Hapo unaendelea kuwapeleka shimoni. Vitu visivyohesabika ni mchanga, maji na mwazo yasiyoisha (infinity continuity). Kama wewe ni mtaalamu wa lugha hasa kiingereza hebu weka mapendekezo yake katika lugha halisia ya 'Wales' (Native English) ili somo lieleweke vema kama mfano katika utungaji wa sentensi Uwezo mzuri wa kuongea au kuandika kwa kutumia lugha ya kiingereza kunategemea kuwa ni sharti iwe ndio lugha yako ya kwanza kwa mawasiliano na kufikiria badala ya kutumia kimatengo kufikiria unahamishia kwenda kiswahili kisha ndio unapeleka namna ulivyofikiria, kuelewa, kutafisiri na kuamua hicho kilichojitengeza ndio kinapaswa kuzungumzwa. Ni bora wakati unaandika unaweza ukatumia 'proofreading' grammar and spelling correction' kupiga msasa ujumbe wako.
Tatizo ni kwamba ni lugha yako ya kwanza ambayo hata mama na baba walikukuza kufanya mawasiliano ya siku kwa siku. Pili lugha hiyo ndio unayotumia kufikiria, kuelewa na kutafsiri kabla hujatamka au kuandika?
Native English
A "native speaker of English" refers to someone who has learned and used English from early childhood. It does not necessarily mean that it is the speaker's only language, but it means it is and has been the primary means of concept formation and communication.
Katika nchi za Afrika Uganda ndio inaongoza kwa watu wake kuongea kwa kiingereza fasaha ijapokuwa kinaharibiwa na lafudhi ya makabila yao.
Afrika Kusini inayofuatia kwa kuongea kiingereza fasaha kiasi, kasoro lafudhi ya kikabila na kiiafrikaner
Inayofuata ni Nigeria ijapokuwa nao lafudhi na maneno ya kienyeji huchanywa sana
Malawi, Zambia na Zimbabwe ziko kwenye nafasi sawa kwa kuongea kiingereza kinachoshabihiana, kilichonyooka na ufasaha kiasi
Kenya wanaongeza kwa kujiamini lakini hakina ufasaha wa mzizi wa lugha halisia kutokana na majivuno na athari za lugha za kienyeji
Tanzania haiko kwenye kumudu matumizi ya lugha ya kiingereza kama taifa kutokana na kufikiri, kuelewa na kutafsiri kwa kutumia lugha ya mama na Kiswahili kisha kutafsiri neno kwa neno kwa mfuatano wa maneno katika lugha ya kiingereza hivyo kupoteza mantiki. (watu wachache sana ama waliosoma wakati nchi inapata uhuru au walienda nje kusoma au kufanya kazi kwa muda mrefu kisha kurejea hao kwa vyotevyote vile huko walikokuwa walikuwa wanafikiri, kuelewa na kutafsiri kwa kutumia lugha ya ughaibuni.