Pre GE2025 Dkt. Ananilea Nkya: Nafasi za ubunge wa Viti Maalum zifutwe kwa sababu zimeanza kutumika isivyostahili. Zilianzishwa ziwe za Mpito sio za kudumu

Pre GE2025 Dkt. Ananilea Nkya: Nafasi za ubunge wa Viti Maalum zifutwe kwa sababu zimeanza kutumika isivyostahili. Zilianzishwa ziwe za Mpito sio za kudumu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania, Dk Ananilea Nkya amesema nafasi za ubunge wa Viti Maalum zilianzishwa kwa kipindi cha mpito kutokana na uwakilishi mdogo wa wanawake.

Dkt Nkya amesema hali imebadilika tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 (miaka 42), wanawake wametumia nafasi hiyo ipasavyo huku lengo la kuanzishwa kwake kwa muda likikiukwa badala yake nafasi hizo zimeanza kutumika isivyostahili.

“Hivyo viti wanawake tulivipigania kweli kweli lakini viliwekwa kwa transition (kwa muda) kwa sababu wakati ule miaka ya 1970 hadi 1980 utafiti uliyoonyesha wanawake walikuwa wanaogopa kwa sababu mfumo ulikuwa unawanyima wanawake kufanya kazi nje ya nyumbani” amesema Dkt Nkya.

Dkt Nkya ambaye pia ni mwanaharakati wa masuala ya wanawake na watoto amesema uzoefu unaonyesha kuna udhalilishaji kwa wanawake wanaogombea nafasi za viti maalum ndani ya vyama vya siasa huku baadhi ya viongozi katika vyama hivyo wakivitumia kwa maslahi yao binafsi.

Ameyasema hayo leo Jumamosi Mei 25, 2024, wakati wa mdahalo wa wazi wenye lengo la kujadili mchakato wa kupata Katiba Mpya ya Tanzania ulioitishwa na Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS).

“Katika kuvipata inakuwa kwa mbinde wanavipata kwa njia ya unyanyasaji, ni wachache wanavipata kwa njia ya uhalali. Pia hawana fursa sawa na wabunge wa kuchaguliwa majimboni mfano nafasi ya Waziri Mkuu hawezi kuingia mbunge wa viti maalum,” amesema Nkya. Idadi ya wabunge wa viti maalum bungeni inafika 113 wanaoigharimu Serikali zaidi ya Sh200 bilioni kila miaka mitano ya uchaguzi, Dk Nkya amesema wabunge hao pamoja na kutowajibika kwa wananchi, pia wanaiingiza Serikali katika matumizi yasiyohitajika.

Pia amesema endapo wilaya zitageuzwa kuwa majimbo idadi ya wabunge itapungua kutoka wabunge 393 hadi angalau wabunge 276 huku ukiokoa gharama kwa Serikali ya hadi Sh200 bilioni zinazotumika kulipa wabunge wa viti maalum, fedha inayoweza kugharamia Bima ya Afya kwa watoto chini ya miaka mitano.

Naye Mchambuzi wa Masuala ya Kisiasa, Deus Kibamba, mwarobaini wa changamoto ya viti maalum bungeni itaondolewa kwa kuanzishwa kwa mchakato wa Katiba Mpya, mchakato alioutaja kwamba utaondoa mambo yaliyopitwa na muda.

Ili kufikia suala hilo, Kibamba amesema Katiba itakayoanzishwa inatakiwa kuja na mapendekezo ya kufumua na kupunguza mamlaka ya Rais ikiwemo ya kiuteuzi na kuyarejesha kwa wananchi huku akidokeza kwamba ili suala hilo lifanikiwe halihitaji utashi wa kisiasa bali kijamii.
Mwenyekiti wa TLS Kanda ya Ziwa, Steven Kitale ameshauri kuanzishwa Katiba ambayo inashughulikia mapungufu ya kisheria yaliyopo katika taasisi za nchini likiwemo Bunge.

“Mapendekezo haya yatasaidia kujenga msingi imara ya Katiba inayozingatia matakwa ya wananchi na kuleta mabadiliko chanya katika jamii yetu. Ni rai yetu kwa Serikali na viongozi wetu kuyazingatia ili kuwapunguzia wananchi mzigo na kurejesha uwajibikaji katika kodi inayotolewa na wananchi,” amesema Kitale.

Huyu ndiye Iron Lady wa ukweli
 
Ukweli hivi viti maalum ni mzigo kwa uchumi wa Taifa.
Kwa kiingereza tunasema:
She is very right.
Yuko sahihi na wanawake wengi wangekimbilia kwenye majimbo hasa wa upinzani kama uchaguzi ungekuwa wa Haki na Huru.Viti maalum ni matokeo ya uchafuzi wa uchaguzi kuua hilo lazima haki itendeke
 
Mbona rasimu ya Warioba ililiaddress vizuri kabisa hilo suala la VITI MAALUM..kila mkoa Wabunge wawili..wajimbo( mkoa) na viti maalum na wote wa wagombanie..

Shida nchi yetu tunapeleka fedha nyingi kwenye UTAWALA..kwa mtazamo huu maendeleo ya Mama Tanzania, yatakuwa ya KUSUA SUA
 
Back
Top Bottom