Dkt. Bashiru anatoa wapi ujasiri wa kutishia 'usalama' wa viongozi wa juu? Huu ni uhaini sio ukosoaji. Je, ana mahusiano na mataifa ya nje?

Dkt. Bashiru anatoa wapi ujasiri wa kutishia 'usalama' wa viongozi wa juu? Huu ni uhaini sio ukosoaji. Je, ana mahusiano na mataifa ya nje?

Kukosoa kutokana na changamoto na matatizo na kuishauri serikali na viongozi sio jambo geni.

Ila inastaajabisha kuona mtu kama Bashiru anatishia Usalama wa kiongozi wa nchi. Anaongea kwa kujiamini mbele ya kadamnasi na vyombo vya habari kuwa Usalama wa viongozi hauko na uhakika na watishwe. Ni kana kwamba hii nchi iko mikononi mwake na haogopi vyombo vya sheria na dola (ambavyo aliwahi kudai angetumia kubaki madarakani utawala uliopita)

Lakini pia anachofanya ni kuchochea mapambano, uasi, na matumizi ya njia za kuumizana katika mifumk yetu ya kidemokrasia. Maandano ndio kitu kikubwa Tanzania kimewahi kufanyika na kuogopwa lakini sio KUTISHIA USALAMA WA VIONGOZI

Kwa hali ya kawaida mtu ambaye ni mgeni katika chama na kuhudumu katika serikali kwa muda mfupi kuwa na kiburi cha kutishia Usalama wa kiongozi wa nchi bila woga

Tumeshaona viongozi kadhaa wa upinzani tangu tunapata uhuru waliosumbua lakini hakuna ambaye amewahi kutishia Usalama wa Kiongozi wa nchi.

Tusilitazame ili jambo au kauli katika jicho la kisiasa tu

Nani yuko nyumba ya Bashiru? Je, ametokea kuropoka yaliyokuwa moyoni mwake siku zote au alidhamiria kuyatoa ? Kuna nguvu ya nje ya Tanzania yetu anayojivunia? Ana asili ya Uraia nje ya Tanzania?
Mbona mmeingiza baridi hivyoo? Semeni anatumiwa na Cia ila jomba anahoji tu kama mtanzania, sasa sijui ni dhambi au siyo utamuduni kuhoji?
 
Mbona unaandika kama unakimbizwa?
Alitishia kivipi mbona huweki maneno aliyotishia nayo?
Unajua kutishia au unakurupuka tu?
Ni vyema uwe unashikirisha akili wakati wa kuandika kukurupuka!
 
Back
Top Bottom