuna kibosile kimoja cha CCM humo ndani amejifunika mgorori akipeep chini ya pazia la dirisha. Msamaria mmoja alijitolea ka spika kake ka betri kabla ya majirani na CCm kutoa msaada
 
Mbona TV hazituonyeshi haya, jamani
Wanasubiri hadi Slaa akosee kutamka jambo ndipo TBC wataonyesha lakini kama anashusha sera hutawaona, juzi Zitto kajichanganya ndipo tukajua kumbe TBC walikuwepo Kigoma lakini wakati Zitto anaelezea maendeleo ya jimbo lake walikuwa wala hawaonekani.
 
Inawezekana hao wote wana mapenzi na Dr Slaa lakini pia inawezekana ndio sinema za kule vijijini. Kukiwa na kitu chochote watu wanajazana kwenda kusafisha macho.

Hatuwezi kujua ukweli mpaka tarehe 31 Oktoba.

Nenda mikutano ya sisi m kama utawaona pamoja na kuwakusanya toka vijijini. Hawafikii idadi hii bwana. Nani anataka kupoteza siku yake kwa kusikiliza same story mwaka hadi mwaka? Wanapewa ahadi ya maisha bora kisha maisha bora yanaishia kwa wakina Chenge na Rostam na Lowasa na best wao Kikwete?

Tarehe 31.10.2010 watakuwa hivi hivi. Nyota imeng'ara
 
TBC wamekuwa wapo bias kwa ajili ya kuonyesha habari za mkutano ya Slaa
 
TBC wamekuwa wapo bias kwa ajili ya kuonyesha habari za mkutano ya Slaa
bwahahahahaha Kikwete alipopumzika na wao wamekwenda likizo. Utadhani TV ni mali ya Kikwete. Yaani walivyo wajinga wanashindwa hata na Dialo ambaye anatumia vyombo vyake si kwa faida yake tu bali kwa faida ya umma pia. Huwezi kukuta kila siku yuko kwenye headline za vyombo vyake vya habari.
 
Mbona watu niwachache sana ?

Nadhani angehubiri kanisani au kutangaza neno la Mungu angepata watu na wafuasi wengi zaidi !! Kwanini usirudi kanisani Mchungaji ? au sheria za kukukataza kuowa zimekufanya uache kanisa ?
 
dr slaa alivyounguruma hanang na mbulu.

Saturday, September 4, 2010

Dk Slaa anamtambulisha mgombea ubunge wa Hanang, Rose Kamili, katika eneo la Endosak, jirani na nyumbani kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye.
Umati Mkubwa ulijitokeza kumlaki Dk. Slaa katika eneo la Haydom, jimboni Mbulu.
-----------------------

Dk. Slaa ameiteka Manyara.Na wananchi wa Manyara wamemteka pia.Ilikuwaje? Kwanza, walijaa katika mikutano yake katika majimbo ya Hanang na Mbulu.Pili, walizuia misafara yake kokote alikopita wakitaka awahutubie, walau kwa dakika moja tu! Tatu, walimwahidi kufanya mabadiliko makubwa mwaka huu kwa kuchagua wabunge na madiwani wa Chadema, ili kukifanya CCM kuwa chama cha upinzani. Kipya ni kwamba alitumia usafiri wa Kipanya (Hiace) badala ya helikopta kutoka Babati hadi Mbulu, kwa sababu helikopta ilipata hitilafu kidogo siku ya Jumatano mara baada ya kutua mjini Babati ikitokea eneo la Bashnet.Habari na Picha na Mdau Asbert Ngurumo.

 
Wateule wa Viti Maalum CCM wakiona haya nadhani presha inakuwa ikoo juu. Wangapi wateuliwe inategemea idadi ya kura za raisi
 
Mbona watu niwachache sana ?

Nadhani angehubiri kanisani au kutangaza neno la Mungu angepata watu na wafuasi wengi zaidi !! Kwanini usirudi kanisani Mchungaji ? au sheria za kukukataza kuowa zimekufanya uache kanisa ?

Ha ha ha wewe Bull, mwone daktari wa macho, huoni watu? Macho yako yana 'drop effect'
 
Back
Top Bottom