Uchaguzi 2020 Dkt. Bashiru Ally: Mgombea wa Urais ndani ya CCM ambae anaendelea hajawahi kupingwa

Uchaguzi 2020 Dkt. Bashiru Ally: Mgombea wa Urais ndani ya CCM ambae anaendelea hajawahi kupingwa

craq

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2017
Posts
859
Reaction score
1,866
Saa Tisa alasiri kutakuwa na hardtalk mahojiano ya moja kwa moja kati ya Tido Mhando na Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally kupitia Azam TV.
=======

BASHIRU: Ajenda kubwa(Mkutano wa CCM Dodoma) ni kupiga kura kumteua mgombea wa urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, baada ya hapo kutakuwa na hotuba muhimu sana ya ufunguzi ya mwenyekiti wa chama cha mapinduzi. Hutuba hiyo itatoa muelekeo wa utekelezaji wa Ilani chini ya usimamizi wake.

Pia kutakuwa na taarifa ya serikali mbili zinazoongozwa na CCM, taarifa kuhusu utekelezaji wa ilani ya CCM tangu 2015 chama kilipopata ridhaa ya kuongoza serikali hizo mbili.

Kutakuwa na marekebisho madogo ya katiba ya chama ya mwaka 1977 toleo la 2017, marekebisho ambayo sehemu inahusu mabadiliko ya sheria ya vyama vya siasa vinalazimika kubadili katiba zake kukidhi matakwa ya kisheria.

TIDO: Umesema itapigwa kura kuthibitisha mgombea Urais wa CCM upande wa muungano, kwanini haifanyiki hivyo Rais wa Zanzibar, mkutano huu upokee maamuzi yaliyofanywa na vikao vya nyuma?

BASHIRU: Kwanza ni vizuri kufahamu, chama chetu kwa mujibu wa sheria za nchi, vyama vinalazimika kuwa na wanachama na uongozi katika pande mbili za muungano. Mchakato wa kumpata mgombea Urais Zanzibar huanzia kuchukua fomu, baada ya hapo uteuzi wa vikao huanza kuanzia kamati maalum ya halmashauri kuu ya Taifa, ni mchakato ambao upo kikatiba.

TIDO: Kumekuwa na kauli, Dodoma ndio inayochagua mgombea wa CCM Zanzibar badala ya wazanzibari peke yao. Ina maana kuna watu Bara wanahusika katika uteuzi huo, kwanini iwe hivi tofauti na ulivyozungumza mwanzoni?

BASHIRU: Kama nilivyosema, vyama vya siasa vinateua wagombea wa nafasi ya Urais kwa Jamhuri ya muungano na Rais wa Zanzibar kwa mujibu wa katiba zao na kwa mujibu wa sheria za nchi. Vyama vinamteua mgombea, vyama havimchagui Rais. Kinachofanyika ni mchakato wa uteuzi sio uchaguzi. Kwa hiyo hakuna utata wowote na katiba ya CCM kuna azimio la kuunganisha vyama vya TANU na Afro Shirazi, azimio la mkutano mkuu wa pamoja wa vyama hivyo na vyama vilikubaliana vitaunda chama kikubwa cha kimapinduzi na chama hicho makao makuu yake yatakuwa Dodoma.

Mchakato wa uteuzi hauwezi kuwa uchaguzi, uchaguzi unafanywa na wazanzibar.

TIDO: Kwa hio si kweli wale wanaosema huyu ameteuliwa kutoka Dodoma ambae baadae anakuja kuchukua nafasi ya juu sana katika serikali ya Zanzibar?

BASHIRU: Hao si wanaCCM kama wapo wanaosema hivyo, wanaCCM wanaamini katika utaifa na umoja. Ndani ya CCM hakuna Uzanzibari wala Utanzania Bara. Kama sio wana CCM sina hata ya kujadili mawazo yao, ndani ya CCM hakuna mawazo hayo. Katiba hairuhusu ubaguzi pia ndani ya CCM tunakuwa kama wanaCCM wanaoamini katika Utaifa.

TIDO: Wakati wa mchakato wa Zanzibar kuchukua fomu, wengi sana wamejitokeza mpaka kufika 32, ulionyesha kutofurahia Wazanzibari wengi kujitokeza, kwanini?

BASHIRU: Sikuwa nahangaika na idadi, nilikuwa nahangaika na utii wa kanuni na taratibu za chama hata wangekuwa wawili. Nilikuwa nawakumbusha upo utaratibu, tatizo sio wingi wa wagombea, tatizo sifa za wagombea, uwezo wao na mienendo yao ambayo inaweza kuhatarisha au kuimarisha umoja. Kila Rais wa CCM anapomaliza muda wake, wengi hujitokeza.

TIDO: Mpaka sasa majina matano ya Zanzibar hayajatangazwa rasmi, kwanini kumekuwa na usiri?

BASHIRU: Tunayo kanuni ya uongozi na maadili, katika vikao vyote maamuzi yote yanakuwa ya siri na yakihitajika kutangwazwa upo utaratibu, maamuzi yasioyohusu umma yanabaki kuwa siri, kuna utaratibu wa kutoa taarifa mpaka ngazi ya kutoa taarifa.

TIDO: Upande wa Jamhuri, inafamika ni mgombea mmoja tu ambae amepita bila kupingwa, atapigiwa kura ya yeye peke yake. Katiba inasema wanachama wanayo nafasi ya kujitokeza kugombania tiketi ya CCM kwenye Urais. Kwanini kauli ya mazoea(desturi) ina nafasi kubwa kuliko kipengele cha katiba?

BASHIRU: Maisha ya binadamu zina mambo yanayofanyika kwa mazoea au maandishi ya kikatiba, hakuna mahala palipoandikwa mtoto amheshimu mkubwa au mtoto ampishe mkubwa kwenye kiti, ni swala la malezi, swala la mazoea. Katika CCM yapo yaliyoandikwa na yanafanya vizuri, yapo ambayo hajaandikwa na yanafanya vizuri. Katika hilo la mgombea wa urais ndani ya CCM ambae anaendelea tangu tumeingia mfumo wa vyama vingi hajawahi kupingwa.

Hili jambo ni Rasmi kwa mazoea lakini sio rasmi kwa maandishi ya kikatiba.

TIDO: Tathmini yenu hali itavyokuwa upande wa jamhuri ya muungano endapo kutakuwa na upinzani wa kutosha, mnaangaliaje uchaguzi wa mwaka huu ukilinganisha na 2015?

BASHIRU: Malengo ni kushinda uchaguzi wa aina zote, sisi hatuna tatizo la kufanya tathmini. CCM imekuwa ikishinda katika aina zote za uchaguzi. Katika chaguzi ambazo tumezifanya kati ya 2015 na 2020 tumeshinda chaguzi nyingi sana pia tumepokea wanachama wengi wapya na wanaohama.

Kwa upande wa Rais John Magufuli ambae mwaka 2015 alishinda kwa asilimia 58, tuna hakika kwa kazi kubwa aliyoifanya na uongozi shupavu atafanya vizuri zaidi pengine kuliko mgombea yeyote aliewahi kututetea katika uchaguzi wa vyama vingi.

Tuna hakika pia tutashinda uchaguzi wa urais Zanzibar na viti vingi vya uwakilishi, nilikuwa nawatania wapinzani, nikiwaeleza nafunga mitambo wengine wanabeza. Kwa uhakika na kujiamini mitambo sasa iko tayari kwa ajili ya kuleta ushindi.



 
Saa Tisa alasiri kutakuwa na hardtalk mahojiano ya moja kwa moja kati ya Tido Mhando na Katibu Mkuu wa CCM, Dkt.Bashiru Ally kupitia AzamTv.
Hakuna kitu hapo. Atauliza maswali yenye majibu ya kusifia serikali. Yeye mhoji haogopi? Tusubiri tusikie.
 
Aulizwe, " Kugombea kuongoza vyombo vya dola , maane yake nini? "
 
Utasikia anasema aulizwe maswali ya sera.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Saa Tisa alasiri kutakuwa na hardtalk mahojiano ya moja kwa moja kati ya Tido Mhando na Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally kupitia Azam TV.

😂😂😂 Hardtalk 🙈🙈
 
Atakua amemwambia,nikuulize maswali gani na yapi nisikuulize?

Dr. Bashiru ni intellectual, hawezi kufanya pre one-one meeting, yeye anaenda direct to one-one hard talk. Au unam under rate?
 
Swali la kipuuzi kabisa huwa hakuna mawazo ya maana chadema

Matukio yetu ni yakipuuzi kweli kwasababu wapuuzi mnao wengi ndani ya chama?

Hivi CAG tu kaweka maandishi hela hakuna zaidi Trillion 1.5 lakini kuna watu kama wewe wansema swali la kipuuzi?
 
Mahojiano na CCM Dola Magufuli hakuna cha maana hapo ni mazingaombwe tu.
 
Amuulize sera ya CCM ni kukwepa kuonyesha Athari za Ugonjwa wa covid 19
 
Back
Top Bottom