Tetesi: Dkt. Bashiru kupewa Ukatibu Mkuu Kiongozi,mkakati wa kumnyamazisha dhidi ya kuongeza muda wa Urais?

Tetesi: Dkt. Bashiru kupewa Ukatibu Mkuu Kiongozi,mkakati wa kumnyamazisha dhidi ya kuongeza muda wa Urais?

kipumbwi

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2015
Posts
3,162
Reaction score
9,073
Wanabodi,wengi watakua wameshtushwa na uteuzi wa Dr. Bashiru ambae ni Katibu Mkuu wa CCM kupewa wadhifa wa Katibu Mkuu Kiongozi,ila sidhani kama jambo hili limefanyika kwa bahati mbaya!!!

Kabla ya yote naomba turejee sakata la raisi Magufuli kutajwa tajwa kuwa yupo mbioni kubadili katiba(haswa baada ya wabunge wake kama Juma Nkamia,Mzee Kesi,Deo Sanga na hata Spika Job Ndugai kushupalia kuongezwa muda ndani ya bunge!!

Baada ya maneno hayo,ni Dr Bashiru ndio alikua mtu wa kwanza kutoka hadharani kukanusha na kusema raisi Magufuli hatoongeza muda na ataondoka mara moja muda ukiwadia!!

Kwa kauli za Bashiru walau watu walizibeba maana alikua anasimama kama mtendaji Mkuu wa CCM!!

Kikichotokea ni kumuondoa kwenye utendaji Mkuu wa chama,hii ni dhahiri imezima kauli zake za kupinga Magufuli kuongezewa/kujiongeza muda na hii itapelekea Katibu Mkuu mpya wa chama kupatikana ambae atakua mgeni na hatokua na msimamo wa kupinga zike kauli za "atake asitake tutamuongezea"

Kufupisha maandishi ni kua,teuzi ya Katibu Mkuu ni maandalizi rasmi ya kukaa madarakani muda mrefu,kwa kumtoa aliekua akipinga wazi wazi na kumweka karibu na Ikulu ili ale matunda ya Ikuku na ajione na yeye bi sehemu ya Ikulu ili wadumu wote muda mrefu Ikulu na pengine akijaribu kumhadaa kua atamuachia nchi kwa kale kautaratibu ketu- mkristo-muislamu!!!

Naomba pia tufanye rejeo kwa clip hii hapa chini!!
 

Attachments

  • VID-20210226-WA0004.mp4
    5.1 MB
Bashiru kusema vile ni sehemu tu ya mkakati Kama kweli Wana nia hiyo na haikuwa tatizo lazima kuwe na upinzani wa kuwahadaa watu kupitia watu aina ya bashiru lakini usipofikiri vizur huwezi kuona

Ikiwa unabisha nitajie mtu mmoja ambaye anaweza kuwa na msimamo tofauti na mkuu tukiacha hiyo ya maoni ya viongozi mbalimbali kuhusu kuongezewa mda
 
Umejuaje na ulitaka iweje na nani kakwambia? Who is Bashiru by the way ukiachia mbali kuwa mbwabwajaji na mjikombaji mchumiatumbo?
 
Wakati wa utawala wa Mobutu wanafunzi wa vyuo vikuu waliandamana kupinga his absolute power. Matokeo yake viongozi wa mgomo waliuliwa na maiti zao kutupwa mto Congo wakaliwa na mamba. Wengine walifungwa, vyuo vilifungwa na wanafunzi wote walipelekwa kesho ni. Baada ya mafunzo ya kuruta walikula kiapo cha utii wa rais.
 
Wateuliwa wote wanachokisema majukwaani usidhani ni bahati mbaya bali ni maelekezo, hata ukiona kila anayesima lazma amtaje jpm hata pasipo na sababu ya kumtaja jua ni maelekezo, kwahiyo Bashiru kusema vile yalikuwa ni maelekezo na angekuwa kajituma sidhani kama angevumiliwa mpaka leo, sema aliyeleta ukakasi juu ya jambo hilo ni Polepole aliposema Rais hana mpango wa kuongeza muda ila hawazui wananchi kujadiri jambo hilo.
 
Huyu baba akiondoka wengi wataumbuka. Wanatenda kana kwamba watakufa kesho na wala historia itafutwa kwenye vichwa vyetu.
 
Miaka yetu hapa duniani ni 70, ukiwa mwenye nguvu ni 80, nayo ni kwa mateso makubwa. Na raha za dunia zipo nyingi, kila mtu hujichagulia imfaayo. Kama kutawala daima ndio chaguo, msiwazuie, utawadia wakati wataondoka na dunia itasonga mbele.
 
Na hapa ndipo nawaza kifo cha Maalim Seif, Huyu lazima angewashawishi Wazanzibari waikatae move ya kubadili katiba ili mtu fulani ajiongezee muda. Kwa sababu zinahitajika theluthi 2 za Wabunge wa Zanzibar na pia kama ingefanyika referendum ya kuhusisha wananchi basi Maalim alikuwa na ushawishi wa kuwafanya Wazanzibar wakatae hilo labda kama wangelazimisha kwa kuiba kura
 
Back
Top Bottom