Dkt. Allan Kijazi, Katibu Mkuu Maliasili na Utalii na DG TANAPA - Confusion

Dkt. Allan Kijazi, Katibu Mkuu Maliasili na Utalii na DG TANAPA - Confusion

Nduka Original

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2010
Posts
1,012
Reaction score
817
Dkt. Allan Kijazi ni Director General wa Tanzania National Parks na wakati huo huo ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na utalii. Kabla ya hapo alikuwa Naibu Katibu Mkuu na Mh. Samia Suluhu akam-promote kuwa Katibu Mkuu akichukua nafasi ya Aloyce Nzuki.

Kwanza mimi nampongeza kwa uteuzi ila naona kama kuna mgongano wa kimajukumu.

1. Moja ya kazi za Katibu Mkuu ni kusimamia taasisi zilizo chini ya Wizara yake kama accounting officer wa Wizara husika ambapo ana deal moja kwa moja na CEO's wa haya mashirika.

2. Kwenye kuunda Bodi za mashirika baada ya Mwenyekiti kuteuliwa na Rais basi wajumbe wote huteuliwa na Waziri kwa kushirikiana na Katibu Mkuu wa Wizara na wataalamu wengine.

SWALI: Sasa hapa inakuwaje Dkt. Kijazi aendeshe Shirika kama TANAPA then kwenye vikao vya Bodi aingie kama mjumbe/Katibu ambae ndio DG na pia Ex-officio kama Katibu Mkuu halafu akawe questioned na wajumbe ambao yeye amehusika kwenye kuwateua?

Lakini pia CEO wa shirika ndiyo anaye-present report ya Shirika ambapo wakati huo huo ni Katibu Mkuu.

Hii imekaaje wadau?
 
Sasa Kama Hakuna Watanzania wengine walio “Clean na Smart” unatakaje?
Alienacho Huongezewa...
 
Dr Allan Kijazi katibu Mkuu Maliasilia na Utalii na pamoja na awali kuwa DG TANAPA,angekuwa ni Mzigo taasisi aliyokiluwa anaisimamia kuweza kusaidia miradi ya kujamii kwenye vijiji vinavyozungukwa na hifadhi za taifa. Mfano ukarabati wa shule za sekondari na primary ,barabara, miundombinu ya maji, dispensary.

Tanapa imekuwa mzigo kwa vijiji na jamii zinazoizunguka hifadhi za taifa. Sasa tembo wameanza kuuwa wananchi na wananchi wanateseka kutafuta fedha za ukarabati wa shule za watoto wao bila msaada wa tanapa Wala wizara anayoisimamia yeye.

Ni wakati sasa tanapa isaidie miradi ya elimu, afya, maji na barabara kwenye maeneo hifadhi za taifa zinazoizunguka vijiji husika.
 
Kwani yuko peke yake? Mbona hata Msigwa ni Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu wakati huohuo ndio msemaji mkuu wa Serikali ,kuna wengi kweli nchi hii
 
Nasikia TANAPA kuna DG mpya anaitwa Mwakilema huyu alikuwa muhifadhi mkuu wa Serengeti!

Mwakilema ni Deputy DG anaeshughulika Conservation na Community.
Structure ya TANAPA ina Deputy DG's wawili, mmoja wa conservation na mweingine wa corporate issues
 
Well said my friend!!!

Kwakweli hapo wakuu wa nchi wamebugi step.

Ili kuhakikisha kuwa kunakuwa na checks and balance kwenye Wizara na Taasisi zake lazima kusiwe na mwingiliano wa majukumu kwa namna yoyote ile.

DG wa TANAPA kumfanya kuwa KM wa Wizara ya Utalii haifanyi tu kuwa kutakuwa na muingiliano wa utendaji bali inaonyesha kuwa viongozi ni hamnazo i.e shule hakuna, hawajamsoma mwanafalsafa mfaransa aitwae James Montisque aliekuja na dhana ya separation of power and checks and balances na umuhimu wake ktk Utawala.

DG wa TANAPA anatakiwa awajibike kwa KM na baadhi ya majukumu anatakiwa awe assigned na KM na hata performance appraisal yake DG inatakiwa ipitiwe na KM kabla ya kwenda kwa aliyemteua kwa maana ya Mh. Rais, KM anatakiwa ashirikiane na Mh. Waziri kuteua wajumbe wa Bodi na kuandaa reports kwaajili ya Wajumbe wa Bodi ambao watatakiwa waipitie report yake na papo hapo KM anatakiwa kuwa Mjumbe wa Bodi.

Sasa unapomteua DG wa TANAPA kuwa KM wa Wizara ya Utalii inaleta confusion mbaya sana na kupelekea kama vile viongozi wetu hawajaenda shule kabisaaa!!!!

Tafadharini sana, tunaomba hilo jambo lirekebishwe haraka iwezekanavyo ili kuzuia kuzorota kwa utendaji kazi wa TANAPA na Wizara ya Utalii yenyewe.

Asante.
 
Afukuze wasaidizi na washauri wake!!! Wanajua kabisa jambo limekaa tenge halafu wananyamaza! Wanamtegea! Kosa siyo la mama!! Ni kosa la wasaidizi wake!!
 
..mimi nadhani hakuna confusion yoyote.

..baada ya Kijazi kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu, nafasi yake ya zamani itakaimiwa mpaka atakapopatikana dg mpya wa tanapa.

..kwa maneno mengine, kwasababu dg wa tanapa amepangiwa kazi nyingine na raisi, basi wizara, au bodi ya wakurugenzi wa tanapa, inatakiwa kuteua kaimu / acting dg atakayeongoza tanapa mpaka pale atakapoteuliwa dg mpya.
 
Back
Top Bottom