Dkt. Bashiru: Aliye na dola ndiye ananufaika nayo kubaki madarakani, hata CHADEMA ikiingia madarakani ikaondolewa kwenye dola ni uzembe wao

Dkt. Bashiru: Aliye na dola ndiye ananufaika nayo kubaki madarakani, hata CHADEMA ikiingia madarakani ikaondolewa kwenye dola ni uzembe wao

Nasema tena ,Polisi na jeshi ndo wakumuomba Bashiru asahihishe kauli yake Wakinyamaza ina maana kuwa wako pamoja juu ya maneno yale.

Kimya chao kinatupa sisi wananchi wasi wasi na kuonesha kuwa hamna siasa nchii hii ,utawala ni wa kiiimla.
 
Inawezekana bashiru kakutana na hali inayomkera, akaamua kutamka maneno yanayoonyesha hali halisi, alafu tatizo likawa kwa wapokeaji, sisi ni wepesi sana wa kutoa hukumu bila kutafakari.

Nafikiri muhimu ni kujiuliza nini kimejificha nyuma ya kauli yake, tusiwe wepesi sana kutoa hukumu, yawezekana hata yeye anaishi katika mazingira asiyoyaopenda,

Je, tunajua ni nani yupo nyuma ya yote yanayotendeka?
 
the truecaller, Huo ndio uelewa wako Dola aliyoimaanisha Bashiru ni pamoja na vyombo vyote vya ulinzi na usalama pole kwa maandishi yako marefu yenye upotoshaji.
 
Hukuona kilichotokea zanzibar 2015?Hiyo ndio maana ya dola!Au pia muulize kafulila,jumla ya kura zilionesha yeye ndiye kashinda lakini mkurugenzi kamtangaza yule mama wa CCM ndiye mshindi,alihangaika na ushahidi mahakamani akapigwa kalenda mpaka akachoka,wakaona wampe ofa ajiunge nao kisha apewe shavu!Hiyo ndio maana ya alichokisema Bashiru!
Na huu uchaguzi wa serikali za mitaa ni kiashiria kingine cha alikuwa na maana gani. Kuanzisha wasimamizi mpaka wote
 
Bashiru tutatumia DOLA.


"Wanaosubiri sisi tulegelege kwenye kutumia dola kubaki kwenye dola watasubiri sana, hata Trump kumuondoa ngumu, kuna nafuu kubwa na faida kubwa chama kilichopo madarakani kutumia nguvu za dola kufanya mambo ya kujenga imani kwa wapiga kura ili kiweze kubaki madarakani"- Bashiru

"Aliye na dola ndiye ananufaika na dola ile kubaki madarakani, huo ni ukweli na hata CHADEMA ikiingia madarakana ikaondolewa kwenye dola ni uzembe wake. Kwasababu ana nafuu na faida ya kuendelea kubakia" - Dkt. Bashiru Ally, Katibu Mkuu
 
Chama cha Mapinduzi kinatumia vizuri Sana dola ili kuendelea kubaki kwenye dola na Rais Magufuli ametusaidia sana kwenye hilo.

Msikilize Dk. Bashiru Ally Kakurwa akifafanua kwa kina dhana ya chama tawala na matumizi ya dola kubaki kwenye dola

 
serikali bila watu ni sawa na chakula pasipo mlaji...tukiwachangamkia bado morali ya watanzania ni kubwa juu ya lissu na chadema kwa ujumla hakika watang'oka

#kura yangu kwa lissu, ole wako lisu ukubali ku- sign baada ya meko kushinda walahi tutaonana wabaya sana.
 
Ccm mlibugi wenyewe kutowaheshimu watanzania. Hasa huyu black wenu wa Sasa, mtulie tuliiii. kinyozi ananoa wembe taratibu
 
Mwaka huh nguvu ya umma ndio itayotumika ,ambayo ndio kiboka ya nguvu za fola za aina yoyote ile ,muulize Likasheko?
 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ali, amekiri chama chake kuitumia dola kuhakikisha kinabaki madarakani.

Amesema kama chama chochote kinachoongoza serikali kitashindwa kutumia dola kubaki madarakani, utakuwa uzembe wa chama chenyewe. Kwa kulitambua hilo, Dk. Bashiru amesema CCM imekuwa ikitumia dola kujihakikishia ushindi wakati wa uchaguzi na mwaka huu wamepanga “kuitumia dola kweli kweli”.

26AB45D8-A622-4F5D-A664-908B58A7CF9F.jpeg
 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ali, amekiri chama chake kuitumia dola kuhakikisha kinabaki madarakani...
Dola na nguvu ya uma wapi na wapi..! Kwaio wako radhi kurusha mabomu ya kivita mtaani sio...

Haya sawa tushajua hilo na Mungu pia yuko upande wetu siku zote mpaka haki ipatikane..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Bashiru Ally akifanya mahojiano na kituo cha utangazaji ITV amenena haya kuelekea uchaguzi Oktoba 2020.


HOTUBA KWA UFUPI


CCM imejiandaa kushinda kihalali, na ushindi wenyewe sio wa Oktoba, ulianza kutafutwa tangu 2015,hiyo ndio tiketi yetu

Tatizo kubwa tulilokuwa nalo katika nchi yetu wananchi walishaanza kupoteza imani katika mchakato wa uchaguzi, na kuna wakati tumefikia hatua ambayo wanaojiandikisha idadi yao inakuwa kubwa lakini wanaojitokeza kwenda kupiga kura idadi inapungua hilo si jambo zuri.

Nasikia watu wanasema uchaguzi uwe huru na haki,lakini lazima tupanue tafsiri ya haki,eneo kubwa ambalo tunahitaji kuwekeza nguvu zaidi ni ushiriki wa vijana na akinamama,haya ni makundi ambayo mara nyingi hutumika na wanasiasa lakini hayanufaiki na jasho lao.

Hakuna atakayeteuliwa ndani ya CCM hasa waliyopo madarakani, bila kwenda kwenye rekodi ya utendaji wao..hakutakuwa na uteuzi wa bure.

Ukishika mbili zote zinaweza zikachomoka, aliye na dola ananufaika na dola hiyo kubaki madarakani, huo ni ukweli hata CHADEMA ikiingia kwenye dola kuiondoa kwenye dola utakuwa ni uzembe wake kwa sababu ana nafuu na faida yakuwa na dola.

Ninachoomba mimi wanasiasa wenzangu wafate sheria,maelekezo na taratibu,kwasababu nchi hii tukigeuza kuwa wakati wote ni kusema chochote na kufanya chochote..tutatafutana,ni vizuri tukawa na utaratibu wa kutujengea nidhamu.

Ni shabaha yetu kufika 50/50 lakini ni safari ndefu na ngumu lakini tutafika, hakuna kurudi nyuma, kwa ufupi ni mapambano.

Mchakato wa katiba mpya ni kiporo kilichochacha, ukila utaumwa matumbo.

Wanaosubiri sisi tulegelege kwenye kutumia dola kubaki kwenye dola watasubiri sana, hata Trump kumuondoa ngumu, kuna nafuu kubwa na faida kubwa chama kilichopo madarakani kutumia nguvu za dola kufanya mambo ya kujenga imani kwa wapiga kura ili kiweze kubaki madarakani. Aliye na dola ndiye ananufaika na dola ile kubaki madarakani, huo ni ukweli na hata CHADEMA ikiingia madarakana ikaondolewa kwenye dola ni uzembe wake. Kwasababu ana nafuu na faida ya kuendelea kubakia.

Ukidhulumu mtu nikajua natafuta dola ishughulikie mtu aliyedhulumu ili nibaki madarakani, na kwakweli zamu hii ninahakika ya kushinda uchaguzi kwa sababu nitatumia dola barabara.

Ninachojua mimi hakuna mikutano iliyozuiliwa,na Polepole ni Katibu wa Itikadi na Uenezi anatangaza tuliyoyafanya ili CCM isiondolewa madarakani,sasa unataka ayatangazie wapi,chumbani?

Ilani sio Msahafu, inaweza kutekelezeka kwa kiwango fulani na si lazima iwe asilimia 100.

Hii hali ya kisiasa mnaiona,na vyama vyetu mnaviona,hivi kuna tishio ya ushindani wa kufa na kupona katika nchi hii,kiasi ambacho tuwe na uoga kwamba hautakuwa huru na haki?,mimi ntamuibia nani ana nini huyo?

Sitaki kufanya siasa za propaganda hapa, timu mnaziona? unaweza kabisa kuona ni timu gani itafunga mabao mengi? Katika mazingira ambayo kuna ushindani mkali ndio tahadhari inatakiwa kuchukuliwa,sasa jamaa anapigwa hadi mechi za mazoezi,unawasiwasi gani na refaa?

Dkt.Magufuli ametusaidia sana, kutumbua majipu, kusimamia serikali, kudhibiti matumizi mabaya ya pesa, tumetumia vizuri dola kubaki madarakani, kukusanya kodi dola hiyo hiyo ndio tunayoitumia, tulikuwa kwenye bilioni 800 sasa hivi tuko above trilioni 1


----
MAONI YA MDAU
Nimechanganyikiwa kabisa, Kumbe nguvu ya CCM Ni Dola? Katibu wetu mkuu apunguze kuongea Sana kwenye vyombo vya habari.

Kumbe Upinzani unapambana na Dola na CCM kwa Pamoja? Kwa hiyo CCM Haina Tena ushawishi wa kuchaguliwa bila Kutumia Dola?

Vidole vyangu kataa kuandika zaidi utakosea ngoja tu niishie hapa, ila Katibu mkuu naomba anaki zaidi kwenye shughuli za Operations hizi Media amwachie Polepole. Hii statement yake nimekuelewa vibaya? Au ndivyo anavyomaanisha?

Ndio naelewa ile kanuni ya RPC Arusha kuwa kama A=B na B =C basi C =A. Hapa alikuwa anaonyesha uhusiano uliopo Kati ya jeshi la Polisi na CCM. Kuna Mambo ya kuongea hadharani na Mengine Chumbani

Ole Mushi
0712702602

Asante. Nilikuwa natafuta uzi huu sana. Nitaufanyia kazi next time. Kwa leo nataka nifanye kitu kingine.
 
Back
Top Bottom